Kuna vitu kuhusu watu maarufu kama viongozi, wasanii nk. tuliwahi kuambiwa tukiwa wadogo na hata ukubwani ambavyo kwa kweli vilisisimua. Tatizo kuhusu nyepesi hizo ilikuwa ni vigumu kuziona au kusikia katika vyombo vya habari. Hivyo ukweli wake umekuwa ni jambo la kujiongeza mwenyewe. Hizi zifuatazo zilinisisimua sana - kama kuna nyingine tushirikishane tuzijue na kwa mwenye kujua ukweli wake pia ni vizuri akatusaidia.
1. Mwl. Nyerere alimpa Malkia wa Uingereza kifimbo badala ya mkono eti kisa Malkia alikuwa amevaa gloves
2. Dr. Hastings Kamuzu Banda alihasiwa kwa kuwa alikuwa daktari wa Malkia
3. Marvin Gaye aliuawa na baba yake eti kwa kuwa Marvin alikuwa shoga
4. Rais Jomo Kenyatta aliwahi kumtakia Mwl. Nyerere kuwa kuongoza Tanzania ni kama kuongoza maiti
5. Michael Jackson aliwahi kusema kuwa Dar es Salaam inanuka