The Bold Bulletins

The Bold Bulletins

Note: Kutokana na sababu za kisheria na mipango yangu binafsi nimeona ni vyema nikitumia jina langu halisi humu Jamii Forums. 'The bold' itabaki kama alias. Nashukuru uongozi mzima wa JF kwa kuverify account yangu.

Tuendelee...

Huu utakuwa ni uzi wangu maalumu ambao nitakuwa naweka maandiko mafupi mafupi (bulletins). Makala ndefu zitaendelea kama kawaida kwenye nyuzi nyingine lakini hapa nitakakuwa naweka vitu kwa ufupi sana na mara kwa mara.

Karibuni.

Bulletin # 1

VIWANDA VYA KUCHAKATA TAARIFA.??

46ac0456a109a87d1c23d723fe407d24.jpg

dd650842a9d42b5edb5aa35187d6426c.jpg

Kama mtu akikuuliza maswali yafuatayo, unajisi majibu yako yatakuwa ni yapi?
1. Jengo la picha namba moja unahisi linahusiana na
Mkuu namim nikitaka nitumie jina kamili nifanyaje?
 
May God bless you Habib! information is the power though it's bulletin still Kuna vitu vya kujifunza na kutafakari! Peace!
 
IMG-20180523-WA0010.jpg

Intelijensia: Pandikizi Chochezi

Suala la Intelijensia, ujasusi na ushushushu ni kitu adhimu sana kukifahamu si tu kwa manufaa ya usalama wa nchi bali pia yaweza kukufaa hata katika maisha ya kawaida. Mbinu za kijasusi na intelijesia kwa sasa zinatumika katika kila sekta na nyanja ya maisha. Iwe wewe ni mwanaharakati, mwanasiasa, mfanyabiashara, mwanazuoni, mwajiriwa au mjasiriamali… uelewa walau mdogo tu wa masuala ya intelijensia unaweza kukufanya kuwa hatua kadhaa mbele ya wenzako na hata pia kuweza kujikinga dhidi ya mashambulio dhidi yako pale yanapotokea.

Kwa ufupi sana siku ya leo nitaongea kuhusu moja ya mbinu adhimu ya intelijensia yenye kutumika sana ulimwenguni kote na ambayo pia nimeiona imeshika hatamu mno kwa sasa hapa nchini kwetu. Lugha yetu ya kiswahili ni changa hivyo inakosa baadhi ya misamiati kueleza kitu kwa ufasaha unaoulenga. Kwa ukosefu wa msamiati maridhawa nitaiita mbinu hii "Pandikizi Chochezi" ambayo kwa umombo inajulikana kama "Agent Provocateur".

Katika masuala ya ujasusi, pandikizi chochezi ni mtu ambaye anafanya au anashawishi mtu mwingine kufanya kitu kilicho kinyume na sheria au tendo la hila au kumuhusisha mwingine kuhusika kwenye tendo hilo.
Pandikizi Chochezi anaweza kuwa ni afisa wa chombo cha usalama, au afisa wa kiserikali au Idara na hata wakala wa chama cha siasa na kwenye ulimwengu wa biashara anaweza kuwa hata mwajiriwa wa kampuni shindani.

Pandikizi chochezi anatumiwa na Idara iliyomtuma, kujipenyeza kwenye kundi lengwa (mfano chama cha siasa au kampuni au vugu vugu ka harakati) na akiisha kujipenyeza na kukubalika kwenye kundi hilo anakuwa mstari wa mbele kabisa kindakindaki kiasi kwamba anakuwa moja ya watu wenye kutazamwa kwa mwongozo kwenye kundi hilo. Baada ya hapo Pandikizi chochezi anatumia mwanya huo kushawishi wengine kufanya tendo la hila ambalo ni kinyume cha sheria. Lengo kuu hapa linakuwa ni mfano kuvuruga harakati/vuguvugu au kujaribu kupaka matope kundi hilo husika au kulichafua kwenye jamii ama kuifanya serikali kuchukua hatua dhidi ya kundi hilo.

