Mwenye uthubutu wa kuminya upinzani, kuwaamrisha majaji wawafunge wabunge wa upinzani. Kifungo cha Sugu uamuzi ulitoka juu.
Mwenye uthubutu wa kuikata budget ya CAG, aliyeshindwa kutoa maelezo ya T 2.5 zikowapi.
Mwenye uthubutu wa kuongea Kiingereza ambacho anakisikia na kukielewa mwenyewe.
Hii Myth ya trililion kuchotwa hazina bila idhini ya bunge kama ilivyoletwa na Zitto mimi sijawahi kuona ushahidi wake. Katika kutuma lawama zake alidai ndege zilinunuliwa kinyemela bila idhini ya bunge, lakini ukipitia bajeti za Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi kwa miaka ya 2016/2017, 2017/2018. 2018/2019 utaonaona kuwa ununuzi wa ndege zote ulikuwa kwenye bajeti. Miradi yote ya ujenzi na uchukuzi imo kwenye bajeti; ni ajabu kuwa hata uwanja wa Chato ulikuwa kwenye bajeti na ikapitishwa na bunge lakini leo tunalalamika. Mbunge yoyote ana uwezo wa kusimamisha bajeti ya Wizara kwa kuondoa shilingi kama anaona kuna miradi haifai kutekelezwa; na inaonekana Zito naye hakuondoa shilingi yake kwenye bajeti zote.Siku hizi Zito amekuwa anarusha namba hewani ambazo hana ushahidi nazo, na kwa bahati mbaya sana baadhi yetu huchukulia matakamko yake kama kweli tupu hatuchukua muda kupima ukweli wake.Mwenye uthubutu wa kujichotea trillions hazina pesa za walipa kodi bila idhini ya Bunge. Mwenye uthubutu wa kudharau sheria na taratibu zote za Serikali afanye vile atakavyo yeye na mara nyingi kuingiza nchi kwenye hasara kubwa sana.
Mwenye uthubutu wa hivi ambao 99% of the times ni majanga na hasara kubwa HATUFAI KABISA na hastahili kuendelea kuwepo madarakani.
Sisemi kuwa watu wanakurupuka bali ninalosema ni kuwa madai hayo hayana ushahidi. Usifuate unaloambiwa na wanasiasa, wewe chukua muda usome documents halisi. Soma hotuba za bajeti za wizara ya uchukuzi na Ujenzi zote kwa miaka hiyo minne, halafu pia usome ripoti za ukaguzi kwa miaka yote minne. Soma mwenyewe, usipewe summary na mtu mwingine; ukitegemea summary utalatewa summary ya William Barr kuwa there was no collusion!Kasome ripoti ya CAG ya mwaka jana na mwaka huu pia. Wasikilize Wabunge wa upinzani. Watu hawakurupuki na kuandika vitu kutoka hewani.
Mfano kajichotea $495 millions bila idhini ya Bunge kwenda kununua ndege kwa cash, kisha kuigomea ofisi ya CAG isifanye audit ya pesa hizo. Pia kuna trillions zimechotwa na kupelekwa chato bila idhini ya Bunge.
Mtu anayejali maslahi ya nchi na pesa za walipa kodi iweje agomee ofisi ya CAG kufanya ukaguzi wa pesa husika!?
Hakuna sheria yoyote ile ya nchi inayompa mamlaka ya kugomea ofisi ya CAG kufanya audit zaidi ya kutumia udikteta na hofu kubwa ya maovu yaliyofanywa kuhusu pesa husika.
Zitto
Siyo kuwa nimekurupuka, kwani madai haya ni ya siku nyingi sana, na nimepitia nyaraka nyingi sana ili kupata ukweli wake, ndiyo maana nasema ni myth inayotokana na maneno ya Zitto. Wabunge wa upinzani hutoa hisia zao bungeni bila kuwa na ushahidi wowote, kwa mfano kudai kuwa ATCL haikukaguliwa kwa hiyo kuna jambo wanaficha kuhusu ununuzi wa ndege huku ikijulikana kuwa ndege hizo hazikununuliwa na ATCL bali zilinunuliwa na serikali; ATCL imekodishiwa tu. Kuhusu ripoti ya CAG yote niliisoma na yeye mwenyewe anasema kuwa 97% repoti za serikali zilikuwa perfect, 3% ndizo zilikuwa na ripoti zenye mashaka, na hapakuwa na hati isiyoridhisha. Hawezi kufikia conclusion hiyo kuwa hakuna hati isiyoridhisha iwapo kuna pesa zimechotwa kinyemela. Kuwa na hati yenye mashaka hakuna maana ya kuwa ni matumzi haramu, bali ni kutokuwa na record za kutosha kitaalamu.
View attachment 1172626
Kama pesa zingekuwa zinachotwa kinyemela namna hiyo halafu kuna matokeo tunayoona, basi ni wazi kuwa serikali zilizopita zilikuwa zinachota kwa vifaru.
Hiyo post nilliedit baada ya kupost lakini kumbe tayari ulikwishaikopiSiku nyingi sana zipi? Wakati ripoti za ofisi ya CAG zilizoweka bayana uchotwaji wa pesa bila idhini ya Bunge na pia kutojulikana kwa 1.5 trillion ambayo haijulikani imetumika vipi katika ripoti ya mwaka jana na mwaka huu 5 trillions ambazo hata kwenye mfuko wa hazina hazikuingia hazijulikani zimetumika vipi?
