Thamani/umuhimu wa watu.

Husninyo

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
23,723
9,190
Hivi umeshawahi kufikiria siku utakayoamka unajikuta upo peke yako nyumba nzima, njiani hukuti mtu, unafika kwenye kituo cha daladala magari yapo ila hakuna mtu, ofisini napo hukuti mtu.
Unajihisi mpweke unaamua uwapigie simu watu wako ila Simu zinaita hazipokelewi. unafungua JF unakuta threads kibao ila hakuna mtu online.
Unagundua kuwa umeachwa mwenyewe hapo ndipo unaanza kuona umuhimu wa watu.

Umuhimu wa watu huonekana pale tunapowakosa ila hatutakiwi tusubiri hadi tuwakose ndio tuoneshe kuwa wao ni muhimu kwetu.
Wana jf wote ni muhimu kwangu na ninawapenda sana, sitaki kusubiri hadi niwakose ndio mjue mlikuwa muhimu kwangu.
Nawatakia siku njema na mungu awabariki.
 
Kama ulivyo muhimu kwa wanaJF Hus!Asante mwaya...umenikumbusha kuwa karibu na watu flani kabla sijawapoteza!
 
Konakali unavyofanya sio vizuri tokea mwaka jana maana niliishakupoteza usipotee tena sio vizuri banaa
 
Kama ulivyo muhimu kwa wanaJF Hus!Asante mwaya...umenikumbusha kuwa karibu na watu flani kabla sijawapoteza!

ahsante mpendwa.
Ukiwapoteza kabla hujawaonesha wao ni muhimu itapain zaidi.
 
Sijwahi kukosa WATU ndiyo maana sijui umuhimu wa WATU!

- Nyumbani nina extended family tupo 20

- Kwenye Kituo Cha Daladala Mbagala Mwisho ni Umati wa watu 24/7

- Kwenye DalaDala nyomi kama kawa

- Ofisini kwetu sisi ni makuli na kuna wengine wanasubiria mmoja afe waingie mzigoni

- JF Online members at any given day ni 6,000 na ushee

WATU ni wengi saaaaaaaaaaaana!
 
Hivi umeshawahi kufikiria siku utakayoamka unajikuta upo peke yako nyumba nzima, njiani hukuti mtu, unafika kwenye kituo cha daladala magari yapo ila hakuna mtu, ofisini napo hukuti mtu.
Unajihisi mpweke unaamua uwapigie simu watu wako ila Simu zinaita hazipokelewi. unafungua JF unakuta threads kibao ila hakuna mtu online.
Unagundua kuwa umeachwa mwenyewe hapo ndipo unaanza kuona umuhimu wa watu.

Umuhimu wa watu huonekana pale tunapowakosa ila hatutakiwi tusubiri hadi tuwakose ndio tuoneshe kuwa wao ni muhimu kwetu.
Wana jf wote ni muhimu kwangu na ninawapenda sana, sitaki kusubiri hadi niwakose ndio mjue mlikuwa muhimu kwangu.
Nawatakia siku njema na mungu awabariki.

na kuna wakati watu fulani wanakukera lakini wakitoweka unawakumbuka tena kwa hiyo unagundua kumbe ulikuwa unawahitaji pamoja na kwamba hukuwa unawapenda
 
Sijwahi kukosa WATU ndiyo maana sijui umuhimu wa WATU!

- Nyumbani nina extended family tupo 20

- Kwenye Kituo Cha Daladala Mbagala Mwisho ni Umati wa watu 24/7

- Kwenye DalaDala nyomi kama kawa

- Ofisini kwetu sisi ni makuli na kuna wengine wanasubiria mmoja afe waingie mzigoni

- JF Online members at any given day ni 6,000 na ushee

WATU ni wengi saaaaaaaaaaaana!
Kuwa wengi sio tatizo, wanaweza kuwa wengi lakini wakawa USELESS
 
Thanks Husninyo, wewe na jf ni wamuhimu sana, na hawa muuza vitumbua, duka, konda, maji, trafiki, madafu, chips nk.. nk. ni muhimu
 
Ahaaa ahaa ahaa Elia umenifurahisha na kunikumbusha mbali sana
 
Thanks Husninyo, wewe na jf ni wamuhimu sana, na hawa muuza vitumbua, duka, konda, maji, trafiki, madafu, chips nk.. nk. ni muhimu

Ha ha ha Ellia bana unapenda kula wewe umekumbuka wauza chakula tu ha ha ha ha vitumbua umenikumbusha mbali sana sijala nina miaka kama 10
 
Back
Top Bottom