Bongo kote kubaya tu, labda uniambie sehemu zenye 'kujitahiditahidi'
The Boss,.. Take Zero from this fellow...He is a CAST in purity!...His NO means Yes...Always!
ok.unapoona wewe wanajitahidi ni wapi?
kwa bongo mitaa inayojitahidi ni mitaa ya o'bay , masaki, mbezi beach, michokeni i mean mikocheni na sinza flani hivi (sio kule uzuri et al). Ingawa sometimes huduma za jamii kama maji, maeneo ya wazi etc ni utata, pollution ya kelele na utupaji taka hobelahobela ni wa kiwango cha juu.
ukiambiwa uchague eneo moja la kuishi.
Utachagua wapi.bila kujali gharama..
Na kigezo cha aina ya watu na dating if u r single ukizingatia..
Aisee nimeishi maeneo mengi, ila labda maeneo ya hovyo zaidi naweza kukutajia, maana mengi ni yakawaida sana ila basi tu.Napenda kuishi nimezungukwa na wastaarabu, watu wenye kuheshimu sheria za makazi. Na napenda hali ya utulivu, usalama na mitaa iliyopangiliwa. Nadhani Mbezi Beach kwa kiasi flani kuna asavali. Suala la ku-date ni suala skills zako tu, unaweza ku-date hata kule unapopata mkate wako wa kila siku, etc. sio lazima pale unapoishi.
Aisee nimeishi maeneo mengi, ila labda maeneo ya hovyo zaidi naweza kukutajia, maana mengi ni yakawaida sana ila basi tu.
maeneo ya hovyo zaidi ni Mtoni Azizi Ally-huku ni kuchafu sana, hakuna mifumo ya maji taji taka, watu wanakojoa hovyo, vinyesi vipo kwenye Rambo.
Buguruni kwa mnyamani plus eneo linaloitwa tapa, huku kulikua na da,po zamani , maana mifumo ya vyoo vyote imeelekezwa kwenye mfereji ya maji machafu, huku kunanuka sana, vyoo vyote vimejaa.
Tandale plus manzase kuelekea zamani waliita uwanja wa fisi, huku ni mavi yaliyotapakaa mitaroni, kunammbu wakubwa kama vifaranga, kuna maralia sana, kipindupindu kimepiga kambi hapo.
maeneo ya hatari kuishi ni maeneo ya kuzunguka kabi za jeshi kama kule kunduchi.
Bongo kote kubaya tu, labda uniambie sehemu zenye 'kujitahiditahidi'
teh teh teh..Mkubwa unakomelea msumari, ati mbu wakubwa kama vifaranga..lolz
Ndio maana natafuta shughuli ya kufanya nje ya Bongo Daresalama. Nakubali kuwa Dar ni nzuri kwa kibiashara, ila ki makazi ipo very hopeless, inalazimisha kuchukua watu wengi wakati hakuna miundombinu ya kukidhi maisha ya kisasa.
Hivi ukiwa daresalaam,ni kitongoji kipi unaweza
sema ni the best place to live...
Vigezo vya kuzingatia ni...
Aina ya watu....
Burudani...
Huduma za kijamii,benki,soko n.k.
Dating..
Na vinginevyoo
mimi nafikiri kwa sasa makumbusho ndo the best place
kwa vigezi hivyo..
Wewe unasemaje????
Mimi naona kwa vigezo vyako na kwa jinsi hali ilivyo Tanzania best place to live ni kaburini :Aina ya watu: Hakuna mafisadi, hakuna kukojoa kwenye masinki, viongozi hawatukanani hadharani mbele ya watoto na wajukuu.Burudani: hakuna haja ya burudani.Huduma za jamii:Hazihitajiki, hakuna tanesco, dawasco, TRL ya wahindi, watoto hawakalii ndoo darasani, hakuna foleni za kijinga etc.