Jigsaw
JF-Expert Member
- Jun 17, 2011
- 1,823
- 680
Kuna quality za rais wa nchi na kuna quality za usanii!
Kuna busara ya kuwa kiongozi wa nchi na kuna busara ya kuwa kiongozi wa vikao vya harusi!
Bahati mbaya kuna namna ya kulazimisha mtu fulani a-fit sehemu fulani, bahati nzuri kuwa kila anapoweza kufit mtu ndipo anapowekwa kidemokrasia kutokana na akili za waliomweka hapo!
Kwa bahati mbaya mimi sina cha kufuata mkondo, sijawa mbwa mimi wala sina anayenipigia mluzi, ni huru kutoa mawazo pasi kujua au kujali mwingine ataumia vipii
Swala la Arusha, swala la lile sakata la umeya na madiwani, si swala la kuchekewa, damu imemwagika kule!
Ni ufisadi sana kufikiri kuwa yale tunayoyawaza sisi tu ndiyo yako sahihi.
Si busara Slaa kuingilia maamuzi ya madiwani ambao kimamlaka ni wawakilishi wa chama kule kwenye maeneo yao. sidhani kama rais anaweza kuingilia maamuzi ya mkuu wa wilaya kama yale maamuzi yalilenga katika kuleta amani na kusaidia wananchi wa eneo husika
Hii si aibu ya chadema tu, ni aibu ya uongozi wa juu, kutowatumaini wala kuwaamini hawa madiwani, ambao kwayo wanaleta na kusambaza sera za chadema; kibaya risk kubwa iko kuwa madiwani wengi zaidi watatumika kuiweka CCM madarakani kwani ni DHALILISHO LA MADIWANI WOTE....they are kids they can not think what a joke!!si busara hata kidogo na ni ufisadi wa kurubuni watu kuwa chadema ilikuwa haijui kinachoendela huko Arusha,
kila kitu kilikuwa wazi vyombo vilitangaza, na LEO ghafla akina slaa wanashtuka kama vile wamefumaniwa na wake za watu kuwa madiwani hawakuwa sahihi!
Miafaka ipo, haikwepeki inaishi, inakua inatafutwa, ili amani iwepo! HIVI ingekuwaje kama chadema wangekuwa chama tawala kwenye issue hii ya Arusha??Slaa umeishaharibu vitu vingi, ila wale vipofu wako wanaojaribu kwa upofu wao hata kukuona uko sawa na Nyerere! (God Forbid!) ili swal la Arusha limekaa kimaslahi zaidi na siyo ki-nchi zaidi! Nilijua ukimya huu umejengeka kibusara kumbe una kula tuition ya kuwa puppet!watu wako mahali fulani ambao wakilala na kuamka wanaota chadema ishike dola, wako watu mahali fulani wanaona credibility ya wabunge wa chadema, wako wanaoona kwa pandembili......Hivi SLAA ANGEKUWA RAIS ingekuwaje?
Slaa angezuia magazeti yasimchore katuni , SLAA ASINGEKUBALI KUTOKA MADARAKANI KWA NGUVU YA DEMOKRASIA.....Thanks God you are not president!
Swala la Arusha kwa namna nyingine limewaharibia tena.....Lema tunamjua, is just another gang in the house, nguvu za maneno na mob saikoloji havitamfikisha popote......certainly we need change but not changes that alerts us differently!!
MBIO ZA CHADEMA HII zinapeleka kuwa si chama cha demokrasia bali cha kibabe, jeuri, chama ambacho kingekuwa na dola wangekuwa madikteta.
Mbowe hana tatizo, yeye ili mradi biashara zake ziende salama in the name of politics!! bila kujua anamwingiza Slaa chooni, slaa bila kujali hatima yake na mtoto wake mchanga analipuka tu!!! TUTAFANYA UCHAGUZI UPYA WA MADIWANI....TUTAUNDA TUME YA MARANDO ......CCM style....shame on you!!!!!
Matatizo ya kwenda na Laptop Bar !!