Tetesi: Shughuli zote kusimama Mtwara leo kushinikiza Murji aachiwe


T

tenende

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2012
Messages
6,559
Likes
10
Points
135
T

tenende

JF-Expert Member
Joined Jan 10, 2012
6,559 10 135
Tetezi nilizozipata kutoka kwa wakazi wawili wa mtwara (ambao ni wafanyabiashara) zinasema kwamba wakazi wa mtwara leo wanafanya mgomo baridi bila kupambana na mtu ili kushinikiza mbunge wao aachiwe. Wamepanga kutofungua biashara yoyote wala kuendesha maandamano ya aina yoyote kwa siku nzima ya leo.

Wafanya biashara hao wawili walifuata mzigo Dar na sasa wameamua kusubiri siku ya kesho ipite ndipo waende.

Big show tupe taarifa!

*Wananchi wakimbia tena makazi yao
*Serikali yapita mitaani na vipaza sauti
WAKATI Mbunge wa Mtwara Mjini, Hasnain Murji (CCM) na viongozi kadhaa wa vyama vya siasa wakitarajia kupandishwa mahakamani leo, hofu kubwa ya kutokea machafuko imetanda katika mitaa mbalimbali mjini hapa.


Mbali ya Murji, viongozi wengine wanaoshikiliwa majina na vyeo vyao kwenye mabano ni Katani Ahmed Katani (33), Said Kulaga (CUF), Hassan Uled (NCCR-Mageuzi), Hamza Licheta (TLP), ambao wote kwa pamoja wanadaiwa kuunganika kulisema suala la gesi.

Murji, amekamatwa kwa kile kinachodaiwa alitoa kauli ya uchochezi Desemba 31, mwaka jana katika ukumbi wa Kanisa la Pentekoste uliopo mjini hapa, ambapo aliwaambia wananchi anaungana nao kupinga mpango wa Serikali kusafirisha gesi kwenda Dar es Salaam kwa njia ya bomba.

"Katika mkutamo huo, alisema; "mimi mbunge niliyechaguliwa na wananchi wa jimbo la Mtwara Mjini na wananchi wa jimbo hili ndio walionipa ridhaa ya kuwawakilisha Bungeni, ndio walioniajiri kuwatumikia, kwa hiyo naungana nao kwa moyo mmoja kuhakikisha haki na mahitaji yenu ya msingi yanapatikana," alisema Murji.

Kutokana na kutanda kwa hofu hiyo, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mtwara, juzi ililazimika kukutana katika kikao cha dharura.

Habari zinasema, katika kikao hicho, moja ya ajenda kubwa iliyokubaliwa ni uongozi wa mkoa kutoa magari yaliyofungwa spika kubwa, ili kuzunguka mitaani na kuwaomba wananchi wasijaribu kukimbia makazi yao kwa kuhofia fujo.

Hali hiyo, ilionekana jana wakati gari la halmashauri ya Mtwara Mikandani ilipoanza kuzunguka, huku ‘MC' akiwaasa wananchi kutoacha makazi yao, bali waendelee na shughuli zao za kila siku kama kawaida.

Kabla ya kamati hiyo kukutana juzi, kulikuwa na uvumi na vitisho kutoka sehemu mabambali mjini hapa, unaowataka wananchi wote kufunga huduma zote za kijamii leo na kwenda Mahakama ya Hakimu Mkazi.

"Tangazo, tangazo, tangazo, tunapenda kuwatangazia wananchi wote wa Manispaa ya Mtwara Mikindani kuwa uvumi na vitisho vinavyoenezwa siku ya Jumatatu Juni 10, mwaka huu, vinavyowataka musitishe huduma zote za kijamii ili muelekee mahakamani kusikiliza kesi ya watu waliokamatwa kutokana na vurugu zilizotokea hivi karibuni… tunawaomba wananchi msikubaliane kabisa na kauli hizo… endeleeni na shughuli zenu za kila siku kama kawaida.

