Tetesi: Zitto kufanya press conference Dar!!!?

Status
Not open for further replies.

Kiranja

JF-Expert Member
May 19, 2007
751
336
Kuna taarifa kwamba Zitto Zubeir Kabwe na Peter Serukamba wanatarajiwa/wanafanya/wamefanya press conference ya pamoja jijini Dar es Salaam leo.

Sina hakika kama wanazungumzia nini, lakini tetesi zinaweza kuwa wanazungumzia tatizo la umeme mmkoani Kigoma na kwamba wao ndio wanaojua shida ya umeme na kwamba bora mitambo ya Dowans inunuliwe ipelekwe huko Kigoma.

Kimya kimezidi na kwamba hakuna kati yao anayesema wazi kuhusiana na hayo. Mwenye hayo atuambie, waandishi tujulisheni. Kunani?
 
Last edited by a moderator:
Sasa ndio inadhihilisha kuwa Zitto Dowans ameishaingia kwenye anga za mafisadi; toka lini yeye na Serukamba wakashare podium moja? Kama ni suala la umeme wa Kigoma basi hiyo press conference ingehudhuliwa na wabunge wote wa kutoka Kigoma angalau hata Manju Msambya kama wengine hawatapatikana !!It is unfortunate that this young politician is polluting himself even further.
 
Aisee huyu bwana mdogo Zitto Dowans anaanza kuchafua hali ya hewa!!Walio karibu naye huko Tz .Pamoja na Tanesco kutangaza kununua mitambo mipya miwili yenye kuzalisha 160MW yeye bado anang'ang'ania Dowans!
 
I ll put my opinion jus wen there z a confirmation of such an event....
Ntakuwa na meeengi ya kuchangia,but as for now lemme hold ma breath!
 
Hold on, you are too quick to make judgements! Hata hamjathibitisha kama huo mkutano ulikuwepo na kitu kiliongelewa tayari mmeshaanza kumwaga radhi, nyie watu mna mambo sio kidogo!!
 
Hold on, you are too quick to make judgements! Hata hamjathibitisha kama huo mkutano ulikuwepo na kitu kiliongelewa tayari mmeshaanza kumwaga radhi, nyie watu mna mambo sio kidogo!!

Uko sahihi kaka. Bado ni tetesi na kwamba tunamtafuta na kuthibitisha kama kweli ama la. Lakini kama wakizungumzia masuala yao ya Kigoma kama wabunge wa Kigoma. Nadhani Zitto ni kiongozi katika kamati yao ya wabunge wa Kigoma kwa hiyo haitakuwa vibaya na kama hawatahusisha siasa za sasa za Dowans na mengineyo. Lakini kama atakuwa anaimba wimbo ule ule wa kawaida kwa kweli wachezaji watakua wale wale na wengine tutaendelea kuona kama vile kwaya ya Kanisani kuimbwa kwa sauti ya juu na vijana wa madrasa (Zitto) pale Msikitini ama
 
Kimya kingi kina mshindo mkuu. Nina hakika Zitto ataibuka na jambo ZITO
 
Hii maneno mbofu mbofu natoka wapi tena? sasa kama wanakutana pamoja kuongea kuhusu Ujiji kuwa gizani nyie chawauma nini? kinachoudhi tu ni kwamba wale wenzao wa Kasulu Kibondo wapo wapo tu!hata hawasikiki nchi toka uhuru no elektirisiti ni ahadi after ahadi!wakipewa uwaziri ndio basi tena wanahamishia makao yao makuu Dasiramu, Wapiga kura wa Kasulu na Kibondo wanapaswa kuzinduka sasa, kura kwa mwenyeji halisi wa maeneo hayo sio hawa koraptedi na maisha ya mjini, hawana hata huruma na wapiga kura wao! walau jaribuni kumpa kura mgombea ambaye hana makazi Dasilamu Mwanza wala mji wowote mkubwa na mkataba uwe kwa miaka mitano hakuna kununua kiwanja wala nyumba ya mjini! akimaliza masuala ya kupigania bungeni anarudi jimboni kuungana na wapiga kura wake mpaka kieleweke!
 
