The best place to live in dar..

sehemu nzuri ni Boko national housing....kumepimwa,kuna maji,kuna umeme,kila nyumba ina access ya barabara ya molamu,hakuna msongamano,hakuna kelele za baa
 
Bongo kote kubaya tu, labda uniambie sehemu zenye 'kujitahiditahidi'

ndugu yangu wewe, we si ulisema utabakia bongo tu? leo unasema bongo ni kubaya tena? mwe! sikusomi!

bongo kuzuri sana; tembelea Tegeta, Wazo Hill, Madale, Bunju, Mbweni etc! karibu kwetu Goba ndg. Abdul, utakula sana matunda ila usisahau kwenu sijui wapi, usiniambie ni shimo la udongo!!!
 
aisee nimeishi maeneo mengi, ila labda maeneo ya hovyo zaidi naweza kukutajia, maana mengi ni yakawaida sana ila basi tu.
maeneo ya hovyo zaidi ni mtoni azizi ally-huku ni kuchafu sana, hakuna mifumo ya maji taji taka, watu wanakojoa hovyo, vinyesi vipo kwenye rambo.
buguruni kwa mnyamani plus eneo linaloitwa tapa, huku kulikua na da,po zamani , maana mifumo ya vyoo vyote imeelekezwa kwenye mfereji ya maji machafu, huku kunanuka sana, vyoo vyote vimejaa.
tandale plus manzase kuelekea zamani waliita uwanja wa fisi, huku ni mavi yaliyotapakaa mitaroni, kunammbu wakubwa kama vifaranga, kuna maralia sana, kipindupindu kimepiga kambi hapo.
maeneo ya hatari kuishi ni maeneo ya kuzunguka kabi za jeshi kama kule kunduchi.


uzoefu wa kuishi maeneo ya ovyo tu??
Huna uzoefu wa kkuishi kwa wastaarabu?
 
huyu nadhani anaongelea sehemu iliyokaa kimikogo zaidi! Teh teh, ndy maana amekomalia dating!! Wabongo bwana!...............
.........mimi binafsi napendeleea zaidi kuishi mbali sana na mji, sehemu ambayo nyumba haijazungushiwa uzio na jirani yako wa karibu ni nusu kilomita lakini bado unaweza kulala milango wazi, napenda muonekano wa nchi, napenda kuona mabonde, milima tena karibu na mto, ndege wanalia kwa uzuri, bila shaka sehemu tulivu na salama ni kijiji, unajichagulia shamba kuubwa na kkuboresha makazi maji ni rahisi tu, umeme ni solar na standby generator, muhimu karibu na barabara.


sio mikogo...
Napenda eneo lenye nightlife iliyochangamka
ndo maana makumbusho napaona pazuri
mimi naishi tegeta,utulivu mkubwa mno...
Hadi naboreka sometimes.
 
Napenda uswazi, ambako ninapata fursa ya kuona Mwali anachezewa ngoma za Kizaramo usiku kucha. Maeneo ya Kiwalani yanafaa sana na nilienjoy wakati naishi kule, ila tatizo ni vibaka na roba za mbao.
 
Sinza ndio poa.....

Vigezo...
Baada ya Nyumba 4 unakutana na Grocery,Pub,Bar na Nightclub Hamna vibaka (wakabaji),Maji ya Uhakika (Line ya Ikulu),Jirani na Mlimani City ambayo ni One stop Shop,Madada poa kwa saana.... Etc Bar ukiamua kujilipua mpaka asubuhi kuna Meeda Night Club,Corner Bar etc...
 
sinza ndio poa.....

Vigezo...
Baada ya nyumba 4 unakutana na grocery,pub,bar na nightclub hamna vibaka (wakabaji),maji ya uhakika (line ya ikulu),jirani na mlimani city ambayo ni one stop shop,madada poa kwa saana.... Etc bar ukiamua kujilipua mpaka asubuhi kuna meeda night club,corner bar etc...


sinza mori kwa kweli pazuri...
 
Sinza ndio poa.....

Vigezo...
Baada ya Nyumba 4 unakutana na Grocery,Pub,Bar na Nightclub Hamna vibaka (wakabaji),Maji ya Uhakika (Line ya Ikulu),Jirani na Mlimani City ambayo ni One stop Shop,Madada poa kwa saana.... Etc Bar ukiamua kujilipua mpaka asubuhi kuna Meeda Night Club,Corner Bar etc...
hizi huduma hata suka zipo!CHAWOTE BAR INAKESHA MARA KIBAO!unakula taska huku unahesabu magari ya mkoani!
 
hizi huduma hata suka zipo!CHAWOTE BAR INAKESHA MARA KIBAO!unakula taska huku unahesabu magari ya mkoani!

Hali kadhalika Basihaya campsite, Boko View Hotel, Tegeta By Night, Zero pub. Unakula bia huku unaangalia watalii wanaenda kushangaa bagamoyo. Karibuni kwetu Boko.
 
hizi huduma hata suka zipo!chawote bar inakesha mara kibao!unakula taska huku unahesabu magari ya mkoani!

mkuu buffalo usiisahau, kuna KILIMANI pale napo pazuri, halafu pale kilimani huwezi amini kuna bavaria 8.6, hii bia naisakaga sana bar nyingi hawana hii kitu
 
mwamba ngoma uvutia kwake, popote kambi ilimradi nina pa kulala, misosi napata na mavazi hayanipigi chenga bila kusahau afya bora!
 
Hali kadhalika Basihaya campsite, Boko View Hotel, Tegeta By Night, Zero pub. Unakula bia huku unaangalia watalii wanaenda kushangaa bagamoyo. Karibuni kwetu Boko.


Boko napo kumevamiwa cku hizi, enzi zile hata hawajatengezeza road nilikuwa naona kama natokea dar kwenda kigoma...lol, cku za Eid ndio balaa na road yaani vurugu tupu na waendao bagamoyo....
 
Back
Top Bottom