"Wananchi wote endeleeni kama kawaida na shughuli zenu na wala musiogope kitu chochote, atakayefanya vurugu ama fujo atashugulikiwa mara moja, Jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ), lipo kwa ajili ya kulinda amani ya nchi," alisema MC huyo.

Katika hali ya kushangaza, ‘MC' huyo alikuwa akisindikizwa na magari mawili ya askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

STENDI KUU
Licha ya tangazo hilo, MTANZANIA ilifika stendi kuu ya mabasi mjini hapa na kushuhudia mamia ya watu wakipanda mabasi kuelekea mikoa ya Dar es Salaam na Lindi.

Kitendo hicho, kimeonekana wazi kuwashtua watu wengi, ambao walisema inawezekana wananchi hao wameamua kikimbilia nje ya Mtwara kuhofia fujo ambazo zinaweza kutokea.

Mmoja wa abiria hao, Maalim Omar Kifule alisema ameamua kuondoka ili kuokoa maisha yake pamoja na familia.

"Mie naelekea Dar es Salaam, siwezi kuendelea kukaa kama ulivyosikia kesho (leo), kunaweza kutokea machafuko, licha ya Serikali kusema ulinzi umeimarishwa," alisema Kifule.

"Hata kama wanasema JWTZ wapo, watatulinda sisi raia na mali zetu, siwezi kabisa kufungua biashara yangu naogopa kuaribiwa bidhaa zangu… wapo watu ambao wanapita mitaani kuangalia nani kafungua na nani kafunga…sasa wapite wanikute nimefungua biashara yangu, watasema nimewasaliti wana Mtwara, nina raha gani mpaka nifungue biashara siku hiyo," alisema mfanyabiashara ambaye hakutaka jina lake litajwe gazeteni.

Mei 17, mwaka huu mji mzima wa Mtwara, ulisitisha huduma za kijamii kutokana na fujo kubwa iliyoambatana na uharibifu wa mali zilizosababishwa na wananchi kujichukulia sheria mkononi.

Baada ya fujo, tukio kama hilo lilijirudia tena Mei 22 na 23, ambapo huduma zote zilisitishwa kutokana na wasiwasi huo.

Akizungumza na gazeti hili maeneo ya Stendi hiyo, Husseni Chipoko, Mkazi wa Mbeya Mjini hapa, alisema yeye alifika stendi kwa ajili ya kusafirisha familia yake kwenda Dar es Salaam, hadi hali itakapotulia.

"Nimeamua kusafirisha familia yangu kwenda jijini Dar es Salaam, kutokana na uvumi ulioenea kuwa siku ya Juni 10 mwaka huu watu wote wasitishe huduma za kijamii ili waende Mahakamani…sasa mimi naogopa yasije yakatokea kama yale ya mwanzo.

RPC MTWARA
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Linusi Sinzumwa alipoulizwa kuhusiana na hali hiyo, alikiri kuwapo na uvumi huo na kusisitiza kuwa Serikali imejipanga vizuri kukabiliana na hali hiyo.

"Kumekuwapo na maeneo ya mitaani tu, lakini tunawaomba wananchi wakae na waendelee na shughuli zao kama kawaida," alisema Kamanda Sinzumwa.
 
Chris Lukosi

Chris Lukosi

Tanzanite Member
Joined
Aug 23, 2012
Messages
4,586
Likes
35
Points
145
Chris Lukosi

Chris Lukosi

Tanzanite Member
Joined Aug 23, 2012
4,586 35 145
Huko mtwara inabidi vijana wa FFU Ukonga AKA Ghasia kuu waende kupiga kambi kama mwezi tu na nina uhakika hatutasikia tena akina njomba wanchema tuchimumunye wala tuchiteme
 
T

tenende

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2012
Messages
6,559
Likes
10
Points
135
T

tenende

JF-Expert Member
Joined Jan 10, 2012
6,559 10 135
Mmmmhh Mtwara nako!...
 
M

mahoza

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2012
Messages
1,246
Likes
415
Points
180
Age
57
M

mahoza

JF-Expert Member
Joined Mar 11, 2012
1,246 415 180
Lukosi, FFU wakati wanataka wasikilizwe? Sio kila kitu ni mtulinga.
 
