Tetesi: Shughuli zote kusimama Mtwara leo kushinikiza Murji aachiwe

tenende

JF-Expert Member
Jan 10, 2012
6,511
500
Tetezi nilizozipata kutoka kwa wakazi wawili wa mtwara (ambao ni wafanyabiashara) zinasema kwamba wakazi wa mtwara leo wanafanya mgomo baridi bila kupambana na mtu ili kushinikiza mbunge wao aachiwe. Wamepanga kutofungua biashara yoyote wala kuendesha maandamano ya aina yoyote kwa siku nzima ya leo.

Wafanya biashara hao wawili walifuata mzigo Dar na sasa wameamua kusubiri siku ya kesho ipite ndipo waende.

Big show tupe taarifa!

Huko mtwara inabidi vijana wa FFU Ukonga AKA Ghasia kuu waende kupiga kambi kama mwezi tu na nina uhakika hatutasikia tena akina njomba wanchema tuchimumunye wala tuchiteme
 
Lukosi, FFU wakati wanataka wasikilizwe? Sio kila kitu ni mtulinga.
 
Huko mtwara inabidi vijana wa FFU Ukonga AKA Ghasia kuu waende kupiga kambi kama mwezi tu na nina uhakika hatutasikia tena akina njomba wanchema tuchimumunye wala tuchiteme

Lukosi,
Haya bwana. Mtumikie kafiri upate mtaji. Hoja zako mara nyingi naona kuwa zinazidi upenzi. Hebu jiweke miguuni kwa Mwanamtwara au Mtanzania wa kawaida, unaweza kupendekeza kukaliwa na FFU kwa madai ambayo kimsingi kuna chembechembe za ukweli ndani yake?
 
Huko mtwara inabidi vijana wa FFU Ukonga AKA Ghasia kuu waende kupiga kambi kama mwezi tu na nina uhakika hatutasikia tena akina njomba wanchema tuchimumunye wala tuchiteme
Huijui Mtwara wewe! kule hawakai watu wanaofikiri kujinyonga kama wewe! kule kuna watu wakisema hawataki wanamaanisha hawataki! hawana ndimi mbili kama wewe muoga.
 
Huko mtwara inabidi vijana wa FFU Ukonga AKA Ghasia kuu waende kupiga kambi kama mwezi tu na nina uhakika hatutasikia tena akina njomba wanchema tuchimumunye wala tuchiteme

Nini FFU? Huko wametumwa mpaka JW lakini ngoma bado mbichi.kosa ni hilo kudhani kuwa nguvu zitamaliza mgogoro huu.serikali inajidanganya. wengi wa watu walioko serikalini wanawaona wamakonde wajinga fulani, wamekosea. ni watu wenye msimamo na wako focused kwenye jambo hili.
kusimamisha huduma za kijamii leo hakuna uhusiano wa kukamatwa mbunge wao kwani jambo hili lilisha pangwa karibu wiki mbili hivi kabla.serikali ijipange, kwani kadiri wanavyo kamata watu ndivyo wenyewe wanavyo zidi kuungana against the GOVERNMENT.
 
Mkuu kuina kipindi lazima ujue kuwa kuna serikali
 
Huko mtwara inabidi vijana wa FFU Ukonga AKA Ghasia kuu waende kupiga kambi kama mwezi tu na nina uhakika hatutasikia tena akina njomba wanchema tuchimumunye wala tuchiteme
Nilidhani mapepo yanaendelea kukutoka kumbe ndio kwanza yanaendelea kukuingia!
 
Matokeo ya akili finyu ya viongozi, kudhani kulazimisha mambo kama zamani kunawezekana, wasukuma tumeaachiwa mashimo tu uko Shinyanga na Mwanza, upande wangu wa kizanaki ndio usiseme, Musoma hawajafanya lolote lile, kukumbatia wawezekaji na ulaji wao tu.

Kung'ang'ania kujenga ilo bomba kuna naamna, hata sie tupo upande wa wanamtwara.
Wangekua viongozi makini, haya mambo yasingefika huko, ila wao watalazimisha issue, FFU na JWTZ, mpaka polisi, wakishindwa kabisa, wataanza kuhonga, ili wanamtwara wafarakane, mbona mbinu zao tunazijua.......
 
Huko mtwara inabidi vijana wa FFU Ukonga AKA Ghasia kuu waende kupiga kambi kama mwezi tu na nina uhakika hatutasikia tena akina njomba wanchema tuchimumunye wala tuchiteme

Nina wasiwasi na mafanikio yako pengine una godfather, yaani katika kufikiri kwako huo ndio uamuzi wa busara uliouona?kwa ufahamu wako ndio maana unatapatapa mara leo nywele kesho ndevu mwisho utakuwa mav****. Tafakari chukua hatua.
 
Mgomo huo utakuwa wanawatesa wananchi wenzao masikini.
 
Siku zote vita vya panzi, furaha ya kunguru. Mtwara fanyeni kazi acheni kushindana na Serikali, katika kutafuta haki lazima sheria ichukue nafasi yake.
 
Hivi Cris Lukosi unaelewaga unacho comment?

Nakushauri ukasome course moja inaitwa " Critical thinking and logical argumentation"

Poor jf member

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Nilidhani mapepo yanaendelea kukutoka kumbe ndio kwanza yanaendelea kukuingia!

Mkuu!

Wewe subiria. Ni suala la muda utaona matokeo yake. Nilisha sema hapa kwamba "ATALAANIWA YEYE NA UZAO WAKE WOTE". Na hata huku anako jipendekeza siku yaja watamuona kama kinyesi tuu!

Mkuu! Weka maneno haya katika kumbukumbu zako na utaniaminia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…