LOVINTAH GYM

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
459
643
DEFLATION

Hiki ni kipindi ambacho bei za bidhaa hushuka, na hufanya thamani ya pesa kuongezeka.

Hapa ndio unajikuta ukienda sokoni na 10,000 unanunua mahitaji yote ya week na change inabaki.

Chanzo cha kushuka kwa bei.

1.Economies of scale.

Kampuni ikiweza kuzalisha bidhaa nyingi na gharama za uzalishaji kuwa ndogo hii itasaidia bei ya bidhaa kuwa ndogo na kampuni iendelee kupata faida.

Kumbuka supply ikiongezeka na demand ikawa constant ni automatic bei itashuka.

2. Technological advancement

Ukuaji wa teknolojia kutasaidia mzalishaji kupunguza gharama za uzalishaji na kuuza bidhaa kwa bei ya chini, kumbuka supply ikiongezeka na demand ikawa constant ni automatic bei itashuka.

3. Competition

Kukiwa na ushindani kutasababisha wauzaji kushusha bei, ili waweze kupata mauzo ya kutosha, kumbuka supply ikiongezeka na demand ikawa constant ni automatic bei itashuka.

4. Sheria za nchi

Serikali ikiongeza ruzuku kwa wafanyabiashara, hii itasababisha ongezeko la bidhaa na gharama kupungua, kwahiyo bei za bidhaa zitakuwa chini.

Pia serikali ikikataza bidhaa kuuzwa nje ya nchi, inamaana supply ya bidhaa itakuwa kubwa ndani na nchi na ile surplus iliyokuwa ikauzwe nje itatakiwa kutumika ndani ya nchi.

Pia serikali ikiongeza faida kwa wawekezaji, basi watu wengi wataona ni kheri watunze pesa zao ili wapate riba kubwa kuliko kutumia hovyo.

Pia serikali ikipandisha riba kwa wakopaji, hii itafanya watu wengi watunze pesa zao maana anajua akitumia vibaya akakopa, atatakiwa kulipa riba kubwa.

Ilikua akichukua mkopo wa gari analipa asilimia 10 tu, ila serikali ikapandisha mikopo riba irudi kwa asilimia 25.

Mtu ataona ni kheri apande daladala kuliko kununua gari, kumbuka demand ikishuka na supply ipo constant, bei lazima ishuke.

4.Majanga.

Hiki ni kipindi cha shida, mfano mtu akifukuzwa kazi atakuwa mbahili wa kutumia pesa zake kwenye kitu chochote ambacho sio cha ulazima.

Mfano 2:

Madaraja yamevunjika, inamaana magari yaliyokuwa yanafata mizigo kutoka eneo husika inakuwa ngumu kwenda kuchukua. Tena ikiwa ni vitu vya kuharibika kama nyanya, mihogo basi wakulima wa eneo hilo itabidi wauze kwa bei ya chini.

Japo wale waliokuwa wanategemea kuchukua mihogo na nyanya kutoka hiko kijiji kwao bei zitapanda kutokana na uhadimu wa bidhaa.
MADHARA YA DEFLATION KATIKA NCHI

1. Unemployment

Ni kitendo cha ajira kupungua, Kama bei zikiwa chini kwasababu ya ukuwaji wa teknolojia, inaaana kazi ambayo ilikuwa ifanywe na watu 10 sasahivi inafanywa na watu 2, Inamaana watu 8 wote wamekosa kazi.

2. Reduction in investment

Muuzaji siku zote analenga faida kubwa, sasa akiona bei ya bidhaa imekuwa ndogo na wauzaji ni wngi ataona bora abaki na pesa yake kuliko kuwekeza kwenye hio biashara.

3. Kuongeza thamani ya pesa.

Mfano mtu anayeishi Iringa au Mbeya ukimpa 10,000 basi ataweza kununua vitu vingi tofauti na ukimpa 10,000 mtu wa Dar.

4.Recession

Hiki ni kile kipindi ambacho makampuni huanza kufeli, wateja wamepungua na supply ipo kwahio inabidi washushe bei ili kuvutia wateja.

Mfano kampuni ya kuuza magari, wanunuzi wa magari wakiwa wanaongezeka basi automatically ataajiri vijana wa sales wengi, ila wanunuzi wakianza kushuka basi ataanza kufukuza watu kazi, na wanaobaki wanaweza kupunguziwa mishahara yao.

Pia bei za bidhaa zikishuka mzalishaji anaanza kuona faida anayopata ni kidogo kwahiyo ni kheri afunge biashara, kwahiyo wale watu aliyowaajiri watakosa kazi.

5. Mikopo kuongezeka thamani.

Kumbuka bei ikiwa chini ina maana pesa utakayoishika na yenyewe itakuwa chini, hivyo inakuwa ngumu kulipa madeni ipasavyo kutokana na kupata pesa kidogo na inakuwa ngumu kampuni kukua.

6. Increase in consumpition.

Bei za bidhaa zikiwa chini, hii inaweza fanya watu wengi wanunue bidhaa hata kama walikuwa hawana uhitaji nazo.

Kumbuka the lower the price, the higher the demand.

Mfano:

Bei ya kupanda mlima kilimajaro ikiwa chini basi hii inaweza sababisha watalii kuongezeka, na hii itasababisha kukuwa kwa sector nyengine za biashara na kukuza uchumi wa nchi.

7. Kuua viwanda vyengine.

Kmama mnakumbuka kwenye oligopoly, muuzaji mpya akiingia na akashusha bei zaidi ya wenzake ili kupata wateja wengi basi wale oligopoly watashusha chini zaidi , ili kuhakikisha muuzaji mpya ashindwe kupata faida na mwishowe afunge biashara, akifunga biashara wao watapandisha bei zaidi kwasababu wamebaki wachache.

Kwahiyo bei kuwa chini kuna wazalishaji wengine watashindwa kumudu gharama za uzalishaji, na kupata hasara na kuona ni kheri wafunge biashara.

Pia bidhaa zinazotoka nje zikiletwa kwa bei rahisi basi inakuwa ngumu nchi husika kuwa na viwanda, maana uzalishaji wa nchi za nje una faida ya teknolojia kuwa juu, na economies of scale kutokana na mitaji mikubwa. Hii hupelekea viwanda vya ndani ya nchi kushindwa kuendelea kuzalisha kwasababu bei zao zitakuwa juu na hamna atakayenunua.

Note:

Mara nyingi thamani ya pesa ikiongezeka, upatikanaji wa hio pesa huwa mgumu sana na hiki sio kitu kizuri kwa maendeleo.

Toa mfano wa mikoa ambayo vitu vyake ni bei rahisi ila kuipata hio hela ni changamoto.

Karibuni sana wachangia mada.

#uchumi #deflation #economics
 
Umesema daraja kuharibika kuwa wakulima watahitajika kuuza kwa bei ya chini. Kutafanya bei ya bidhaa kuwa chini. Hapo No bidhaa ikiadimika itapata bei kwa sabab demand itakuwa kubwa kuliko supply
 
Umesema daraja kuharibika kuwa wakulima watahitajika kuuza kwa bei ya chini. Kutafanya bei ya bidhaa kuwa chini. Hapo No bidhaa ikiadimika itapata bei kwa sabab demand itakuwa kubwa kuliko supply
yes upande wa pili ambapo ndio huwa wananunua hio bidhaa, ila kwa wale wa pale kijijini kwasababu wote ni wakulima hakuna wa kumuuzia mwenzake ni hasara.
 
Back
Top Bottom