Huku Katoliki tuna ibada usiku!
Kanisa linakuwa gizani, waumini tunakusanyika nje!
Moto unawashwa na Padre wetu anaanza Sala takatifu za ufunguzi
Mshumaa unawashwa na tunaongozana kanisani, Padre anatangulia na mshumaa unaangaza kanisa ambalo lilikuwa gizani!
Kanisa kuwa gizani Ni ishara ya ulimwengu kuwa gizani kabla nuru iliyoletwa na Kristo kwa ufufuko wake!
Masomo Saba yanasomwa kutoka kwenye agano la kale!
Masomo haya Ni summary ya historia toka uumbaji, uovu wa mwanadamu na gharika kuu, utumwa wa Israel huko Misri, kuondoka Misri kuelekea Nchi ya Ahadi, Maisha ya waisrael nchi ya agano, na utabiri wa ujio wa Kristo kutoka kwa Manabii,
Baada ya masomo ya Agano la kale, mishumaa ya Altare inawashwa na somo moja agano jipya linasomwa
Kuwashwa mishumaa altareni, Mara baada ya masomo ya Agano la kale Ni ishara kuwa, Agano la kale limekamilika, Agano la watu walioishi gizani, na Sasa nuru ya Agano jipya limeingia ulimwenguni
Agano la Yesu Kristo!
Injili inasomwa na kisha mahubiri,
Baada ya Injili Ni shangilio kubwa la Pasaka! Yaani ufufuko wa Kristo Bwana wetu!
Kengele zinagongwa na nyimbo za shangwe zinaimbwa!
Hakika Kristo Yesu amefufuka Jumamosi usiku kuamkia Jumapili
Huko Yerusalemu, usiku wa Jumamosi ulikuwa wa giza kuu la huzuni kwa jamii ya wafuasi wa Kristo, kwani Yesu alikuwa amelala kaburini
Jumapili wakristo wale wakapata habari njema!
Yesu Kristo wa Nazareti, yaani Bwana na mwokozi wao, amefufuka!
Jumapili ile Ilikuwa furaha kwa wakristo wale, isiyokifani!
Jumapili ikatakatifuzwa, ikawa siku tukufu, siku yenye nuru kuu kwa wanadamu ulimwenguni, kupita siku zote!
Jumapili imewekwa kuwa siku ya kumshukuru na kumtukuza Mungu mkuu wa ulimwengu aliyetuokoa kwa njia ya mwanae Yesu Kristo!
Naona msabato amenuna!
Hakuna la kununiana hapa!
Mungu aliamuru kupumzika na kumtukuza siku ya Saba, na amri hio haikusema siku hio ya Saba Ni Jumamosi! Siku hii iliitwa siku ya sabato, na jumapili ikaitwa siku ya kwanza ya Juma!
Hapo kabla siku hazijatambuliwa kwa jina la jumapili, Jumamosi au ijumaa!
Hongera wakristo kushangilia na kuadhimisha kumbukumbu ya mateso na ufufuko wake Bwana!
Tumsifu Yesu Kristo!
Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app