Kuna sheria inayompa mamlaka ya kuzuia ofisi ya CAG kufanya audit ya pesa za walipa kodi? Waliomtangulia hawajawahi hata mara moja kuizuia ofisi ya CAG kufanya audit ya pesa zozote za walipa kodi. Unadhani kwanini yeye kagomea audit ya $495 millions kununua ndege, pesa zote zilizopelekwa chato, 1.5 trillions ambayo haijulikani ilipo katika ripoti ya mwaka jana na 5 trillions haijulikani ilipo katika ripoti ya mwaka huu?
Bunge linatenga pesa halafu Wizara inasimamia; kwa hiyo madai ya kuchota pesa hazina kinyemela bila kupitishwa na bunge sasa tukubali siyo kweli.Uamuzi wa kuhamisha ujenzi wa airport kutoka Geita na kwenda Chato ulifanywa na nani na kuthibitishwa na nani? Unilateral decision ya Waziri au Rais? isnt that abuse of power? or rather deceiption?
Hatari ni kuwa hana Muda wakujenga BOLD and DARING Institutions( Kitu nachoamini akitaka anaweza na akiondoka tutamkumbuka kwa kujenga strong institutions) , yuko busy Kujijenga yeye.
Muda utasema.
Build strong institutions and being individually bold and daring aren't mutually exclusive. So personally I think he can continue with his leadership style only if the end game is to make the country and the institutions the country depends on stronger.
Duh...kuandika unapenda lkn ukiangalia matukio yanayotokea, ukaangalia watoto wako, mme...basi unasema ngoja nibaki kuwa msomaji walau nishuhudie wanangu wakikua...
Data utazitoa wapi hali watoa data wanabambikwa kesi? Kwa Mh.Kikwtw tulona kwa sababu watu waliruhusiwa kusema kile ambacho wewe unaona kilikuwa kibaya kwa wakati ule..hv sasa utapata habari kutoka serikalini tu hakuna chanzo chochote cha habari.
Tatizo si kuwa na habari za uhakika tatizo ni kuwa wenye madaraka hawataki kusikia wasichopenda...Najua unaelewa ninachomaanisha lkn unahamua kutwist twst maneno..uko kwenye hofu kama mimi lkn umeamua kutetea ili na wewe ushuhudie wanao wakikua kama mimi..
Hapo juu umesema kuhusu utawala wa Kikwete hizo data kuhusu utawala wa.Mh.Kikwete ulizitoa wapi? Ulizitoa kwa vyombo vyenye mamlaka? Au Kwa Mh.Kikwete ni sawa kwa Magufuli si, sawa?Tuwe na imani kuwa kuna vyombo vyenye mamlaka ya kutoa statistical data za serikali; iwapo unapewa data na serikali halafu unasema ni za uowongo wakati wewe huna mamlaka ya kukusanya data hizo, unaishia kujipikia data za kukufurahisaha tu lakini siyo realistic. Kwa marekani kila mwisho wa mwezi Wizara ya kazi hutoa data kuonyesha ni watu wangapi wampata ajira mwezi huo, halafu Wizara ya Biashara nayo hutoa maendeleo ya cuhumi kwala baada ya miwezi mitatu Trump alikuwa anapinga data hizo wakati wa Obama lakini leo anakubaliana nazo.
Sheria hiyo ya kudhibiti utoaji wa takwimu za serikari siyo nzuri kidemokrasialakini vile vile inapunguza upotoshaji usiokuwa na ushahidi. Kama hatuna imani na vyombo vyetu vya serikali kuhus takiwmu zake, basi hilo ni jambo tofauti kabisa.
Cool down; wewe pitia bajeti zote za serikali wakati wa Kikwete, halafu vile vile pitia bajeti zote za serikali wakati wa Magufuli; hazifichwi kama nilivyomuonyesha ndugu yangu BAK huko nyuma. Matumizi yote yaliyoko kwenye sehemu inayoitwa Recurrent Expenditure kwenye bajeti hizo ndiyo ambayo huingia mitaani, halafu yale ya Capital au Development Expenditure ndiyo yanayojenga miradi ya maendeleo. Matumzi haya yako wazi kwenye kila Wizara, ukitaka nitakutafutia lakini yako wazi kabisa. Kikwete alikuwa na recurrent expenditures kubwa sana kuliko capital expenditures, na kuna mara kadhaa Ofisi ya Rais ilikuwa inazidisha kiwango kilichoidhinishwa na Bunge kutokana na safari nyingi za nje ingawa hatukulalamika. Safari moja ya Rais ilikuwa inaongozan na ujumbe wa tu wengi sana ambao wote walikuwa wanalipwa allowances!.Hapo juu umesema kuhusu utawala wa Kikwete hizo data kuhusu utawala wa.Mh.Kikwete ulizitoa wapi? Ulizitoa kwa vyimbo vyenye mamlaka? Au Kwa Mh.Kikwete ni sawa kwa Magufuli si, sawa?