Nono

Nono

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2008
Messages
1,347
Likes
144
Points
160
Nono

Nono

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2008
1,347 144 160
Huko mtwara inabidi vijana wa FFU Ukonga AKA Ghasia kuu waende kupiga kambi kama mwezi tu na nina uhakika hatutasikia tena akina njomba wanchema tuchimumunye wala tuchiteme
Lukosi,
Haya bwana. Mtumikie kafiri upate mtaji. Hoja zako mara nyingi naona kuwa zinazidi upenzi. Hebu jiweke miguuni kwa Mwanamtwara au Mtanzania wa kawaida, unaweza kupendekeza kukaliwa na FFU kwa madai ambayo kimsingi kuna chembechembe za ukweli ndani yake?
 
Gwalihenzi

Gwalihenzi

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2011
Messages
5,116
Likes
52
Points
145
Age
58
Gwalihenzi

Gwalihenzi

JF-Expert Member
Joined Oct 21, 2011
5,116 52 145
Huko mtwara inabidi vijana wa FFU Ukonga AKA Ghasia kuu waende kupiga kambi kama mwezi tu na nina uhakika hatutasikia tena akina njomba wanchema tuchimumunye wala tuchiteme
Huijui Mtwara wewe! kule hawakai watu wanaofikiri kujinyonga kama wewe! kule kuna watu wakisema hawataki wanamaanisha hawataki! hawana ndimi mbili kama wewe muoga.
 
J

JERUSALEMU

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2012
Messages
2,756
Likes
1,829
Points
280
J

JERUSALEMU

JF-Expert Member
Joined Sep 19, 2012
2,756 1,829 280
Huko mtwara inabidi vijana wa FFU Ukonga AKA Ghasia kuu waende kupiga kambi kama mwezi tu na nina uhakika hatutasikia tena akina njomba wanchema tuchimumunye wala tuchiteme
Nini FFU? Huko wametumwa mpaka JW lakini ngoma bado mbichi.kosa ni hilo kudhani kuwa nguvu zitamaliza mgogoro huu.serikali inajidanganya. wengi wa watu walioko serikalini wanawaona wamakonde wajinga fulani, wamekosea. ni watu wenye msimamo na wako focused kwenye jambo hili.
kusimamisha huduma za kijamii leo hakuna uhusiano wa kukamatwa mbunge wao kwani jambo hili lilisha pangwa karibu wiki mbili hivi kabla.serikali ijipange, kwani kadiri wanavyo kamata watu ndivyo wenyewe wanavyo zidi kuungana against the GOVERNMENT.
 
Chris Lukosi

Chris Lukosi

Tanzanite Member
Joined
Aug 23, 2012
Messages
4,586
Likes
35
Points
145
Chris Lukosi

Chris Lukosi

Tanzanite Member
Joined Aug 23, 2012
4,586 35 145
Nini FFU? Huko wametumwa mpaka JW lakini ngoma bado mbichi.kosa ni hilo kudhani kuwa nguvu zitamaliza mgogoro huu.serikali inajidanganya. wengi wa watu walioko serikalini wanawaona wamakonde wajinga fulani, wamekosea. ni watu wenye msimamo na wako focused kwenye jambo hili.
kusimamisha huduma za kijamii leo hakuna uhusiano wa kukamatwa mbunge wao kwani jambo hili lilisha pangwa karibu wiki mbili hivi kabla.serikali ijipange, kwani kadiri wanavyo kamata watu ndivyo wenyewe wanavyo zidi kuungana against the GOVERNMENT.
Mkuu kuina kipindi lazima ujue kuwa kuna serikali
 
H

Honolulu

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2012
Messages
5,650
Likes
35
Points
145
H

Honolulu

JF-Expert Member
Joined Jan 20, 2012
5,650 35 145
Huko mtwara inabidi vijana wa FFU Ukonga AKA Ghasia kuu waende kupiga kambi kama mwezi tu na nina uhakika hatutasikia tena akina njomba wanchema tuchimumunye wala tuchiteme
Nilidhani mapepo yanaendelea kukutoka kumbe ndio kwanza yanaendelea kukuingia!
 
jebs2002

jebs2002

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2008
Messages
6,018
Likes
3,833
Points
280
jebs2002

jebs2002

JF-Expert Member
Joined Sep 3, 2008
6,018 3,833 280
Matokeo ya akili finyu ya viongozi, kudhani kulazimisha mambo kama zamani kunawezekana, wasukuma tumeaachiwa mashimo tu uko Shinyanga na Mwanza, upande wangu wa kizanaki ndio usiseme, Musoma hawajafanya lolote lile, kukumbatia wawezekaji na ulaji wao tu.

Kung'ang'ania kujenga ilo bomba kuna naamna, hata sie tupo upande wa wanamtwara.
Wangekua viongozi makini, haya mambo yasingefika huko, ila wao watalazimisha issue, FFU na JWTZ, mpaka polisi, wakishindwa kabisa, wataanza kuhonga, ili wanamtwara wafarakane, mbona mbinu zao tunazijua.......
 
leipzig

leipzig

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2013
Messages
2,655
Likes
729
Points
280
leipzig

leipzig

JF-Expert Member
Joined Jan 9, 2013
2,655 729 280
Huko mtwara inabidi vijana wa FFU Ukonga AKA Ghasia kuu waende kupiga kambi kama mwezi tu na nina uhakika hatutasikia tena akina njomba wanchema tuchimumunye wala tuchiteme
Nina wasiwasi na mafanikio yako pengine una godfather, yaani katika kufikiri kwako huo ndio uamuzi wa busara uliouona?kwa ufahamu wako ndio maana unatapatapa mara leo nywele kesho ndevu mwisho utakuwa mav****. Tafakari chukua hatua.
 
C

COPPER

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2012
Messages
2,054
Likes
632
Points
280
C

COPPER

JF-Expert Member
Joined Dec 28, 2012
2,054 632 280
Tetezi nilizozipata kutoka kwa wakazi wawili wa mtwara (ambao ni wafanyabiashara) zinasema kwamba wakazi wa mtwara leo wanafanya mgomo baridi bila kupambana na mtu ili kushinikiza mbunge wao aachiwe. Wamepanga kutofungua biashara yoyote wala kuendesha maandamano ya aina yoyote kwa siku nzima ya leo.

Wafanya biashara hao wawili walifuata mzigo Dar na sasa wameamua kusubiri siku ya kesho ipite ndipo waende.

Big show tupe taarifa!

Mgomo huo utakuwa wanawatesa wananchi wenzao masikini.
 
Mtoto halali na hela

Mtoto halali na hela

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2012
Messages
24,357
Likes
7,653
Points
280
Mtoto halali na hela

Mtoto halali na hela

JF-Expert Member
Joined Aug 10, 2012
24,357 7,653 280
Siku zote vita vya panzi, furaha ya kunguru. Mtwara fanyeni kazi acheni kushindana na Serikali, katika kutafuta haki lazima sheria ichukue nafasi yake.
 
G

gayo

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2011
Messages
243
Likes
15
Points
35
G

gayo

JF-Expert Member
Joined Feb 17, 2011
243 15 35
Hivi Cris Lukosi unaelewaga unacho comment?

Nakushauri ukasome course moja inaitwa " Critical thinking and logical argumentation"

Poor jf member

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
S

Selungo

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2009
Messages
1,272
Likes
1
Points
0
S

Selungo

JF-Expert Member
Joined Sep 23, 2009
1,272 1 0
Nilidhani mapepo yanaendelea kukutoka kumbe ndio kwanza yanaendelea kukuingia!
Mkuu!

Wewe subiria. Ni suala la muda utaona matokeo yake. Nilisha sema hapa kwamba "ATALAANIWA YEYE NA UZAO WAKE WOTE". Na hata huku anako jipendekeza siku yaja watamuona kama kinyesi tuu!

Mkuu! Weka maneno haya katika kumbukumbu zako na utaniaminia.
 

Forum statistics

Threads 1,273,280
Members 490,351
Posts 30,476,446