Mbinu hii inatumiwa mfano na serikali nyingi au vyombo vya usalama pale ambapo wanahitaji kupiga marufuku kundi fulani (chama cha siasa, vuguvugu au kampuni) hivyo pandikizi chochezi anatumiwa ili kuipa serikali au idara ya usalama sababu ya kuwachukulia kundi hilo hatua.

Si hivyo tu, lakini pia Pandikizi chochezi anaweza kutumia kushawishi mtu mwingine kufanya tukio la kudhuru kama vile mauaji bila anayetumiwa kujua. Yaani kwamba pale ambapo Idara husika au serikali husika ikihitaji 'kumu-eliminate' mtu fulani lakini haitaki yabakie maswali na sintofahamu, wanaweza kutumia Pandikizi Chochezi kushawishi mtu wa kawaida kufanya tukio hilo la mauaji pasipo mtu anayetumiwa kujua kuwa anatumika.

Nitatoa mifano michache…

IMG-20180523-WA0011.jpg

Inawezekana wengi hawafahamu kwamba Kim Jong-Un hakuwa chaguo la kwanza la baba yake Kim Jong-il kumrithi kuongoza taifa la Korea Kaskazini.
Chaguo la kwanza la Kim Jong-il lilikuwa ni mtoto wake wa nje aliyeitwa Kim Jong-nam ambaye alizaliwa mwaka 1971 na mwanamke aitwaye Song-Hye-rim. Kutokana na baba yake (yaani babu yao akina Kim Jong-nam na Kim Jong-un) kutokukubali mahusiano ya kimapenzi kati ya mwanaye Kim Jong-il na yule mwanamke Song Hye-rim ilibidi alipozaliwa Kim Jong-nam afichwe kwa kupelekwa kuishi na shangazi yake na baadae alipelekwa nje ya nchi ambako alikaa huko utoto wake wote na kusoma huko kwenye nchi za Urusi na Uswisi na kurejea Korea Kaskazini mwaka 1988.

Kama maandalizi ya kumrithi baba yake, mwaka 1998 Kim Jong-nam aliteuliwa kuongoza Wizara ya Masuala ya Usalama wa Taifa. Pia Kim Jong-nam alipewa jukumu na baba yake kuongoza kamati ya Taifa ya kuunda sekta ya Tehama nchini humo.
Pia ni Kim Jong-nam ambaye aliambatana na baba yake kwenye ziara ya nchini China mwaka 2001 ili kujadili namna ambavyo wachina wanaweza kuwasaidia kuinua sekta ya Tehama nchini Korea Kaskazini.

Kila aina ya maandalizi yalikuwa yanafanyika kumuandaa Kim Jong-nam kuwa mrithi wa Kim Jong-il kuongoza taifa la Korea Kaskazini.

Japokuwa Kim Jong-nam alikuwa anafanana sana kihaiba na baba yake kutokana na hasira zake, hisia za haraka na ujuzi wa masuala ya sanaa kama vile uandishi wa miswada ya filamu lakini Kim Jong-nam alikuwa na kasoro moja mbaya… alikuwa ni mtu mwenye kupenda anasa na wanawake hovyo. Kulikuwa na uvumi kwamba Kim Jong-nam mara kadhaa amekuwa akitoka nje ya Korea Kaskazini kwa pasipoti za kughushi zenye majina ya uongo ili kwenda kufanya starehe Macau, China na hata Japan. Uvumi huu ulikuwa ukikanushwa mara nyingi na serikali ya Korea Kaskazini.

Za mwizi ni arobaini, mwezi May mwaka 2001 Kim Jong-nam alikamatwa na mamlaka ya uhamiaji nchini Japan akijaribu kuingia nchini humo kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Narita akitumia hati ya kughushi ya kusafiria ya taifa ya Dominican Republic na jina bandia la asili ta kichina la Pang Xiong. Alikamatwa akiwa ameongozaba na wanawake wawili na baada ya kuhojiwa alieleza kuwa alikuwa amelenga kwenda sehemu ya starehe ya Tokyo Disneyland.
Ilikuwa ni aibu kubwa kuwahi kutokea kwa taifa Korea Kaskazini… ati mrithi wa kiti cha kuongoza taifa hilo anatoroka nje ya nchi na hati bandia za kusafiria ili akale starehe na wanawake.
Sitaeleza sana lakini hii ndio ilikuwa sababu ya Kim Jong-nam kuondolewa kwenye mpango wa kumrithi baba yake Kim Jong-il.

Ndipo hapa ikaanzishwa kampeni nchini Korea Kaskazini yente kauli mbiu isemayo "Mama tunayemuheshimu ndiye mtiifu zaidi kwa Kiongozi wetu Mtukufu" (wakimaanisha mama yake Kim Jong-un kiongozi wa sasa wa Korea).

Kwa hiyo taratibu Kim Jong-un akaanza kupigiwa ndogondogo aanze kuiteka mioyo ya wananchi wa Korea Kaskazini na wananchi wamsahau Kim Jong-nam.

IMG-20180523-WA0012.jpg

IMG-20180523-WA0014.jpg

The rest is history, Kim Jong-un alitawazwa kuwa kiongozi wa taifa la Korea Kaskazi tarehe 24 Desemba mwaka 2011baada ya kifo cha baba yake Kim Jong-il.

Inaelezwa kuwa Kim Jong-nam na Kim Jong-un hawajawahi kuonana tangu wazaliwe kutokana na tamaduni ya Kikorea ya kuwalea mbali mbali watoto ambao mmoja katu yao anatarajiwa kuwa kiongozi.
Kwa mujibu wa vyombo vya intelejensia vya Korea kusini, kwa mara ya kwanza walionana baada ya baba yao kufariki ambapo Kim Jong-nam aliruhusiwa kuingia Korea kaskazini kutoa heshima zake za mwisho kwa baba yake lakini hakuruhusiwa kuonekana kwa umma.

Baada ya hapo maisha yakaendelea mdogo mtu (Kim Jong-un) akiongoza taifa la Korea Kaskazini huku kaka mtu Kim Jong-nam akiishi kwa kutanga tanga kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine.
Lakini pia kihoro cha kuikosa nafasi ya kuongoza taifa hakikumuisha kaka mtu Kim Jong-nam… alifanya mahojiano kadhaa na vyombo vya habari vya kimataifa akimshutumu mdogo wake kuwa hana uzoefu wa utumishi na lazima uingozi wake utafeli. Alienda mbali zaidi na kuanza kutoa shutuma mara kadhaa kuwa taifa hilo linahitaji kufanya mageuzi ya namna ya uendeshwaji wake kuendana na ulimwengu ulivyo sasa.

Kelele hizi za kaka mtu zilianza kumkera Kim Jong-un. Ndipo hapa aliagiza maafisa wake wa vyombo vya ujasusi kuhakikisha kaka yake anauwawa mara moja.
Kazi hiyo haikuwa rahisi kutokana na kaka mtu naye kuwa na uelewa juu ya masuala ya ujasusi. Alinusurika kuuwawa mara kadhaa nchini Singapore, Macau, na hata uswisi. Majaribio haya yalifanya mataifa hayo husika kuwawashia moto Korea Kaskazini kwamba hawataruhusu mauaji hayo yafanyike nchini mwao.

Ndipo hapa majasusi wa Korea Kaskazini wakaamua kutumia mbinu adhimu… Agent Provocateur… Pandikizi Chochezi ili kuficha uhusika wao na tukio hilo kuonekana halina uhusiano na wao serikaki ya Korea Kaskazini.

Ilikuwa hivi…

Siku ya tarehe 13 February mwaka jana 2017, majira ya saa tatu asubuhi Kim Jong-nam alikuwa amewasili katika uwanja wa ndege wa wa Kimataifa wa Kuala Lumpar kwa kutumia hati bandia ya kusafiria yenye jina Kim Chol… akiwa katika sehemu ya kujihudumia mwenyewe ya check-in, walijitokeza wanawake wawili ambao walimpulizia kitu fulani usoni. Baada ya kupuliziwa tu Kim Jong-nam alidondoka chini na hali yake kubadilika ghafla. Alianza kutoka jasho lingi mfululizo huku akipaparika kama anakifafa.
Mara moja aliwahishwa hospitali na licha ya juhudi za madaktari kuokoa uhai wake, Kim Jong-nam alipoteza maisha.

Kutokana na kutumia jina bandia mwanzoni hakuna aliyemtambua ni nani. Lakini baadae vyombo vya usalama vya Malaysia wakang'amua kuwa alikuwa ni Kim Jong-nam.
Haraka akafanyiwa autopsy ili kujua ni nini hasa kilichosababisha kifo chake… daktari akarudisha majibu kuwa ameuwawa kwa 'nerve gas' hatari aina ya VX.
Hii ilikuwa ni taarifa ya kushtua mno. Gesi hii hairuhusiwi hata kutumika kwenye uwanja wa vita na ilishapigwa marufuku tangu mwaka 1993 na tamko la Kongamano la Kudhibiti silaha za kemikali.

Wanawake wale… wadada wa mjini wasio na mbele wala nyuma wametoa wapi silaha hatari kama hii?

Walipoenda kutazama mikanda ya video ya kamera za ulinzi za Uwanja wa ndege waligundua viroja zaidi. Wakati wale wanawake wanafanya tukio hilo walionekana walikuwa wameongozana na wanaume wanne waliojifunga nyuso zao… lakini kipindi wao wanampulizia Kim ile gesi wale wanaume walitimua mbio.

Polisi wakaanza msako wa kuwapata hao akina dada wawili. Ajabu ni kwamba kesho yake moja ya wale wadada akarejea tena pale uwanja wa ndege. Akakamatwa. Na huyu akasaidia kukamatwa kwa mwenzake.

Walipohijiwa walieleza kuwa walikuwa wamelipwa hela kushiriki kwenye kipindi cha TV kinachohusu Pranks (michezo ya utani kumshitukiza mtu kwa tukio ambalo hakulitegemea) na kwamba tukio la hapo uwanja wa ndege ndio ilikuwa 'prank' yao ya kwanza ambayo walitakiwa kuifanya. Wanadai walishangaa baada ya kumpulizia Kim kitu ambacho waliambiwa ni rangi walipogeuka nyuma hawakuwaona wale wenzao wanaume wanne.

Ukitazama mikanda ya video ya ulinzi pale uwanja wa ndege unathibitisha maelezo ya hawa akina dada… moja, hawakuwa wamejiziba pua na mdogo tofauti na wale wanaume wanne wengine ambao walijifunika nyuso… maana yake ni kwamba hawakuwa wanajua hatari ya ile gesi ambayo walikuwa wanapuliza na hivyo walikuwa wanahatarisha pia maisha yao.
Lakini pili, baada ya Kim kupuliziwa gesi na kudondoka na kuanza kupaparika chini, hawakukimbia bali walibakia na wameduwaa na wameshikwa na bumbuwazi ikionesha dhahiri kabisa hawakutegemea hilo. Na hata kitendo cha yule dada kurejea tena pale uwanja wa ndege kesho yake kujaribu kuwatafuta wale wenzao wanne waliowakimbia pia ilikuwa inatoa pichwa kwamba hawakuelewa uhatari wa tukio walilolifanya.
Kwa hiyo maelezo yao kuwa walikuwa wanadhani wanashiriki kipindi cha televisheni cha 'Pranks' yanakuwa na mashiko kwa kiasi kikubwa.

Nchi zote wamewanyooshea kidole Korea Kaskazini kutokana na tukio hili. Lakini hakuna ushaidi wa moja kwa moja kuthibitisha Korea Kaskazini wamehusika kumuua Kim Jong-nam japo wote tunajua wamehusika. Korea kaskazini wenyewe wanadai kuwa Kim Jong-nam amedhuliwa na 'vimada' wake… wakisisitiza juu ya historia ya Kim Jong-nam kupenda starehe, pombe, wanawake na michezo ya kamali.

Zigo hili wamebebeshwa wadada wale wawili na wanashtakiwa kwa kesi ya mauaji nchini Malaysia. Hivi ninavyoandika ni wiki iliyopita tu upande wa mashtaka umemaliza kuwasilisha ushahidi wao na sasa tubasubiri Jaji aseme kama wale akina dada wana kesi ya kujibu au la.

Hivyo ndivyo ambavyo mbinu ya kutumia 'Agent Provocatuer'… Pandikizi Chochezi inavyofanya kazi. Keep your eyes open…

Ninatoa maelezo kuhusu upatikanaji wa kitabu na maelezo yote ya muhimu.
Machana mwema chief…

Habibu B. Anga 'The Bold,'
To Infinity and Beyond
 
View attachment 784270

View attachment 784271

View attachment 784272

View attachment 784273

msg zangu haujibu eeh??????????????
 
Dah nimekuelewa sana mkuu..keep it up..but vipi hao jamaa waliojificha sura wakalaghai wale kina dada,je hakuna uchunguzi wowote kuhusu wao ni kina nani?!!!...ni hayo tu mkuu
 
AFTERNOON BULLETIN

5e131025061da492df73916885eaf9a5--roswell-new-mexico-autopsy (1).jpg

MPAKA SIKU TUNAONDOKA DUNIANI HATUTAWEZA KUKANYAGA NDANI YAKE

Ukiwa ni mtu ‘mbishi’au tuite ‘mpambanaji’ unaweza kuweka bidii na kufika mahala kokote pale duniani ambako unatamani. Au labda ukiwa mtu mwenye misuli ya kiuchumi, unaweza kutumia wingi wa rasilimali zako kukupeleka mahala kokote pale ambako unapaota. Lakini ziko sehemu ambazo haijalishi una misuli ya kiuchumi kiasi gani au ni mbishi kiasi gani… kamwe hautokuja kukanyaga.

Mwanzoni mwa mwaka jana niliandika makala fupi juu ya baadhi ya sehemu hizi. Leo hii katika andishi hili fupi ningependa tutazame tena japo kwa uchache baadhi ya sehemu hizi ambazo ni watu wachache tu wenye ruhusa ya kukanyaga ndani yake.

196.JPG

Mfano mzuri ni skandali ambayo iliibuka mwanzoni mwa miaka ya 2000 ambapo iligundulika kwamba mwaka 1975 NSA kwa kushirikiana na shirika la mawasiliano la Uingereza waliunganisha mkongo wa mawasiliano katika mfumo wa mawasiliano ya simu za kimataifa zenye kupita nchini Uingereza katika kituo cha mawimbi cha Hunters Stones kwenda kwenye kituo cha kijasusi cha RAF Mentwith Hill na baadae mkongo huo kuboreshwa mwaka 1992 na kuwa wa fibre optics. Hii iliwawezesha NSA katika kituo cha RAF Mentwith Hill kuwa na uwezo wa kunasa na kurekodi zaidi ya simu 100,000 kwa pamoja na kwa wakati mmoja.

Lakini pia kituo hiki kinatumika kama Ground Station ya Satellite za kipepelezi za nchi ya Marekani.
Pia kumekuwa na taarifa za uhakika pia kuwa kituo hiki kinatumika kuratibu mashambullizi ya anga huko Mashariki ya Kati kwa kutumia “drones”.

Mafungamano ya ECHELON na RAF Mentwith Hill Station
Kuna kitu kinaitwa ECHELON. ECHELON ni program maalumu ya kijasusi ambayo inaratibiwa na nchi zenye kujulikana kama “Five Eyes” kwenye jumuiya ya kimataifa kuhusu masuala ya ujasusi.
Ni kwamba katika miaka ya mwishoni mwa 1940s kulianza mafungamano ya kiintelijesia ambayo mwaka 1961 yalizaa makubaliano kati ya nchi za Marekani, Uingereza, Canada, Australia na New Zealand na makubaliano hayo kufanywa rasmi kiserikali mwaka 1971 ambapo walisaini mkataba unaoitwa UKUSA (UKUSA Security Agreement). Mkataba huu unatanabasiha maslahi ya pampja ya kiintelijensia kati ya nchi hizo na kufungua mlango wa kushirikishana taarifa za kijasusi ambazo zina maslahi yao nchi hizo zote tano kwa pamoja. Kama ulikuwa haufahamu basi hii ndio sababu ya nchi za Marekani na Uingereza na hata Cadana kuwa kama ndugu wa damu, kuwa na msimamo mmoja kwenye masuala karibia yote ya kimataifa na kushirikiana kupitiliza kufikia kiwango cha Uingereza kuonekana kama kibaraka wa Marekani. Pamoja na sababu nyingine lakini moja ya sababu kuu kabisa ni huu mkataba wa UKUSA na program ya ECHELON.

Sasa ECHELON ni “code name” ya program hii ya pamoja ya ‘surveillance’ ya kimataifa kukusanya na kuratibu na kuchambua intelijensia za mawimbi (SIGINT – Signal Intelligence) kati ya nchi hizi za ushirikiano wa “Five Eyes”.

Taarifa hizi za intelijensia zinakuwa shared kati ya nchi hizi yote tano kupitia mfumo maalumu wa mtandao unaojulikana kama “Stone Ghost”. Huu ni mfumo wa mtandao wenye ulinzi mkali na usalama wa hali ya juu ambao ni watu wachache mno wana ‘authorization’ ya kuutumia. Mfumo huu wa mawasiliano unasimamiwa na idara ya DIA (Defense and Intelligence Agency) ya nchi ya Mareakni. Kwa wale wenye kufahamu masuala ya intelijensia, ni vizuri kujua kwamba mfumo wa “Stone Ghost” ni tofauti na Interlink. Interlink yenyewe mfumo wake unatumiwa kwa ajili ya mawasiliano kati ya vyombo vya Intelijensia na ujasusi nchini Marekani pekee wakati ambapo “Stone Ghots” inatumiwa kushare taarifa kati ya idara za nchi za muungano wa “Five Eyes”. Nadhani unaweza kuona tofauti ambayo mara nyingi ni rahisi kuchanganya. Miaka ya zamani ili kuweka tofauti hii bayana, mfumo wa ‘stone ghost’ ulikuwa unaitwa ‘Interlink-C’.

images (79).jpeg

RAF Mentwith Hill Station
Moja kati ya sehemu ambazo zitatuchukua miaka mingi sana ili tuweze kufahamu kwa uhakika kabisa juu ya kile ambacho kinaendelea ndani yake basi ni eneo hili la RAF Mentwith Hill (Royal Air Force Mentwith Hill Station) ambalo liko maeneo ya Harrogate, North Yorkshire nchini Uingereza.
Eneo hili ni eneo la kijeshi na liko ndani ya nchi ya Uingereza, lakini ajabu ni kwamba eneo hili linamilikiwa na kuendeshwa na Wizara ya Ulinzi ya Marekani (DOD). Hata wafanyakazi kwenye eneo hili ni wamarekani kutoka idara za USAF na NSA. Makubaliano hasa kati ya nchi ya Uingereza na Marekani mpaka kufikia Marekani kukabidhiwa sehemu hii ya kijeshi bado ni siri kubwa.

