Tetemeko (la ardhi) latokea Dar

Mi nipo kinondoni nimehisi sakafu inatetemeka,baada ya sekunde chache ikarudia.
(kama vile underground train inapita)
 
Yah nipo hapa naona watu wote wapo nje kama vile kunaugeni wanausubiri!
Lakini naona hakuna madhara!!
 
Hata mimi nililisikia nikiwa Msewe, niliona bomba la maji likijichomoa kwenye tanki la maji juu ya nyumba ya jirani!
 
mh! naona mimi niko immune na hayo matetemeko - kila mtu kasikia katoka ofisini - mie WALA sikusikia chochote na nipo tu ofisini

mh! huenda nina special protection from Angels.....................
 
Naaam hata hapa Police Oysterbay pamepitiwa na hilo tetemo ila halikuwa na madhara zaidi ya vikombe kugongana. Michicha yaetu ipo salama.
 
mbona sijalisikia wala kulihisi? Mida hiyo nilikua nakunywa supu katikati ya cbd. Radio 1 sa 7 news wanasema huenda likajirudia
 
Nimesikiliza taarifa ya habari kupitia redio one saa 7:00 mchana,kuwa maeneo ya mjini leo yamekumbwa na tetemeko la ardhi. Wadau hii ikoje maana wengine tuko mbali kidogo na jiji.
 
Mbona sijasikia chochote mie? Ama limebagua? Nilikua maeneo ya chuo kikuu nyakati mnazosema limetokea
 
yeah, nipo mbagala, nimehisi ku shake pia! Ila hapa leo nimejifunza kitu! Kumbe member wengi wa jf wamesoma na wana ajira maofisini, kwani karibu kila member anasema ameshake na kwenye kiti chake ofisini! Kumbe na nyinyi ni moja kati ya watu ambao mnarudisha nyuma maendeleo ya taifa hili. Badala ya kufanya kazi ofisini kwenu mnatumia mda mwingi kutoa hoja na michango jf huku kazi na huduma zenu zikidorora! Sipendi kuona hili likiendelea tena kama kweli sisi ni wazalendo wa kweli!
 
kweli limetokea lakini sio tetemeko la ardhi ni mtikisiko kidogo tu. Tetemeko limetokea JAPAN, wa TANZANIA kwa kukuza mambo bwana
 
Most important Earthquake Data:
Magnitude : 4.8
UTC Time : Friday, June 10, 2011 at 08:28:13 UTC
Local time at epicenter : Friday, June 10, 2011 at 11:28:13 AM at epicenter
Depth (Hypocenter) : 10 km
Geo-location(s) :
Epicenter almost below Buuni Village
very close to Vikundu
44 km (28 miles) SE (125°) from DAR ES SALAAM, Tanzania
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom