Thanx to mobile tracker,found back my phone | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Thanx to mobile tracker,found back my phone

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Paul S.S, Aug 5, 2011.

 1. P

  Paul S.S Verified User

  #1
  Aug 5, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Wakuu juzi kati nilikuwa natoka kupata kilaji nikapata kaajali mitaa ya magomeni kama saa 5 usiku hivi, katika kurupushani ya ajali nikatoka nje ya gari kwa bahati mbaya nikasahau kulock milango wahuni wakajisevia LG yangu.

  Kesho yake majira ya saa 2 usiku ikaingia sms kwa no yangu nyingine na kwa waifu, ina inasema simu ime no xxxxxx inatumiwa na simu no xxxxx, nikashtuka kuja kukumbuka kumbe niliset mobile tracker siku nyingi nilipo inunua kiasi kwamba nilisahau kabisa hiyo maneno.

  Kwakuwa ilikuwa ni no ya voda nikatumia trick ya kujua jina lake kwa kumtumia MPESA kwa kuweka kiwango kikubwa ambacho simu yako haina, kisha ikaleta sms kuwa "huna pesa ya kutosha kumtumia xxxxxxx sh kadhaa", jina la kike

  Bila kukawia nikaipiga ile no fasta,akapokea mdada, nikamwambia wewe ndio fulani, akasema yes nikamwambia hiyo simu imeibiwa na kwa usalama wake airudishe haraka, akakata simu na haikupatikana tena
  kesho yake saa 4 asbh akaweka line ya tigo meseji ikaingia, nikampigia nikachimba biti akakata simu, siku nzima akawa hapoke simu nikawa natuma sms za mikwara, akazima simu.

  Keshokutwa yake akaweka line ya airtel kitendo bila kuchelewa nikampigia, ilibidi awe mdogo tu na akanambia kweli simu kapewa na basha wake na akaomba suluhu nisimfikishe mbali ila hataki kuonana na mimi naweza kuwa na polisi hivyo tukakubaliana aipeleke baa fulani kaunta, akafanya hivyo, akaipeleka kwanza kisha akanipigia nikaenda nikaikuta kaunta.Ila biti nililomchimba lilikuwa sio la kitoto,

  Chakusikitisha ni kuwa nilipo kwenda vodacom kuifunga no yangu ilikuwa na muda wa kutosha wa hewani mwizi wangu akajihamishia lakini Voda walishindwa kunisaidia kumtrace mwizi wangu wakanipa mlolongo mgumu na kunishauri bora kununua nyingine
   
 2. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Oyaaaaaaaaaaaa hii kali sana.
   
 3. lukenza

  lukenza Senior Member

  #3
  Aug 5, 2011
  Joined: Apr 11, 2010
  Messages: 120
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  mkuu maelezo yako yanamake sense kwani unaset vipi mobile tracker maana mimi nimeibiwa simu yangu hivi karibuni lkn sikuweza kuipata
  msaada tafadhali
   
 4. P

  Paul S.S Verified User

  #4
  Aug 6, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Mkuu nadhani LG zote zinakuja na hii application toka kiwandani, Sio simu zote zinakuja na hii appl, inabidi kutafuta za kudownload lakini ni za kulipia, labda tusubiri wataalamu watudadafulie zaidi, maana hata mimi nakumbuka sikumoja wakati naipekua pejua simu yangu ndio nikakutana na hii kitu kwenye security. nikaweka tu bila kujua kama inaumuhimu kihivyo
   
 5. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #5
  Aug 6, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Duh hii kali
  je huo mkwara unaweza kutumwagia hapa labda na sisi tutauhitaji siku hiyo....
   
 6. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #6
  Aug 6, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,159
  Trophy Points: 280
  Lukenza, hii sio advertisement ya LG?
   
 7. m

  mob JF-Expert Member

  #7
  Aug 6, 2011
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,028
  Likes Received: 510
  Trophy Points: 280
  wakuu sim zote za samsung zina izo program ni nzuri sana.
   
 8. Mwendabure

  Mwendabure JF-Expert Member

  #8
  Aug 6, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,056
  Likes Received: 299
  Trophy Points: 180
  Unaweza kudownload free NetQin ktk simu yako na ukapata huduma hiyo bureee! Mi nimeweka na iko poa. Ila usisahau kuleta matokeo na senkyu (hasa kwa PM) ukifanikiwa... Senkyu.
   
 9. P

  Paul S.S Verified User

  #9
  Aug 6, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Mkuu kwanza nili take advantage kwa yeye kutojua najuaje kila sim card anayoweka? nikamwambia hiyo ni simu maalumu kwa kazi za ofisini hivyo hata afanye nini nitajua killa anachofanya inamitambo maalumu.

  nikamwambia kuwa nakwenda voda na kitu cha kwanza voda wanablock namba za watu wake wote wa karibu anaowasiliana nao na watakapo kwenda voda watashikiliwa hadi wakutaje, hivyo asishangae anakuja gugongewa mlango usiku mkali.

