President of China
JF-Expert Member
- Dec 6, 2018
- 31,548
- 89,516
- Thread starter
- #61
Taarifa ikishatoka ni wajibu wa msomaji kutumia zake kichwani azichakate vizuri. Kipindi cha Nyerere taarifa kama hizi zilipokuwa zikitolewa, watu walikaa na kuanza kuzichakata kisha kuzijua kwa undani zaidi.Conspiracy theories zitakuja nyingi sana, na CCM ndiyo ufundi wao upo hapo. Journalism imeshazikwa Tanzania, ukitaka habari ya kweli Tanzania nenda BBC Swahili au DW. Nchi kwisha, ni baada ya miaka karibu 25 tangu Nyerere kuwakabidhi nchi Mbwa. Mtu mweusi hakuna kitu anachoweza. Uchawi tu
Mwalimu aliongea na kusema taarifa inatakiwa itengenezwe vizuri na iweze kumfaa mlaji. Inatakiwa ipikwe inukie na iweze kusomeka na kueleweka. Natumai kwa kigezo cha Mwalimu, taarifa yangu hii imetimia kwenye nyanja zote.
Imebaki sasa kwa walaji wasio na mihemko waisome kwa undani, waitafakari na kisha watafute ukweli.
Wajiulize maswali, je IMBEJU haipo? BBT haipo CHADEMA haipo? CRDB haipo, TADB haipo? 4U Movement haikuwepo?
Baada ya kupitia hatua kwa hatua kwa kutumia kanuni ya uandhishi wa habari, wengine waingie kwenye uchunguzi wa kina na waweze kuongezea palipopelea.
Lakini kuja kuipiga nyundo taarifa, kwa kuibeza huku ukilinganisha na vyombo vingine vya habari; ni kukosea kanuni za usomaji wa watu makini.
Ushauri; tumia muda wako kuunganisha dots zilizo kwenye andiko hili kisha utapata japo mbili tatu.
Asante kwa kunisikiliza. Ngoja nikapate supu ya uyoga