Kleptomaniacs,
Naamini na yawezekana nikawa niko sahihi, 3/4 ya wabunge, Bunge la jamhuri ya Muungano wa TZ wana makazi Dar. Hilo tuliache. Pengine ingawa Kitila Mkumbo ametuomba tuwe na subira na press conference ya Zitto na mwenzake Serukamba, lakini nachelea kusema kuwa, wale ni vijana wa sasa, damu changa, waleta mabadiliko katika majimbo yao. Wakiungana pamoja kuhusu 'common interest' tofauti ya vyama lazima waiweke kando,nawafagilia kwa hili. Kweli kuna wabunge wa kibondo (yeye anakula kuku kwani ni Naibu waziri) na yule wa kasulu(sijui aliko) ambao kwenye majimbo yao suala la umeme labda wananchi wao wanauona umeme wa generators za wafanya biashara, hawa jama wa kibondo na kasulu, wanashughulika na mambo yao na hawana muda wa kuungana na wenzao wa kigoma mjini na kasikazini kudai umeme. Ebu tusubiri matokeo ya press conference then tutasema
 
I refuse to speculate. I will wait until a definitive statement is made.

One thing is clear, the increased transparency and culture of open press conferences catching on will do more to reveal the nature of our public servants and representatives.Unlike some overly controlling bureaucrats -Speaker Samwel Sitta to name one- who are concerned that transparency will disturb further the existing order -read ufisadi and obfuscating secrecy- I think this is a positive trend any way you cut it.

Let's get it from the horse' mouth, let's get the audio and video if possible, let's post it up here and then we can bombard it with the energy of some CERN particle accelerator.
 
Sasa sijui Serukamba atapanda ndege ya saa ngapi kuwahi Dar na kurudi US! Hivi hawa wanaotoa habari hizi wanajua hata watu hawa walipo? Niliwahabarisha hapa kuwa Serukamba anakuja US hakuna anayejiuliza kama amesharudi?
 
Sasa ndio inadhihilisha kuwa Zitto Dowans ameishaingia kwenye anga za mafisadi; toka lini yeye na Serukamba wakashare podium moja? Kama ni suala la umeme wa Kigoma basi hiyo press conference ingehudhuliwa na wabunge wote wa kutoka Kigoma angalau hata Manju Msambya kama wengine hawatapatikana !!It is unfortunate that this young politician is polluting himself even further.

Ana ji pollute vipi? Infact Tanzania ya sasa inataka politicians kama hawa ambao panapo tokea maslahi ya taifa au wananchi wao waliowapigia kura, wanaweka pembeni itikadi zao za kisiasa na wanashirikiana kuondo tatizo. Sio kung'ang'ania tu m simamo unaoathiri taifa simply because utaonekana unamatatizo kichama.

Incidentally, jana huko Kilimjaro, Mbowe amewaeleza wanachama wake wa Chadema kuwa, panapokuwa jambo la maendeleo, washirikiane kikamilifu na viongozi walioko madarakani bila kujali kuwa wanatoka katika chama gani.

Nadhani sasa neno ufisadi limeanza kupoteza maana yake kwani linatumika vibaya kama hapo juu.
 
Rwabugiri.. huu mchezo wa "press conference" ni mazingaombwe yao tu..! Kuna mtu amekuwa akiwachezea watu akili...
 
Rwabugiri.. huu mchezo wa "press conference" ni mazingaombwe yao tu..! Kuna mtu amekuwa akiwachezea watu akili...

Thanks Mzee, halafu kuna watu humu wanaona kama wakirusha kila tetesi sijui ndio wataheshimika au vipi!!!!!!!!!!

Hii tetesi ya press conference sasa inakera.... kama ningekuwa moderator ningeifutilia mbali

:mad:
 
Sasa sijui Serukamba atapanda ndege ya saa ngapi kuwahi Dar na kurudi US! Hivi hawa wanaotoa habari hizi wanajua hata watu hawa walipo? Niliwahabarisha hapa kuwa Serukamba anakuja US hakuna anayejiuliza kama amesharudi?

Labda atashiriki kwa satellite.....
 
Kama wanazungumzia matatizo ya umeme kigoma kwanini press comf isifanyike huko kgm? Wana jf mi ni mgeni jamvini hata glass moja ya maji sijamaliza naomba mnikaribishe
 
Status
Not open for further replies.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom