DOKEZO TFF acheni ubabaishaji, wapeni watu hela zao

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Boran Jakutay

Senior Member
Apr 8, 2023
110
255
Ikiwa imepita mwezi mmoja tangu kutolewa kwa Tuzo za TFF 2023, kuna malalamiko yameibuka juu ya zawadi za washindi.

Kwa mujibu wa mmoja wa washindi wa tuzo hizo, mpaka leo hawajakabidhiwa fedha walizoambiwa watapewa washindi.

Mbali na tuzo walizokabidhiwa siku ya sherehe, washindi waliahidiwa kupewa kiasi cha Sh 5,000,000.

Mtoa taarifa huyo alisema amekuwa akiwauliza viongozi wa TFF juu ya lini atapatiwa fedha zake, lakini amekuwa akipewa ahadi ambazo hazina mwisho wake.

"Siku ile ya sherehe za utoaji tuzo, walituambia tutapewa fedha zetu siku nyingine, mimi nikawa naulizia mara kwa mara fedha zangu nikawa naambiwa nisubiri, mwisho wa siku nikachoka, kiukweli sielewi lini tutapewa," alisema mtu huyo.

Mbali na hilo, mtu huyo alifichua kwamba, hata zile tuzo za kila mwezi, washindi wamekuwa wakizungushwa sana kupatiwa fedha zao kiasi ambacho kwao wanaona si sawa kwani hawapewi sababu za msingi.

===

UPDATE
JamiiForums imefanyia kazi suala hili.

1. Tuzo za TFF 2023

Kuhusu ucheleweshwaji wa zawadi ya fedha kwa washindi wa Tuzo za TFF 2023, Afisa Habari wa Bodi ya Ligi, Karim Boimanda anafafanua:

Hatujawahi kutangaza tarehe ya kutoa zawadi ya fedha, hakuna mshindi aliyeahidiwa wala kuambiwa fedha atalipwa siku fulani, ni ajabu sana kusikia kuwa kuna mtu anasema hajapewa fedha, ni tuzo chache Duniani ambazo mtu anapewa fedha hapohapo jukwaani.

Suala la zawadi ni mambo kati ya TFF na washindi wa Tuzo ndio maana haikutangazwa pale hadharani, mchakato unahusisha wadhamini n.k, fedha huwa haitangazwi itatoka lini, inawezekana wapo waliopewa lakini hawawezi kusema kama wamepewa.

Kwenye suala la Tuzo mambo kama hayo siyo habari na hatuwezi kutangaza lini tutatoa fedha au tumezitoa lini.
Siwezi kukwambia kama fedha zimetoka au hazijatoka kwa kuwa suala hilo haliwahusu watu wengine wote kwa kuwa linahusu ni fedha."

2. Tuzo za Mwezi
Madai kuwa Tuzo za Mwezi napo kuna ucheleweshwaji wa zawadi ya fedha, Afisa Habari wa Bodi ya Ligi, Karim Boimanda anafafanua:

"Hapo pia majibu ni yaleyale, Tuzo inatolewa hadharani na kamera zinamulika lakini fedha hazionekani, hao wanaosema wamecheleweshewa siku wakipewa wanasema kwenye Vyombo vya Habari? Nasisitiza stori ya fedha siyo stori kabisa, hiyo inahusu mshindi na TFF."
 
Karia anazizungushia kwenye ngao ya hisani Tanga, baada ya ngao mtalipwa fedha zenu kuweni na uvumilivu
 
Tumeelewa wanachomaanisha hapo, wale tuliosoma Cuba.
 
Ni aibu taasisi kubwa kutoa zawadi kwa ahadi alafu inachukua muda mrefu bila kuwapa wahusika.
 
Back
Top Bottom