  Pia nilimwambia hiyo simu iliibiwa na Milion kadhaa na laptop nk hivyo atakapo kamatwa asinilaumu kwani nampa muda uirudishe mwenyewe vinginevyo kesi itakuwa yake.

  Mkuu mara ya mwisho alikuwa mdogo pengine alidhani mimi mchawi, aliniomba msamaha sana na kunisihi nisimripoti ndugu zake watapata usumbufu na kujua yeye mwizi na tapeli   
 10. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #10
  Aug 6, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Duh...but angekuwa ana knowledge na nizi tknoloji
  ingekuwa ngumu naona...
   
 11. P

  Paul S.S Verified User

  #11
  Aug 6, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  FF umenifurahisha sana, is it sound like advertisement?
  Simu nyingi sana zina hiyo maneno, huwezi amini baada ya tukio hilo nikaanza kukaguwa simu zangu zingine sijaziona nimekuja kuikuta hiyo appl ipo kwenye simu ya nyumbani vodafone 150 ingawa yenye unaingiza no moja tu.

  By the way kama nitangazo basi mimi ni mbunifu mzuri teh teh teh
   
 12. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #12
  Aug 6, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  I love technology ...
   
 13. P

  Paul S.S Verified User

  #13
  Aug 6, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Sijajua bado kama ukiflash simu au kuifanyia hard reset kama inafuta hiyo maneno, ngoja nijaribu ku google.
  Lakini kwa waTz tulio wengi akili yetu huwa ni kutoa line na kuweka nyingine na kisha anafuta phone book anajua kamaliza mchezo.

  Lakini hebu nikuulize mkuu mfano ikatokea mtu kakuuzia simu na baada ya kuweka simcard yako unakutana na mkasa huu je utairudisha? kumbuka umesajili no yako, assume huwezi kumpata aliye kuuzia
   
 14. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #14
  Aug 6, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  kama nimeinunua kwa bei mbaya.nitaizima kwa muda kwanza
  au kumuuzia mwingine.....lol
   
 15. Brakelyn

  Brakelyn JF-Expert Member

  #15
  Aug 6, 2011
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 1,236
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  mobile tracker ni kweli kabisa inafanya hivyo, sio story.. kwenye simu zingine kama Nokia, BlackBerry, Iphone na Android os userphones hizo applications unaweza kuziweka manually..mfano hiyo niliyoAttatch hapo chini ni ya symbian s60v3 & v5, ya BlackBerry inaitwa PHONEBAK2U Anti-Theft, Iphone ipo iLocalis Anti-theft, Anti-Theft + GPS Security alarm na AntiDroid Theft kwaajili ya Android..zinapatikana kwenye forums mbalimbali kwenye internet na pia Apps stores'..
   

  Attached Files:

 16. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #16
  Aug 6, 2011
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  nilisha ona jamaa wanauza hiyo software ya kulinda simu, nikapuuza.
  Nikiona tena na mimi ntainunua ili kuilinda Siemen yangu C25 Twanga Pepeta
   
 17. Fabolous

  Fabolous JF-Expert Member

  #17
  Aug 6, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 1,302
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Mkuu Paulss Asante sana kwa sredi yako. Kweli hapa tunajifunza vitu vingi sana ambavyo tulikua hatuvijui kabla. Sasa hivi na mimi naweka kwenye Nokia zangu E61i na E 7 .
  Thank you!
   
 18. P

  Paul S.S Verified User

  #18
  Aug 6, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Mkuu inasaidia sana wakati mwingine.
  Lakini kinacho niudhi mimi ni kuwa hivi hawa service provider wetu Voda,Tigo, Airtel nk wanashindwaje kujiorganise na kublock simu zote zitakazo ibiwa kwa imei no?

  Kama handset yenyewe inaweza kuripoti kuwa inatumiwa na no gani je itakuwa kwa hawa provider? inatakiwa ukiibiwa simu unakwenda kuripoti kisha provider wote wanaiblock hiyo imei na simu ina kuwa useless labda akaiuze nje ya nchi hii ingepunguza wizi wa simu.

  Kingine ni mlolongo wa ugumu kutaka hata ku trace namba alizopiga au kujihamishia salio kabla hajatoa simcard yako, yaani yule mdada wa Voda alinipa mlolongo mgumu nikatamani kumnasa vibao, akaishia kunishauri eti bora ninunue nyingine.

  Mimi naona issue ni rahisi kama wakijipanga wenzetu mbele huwezi iba simu ya mtu ukathubutu kuitumia kwa kuweka simcard yako watakupata dakika sifuri, wana deal na watuwako wa karibu unaowasiliana nao mara kwa mara, na hapa swala la usajili ndio umuhimu wake unapokuja
   
 19. HT

  HT JF-Expert Member

  #19
  Aug 6, 2011
  Joined: Jul 29, 2011
  Messages: 1,899
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  ngoja niiseti ktk simu yangu na ya waifu
   
 20. HT

  HT JF-Expert Member

  #20
  Aug 6, 2011
  Joined: Jul 29, 2011
  Messages: 1,899
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  ngoja niiseti ktk simu yangu, na add namba yangu na ya waifu.
  Bravo Paulss
   
Loading...