Kituo hiki cha siri kubwa chenye kukaa kwenye ardhi yenye ukubwa wa kilomita 2 za mraba, kilifunguliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1954 na British War Office (Wizara ya Ulinzi ya sasa ya Uingereza) na mwaka 1958. lakini kituo hiki kilitolewa kwa Marekani kupitia idara yao ya ASA ya kipindi hicho (US Army Security Agency) ambayo kwa sasa imeunganishwa kwenye idara ya Millitary Intteligence ambayo ni sehemu ya INSCOM (US Army Intelligence and Security Command).

Lengo kuu la awali la kuanzishwa kwa kituo hiki lilikuwa ni kufuatilia mawasiliano ya mawimbi na kielektroniki nchini Urusi kipindi kile cha vita baridi.

Mwaka 1966 kituo hiki kilikabidhiwa kwa NSA (National Security Agency) kutoka kwa idara ya ASA ambao ndio awali walikabidhiwa na Uingereza.

Mara nyingi watu hujiuliza, kituo hiki kilianzishwa kwa lengo la kufuatilia mawasiliano ya kieletroniki nchini Urusi kipindi kile cha vita baridi… kwa nini kituo hiki bado kipo mpaka sasa? Je, kwa sasa kituo hiki kina kazi gani hasa?

Japokuwa shughuli zinazoendelea katika kituo hiki ni siri kubwa, lakini kumekuwa na taarifa za uhakika kwamba kituo hiki kinatumiwa na NSA kwa ajili ya kufuatilia mawasiliano ya watu wenye kutiliwa shaka ulimwenguni kote. Si hivyo tu kituo hiki pia kinatumiwa na NSA kunasa mawasiliano karibia yote ambayo wanaweza kuyapata… hata simu za raia wa kawaida tu.

images (80).jpeg

Kwa kifupi basi, hiyo ndio RAF Mentwith Hill Station. Moja ya sehemu adhimu zaidi ulimwenguni. Moja ya sehemu ya siri zaidi ambpo mpaka sasa watu kwenye jumuiya za ujasusi duniani wanakuna mbongo kuweza kung’amua nini hasa ambacho kinaendelea ndani yake. Ni moja ya sehemu ambyo unaweza kuiona kwa mbali na majengo yake na mitambo yake yenye umbo la kuvutia mpaka watu kuibatiza jina mitambo hiyo kama ‘golf balls’ kutokana na umbo lake, lakini kamwe… abadani hata siku moja hatutaweza kukanyaga mguu ndani yake. Ni wachaguliwa wachache tu ndani ya NSA ambao ‘wanafaidi’ kuona upande wa pili wa ulimwengu… upande ambao unakupa nguvu ya kuweza kukulevya na muda mwingine kujihisi kama ulimwengu uko kiganjani.

Nitarudi kujadili eneo lingine.

Mchana mwema chiefs,

Habibu B. Anga ‘The Bold’
To Infinity and Beyond
 
AFTERNOON BULLETIN

View attachment 791285

View attachment 791286

View attachment 791287

View attachment 791288

Hureeei nimekuwa wa kwanza kukoment
 
Kuna nyau mmoja kasoma afu mwisho kakoment kuwa plagiarism ..... Hili jamaa lina wivu hata dada yake haoni ndani

Habibu ni kama aliwahi kumpigia huyo jamaa demu wake!ana inda, wivu na roho mbaya dhidi ya mwanaume mwenzie mpaka anaogopesha!
 
Shukrani sana mkuu kwa kutujuza haya mambo!!!....sema nina swali je engineers waliohusika kukijenga na kukiboresha hivyo kilivyo hawawezi kujua undani wake?
 
Dah hizi nimezipenda hazina mambo ya kusubiri mpaka ujisikie kuweka part zinazofuata wiki zijazo
 
Back
Top Bottom