Tetemeko (la ardhi) latokea Dar

fangfangjt

JF-Expert Member
Apr 25, 2008
571
139
Tetemeko (la ardhi) latokea dar, watu maeneo ya mjini wamelisikia

UPDATES:
Watu PPF tower wameambiwa watoke kwenye jengo

http://earthquake.usgs.gov/earthquakes/recenteqsww/Quakes/usc000440z.php

Magnitude 4.8 - TANZANIA
011 June 10 08:28:13 UTC
Earthquake Details

  • This event has been reviewed by a seismologist.

[URL="http://earthquake.usgs.gov/earthquakes/glossary.php#magnitude"]Magnitude
4.8

7.080°S, 39.628°E
10 km (6.2 miles)
TANZANIA
52 km (32 miles) ESE of DAR ES SALAAM, Tanzania
105 km (65 miles) SSE of Zanzibar, Tanzania
230 km (142 miles) SSE of Tanga, Tanzania
713 km (443 miles) SSE of NAIROBI, Kenya
horizontal +/- 25.9 km (16.1 miles); depth +/- 2.9 km (1.8 miles)
NST= 25, Nph= 26, Dmin=709.1 km, Rmss=1.34 sec, Gp= 83°,
M-type=body wave magnitude (Mb), Version=5

  • USGS NEIC (WDCS-D)
usc000440z

Date-Time Location Depth Region Distances Location Uncertainty Parameters Source Event ID
[/URL]
 
I see, ndo maana hapa kwenye kiti changu nimehisi kurushwarushwa kama mara mbili hivi, ila sikujua ni nini?
 
Yeah, hata mimi nimelisikia! Tusubiri wataalamu watupe yaliyojiri
 
Nipo maeneo ya kati kati ya Jiji la DSM. Kiasi cha dakika 4 zilizopita kumetokea tetemeko kiasi cha kuchezesha viti, meza na vitu kadhaa ndani ya jengo nililokuwemo.
Mwenye taarifa zaidi atujuze!
 
Ni kweli. Nipo maeneo ya Mtaa wa Samora, nimelisikia kiasi cha mara 2. Saa 5: 36
 
Hata mimi nimelisikia Jombaa, Lakini mbona hii habari umeiweka kwenye siasa, Au ni siasa imesababisha kutokea kwa tetemwko hilo?
 
Kwa huu ujenzi holela kila kona majengo yamebanana hakuna open space for gathering in case of any disaster tutapona kweli? Hapo ofisi za uhamiaji Sokoine drive palipokuwa na uwanja mkubwa wa parking, paameshafungwa kinapandishwa ki2 kipya. Sijui likitokea tetemeko kubwa au moto tutakimbilia wapi mji huu.
 
Wakuu, niko maeneo ya Tazara Dar es Salaam ofisi flani, sasa katika mwendo wa Sekunde kama 4 hivi nikasikia jengo lina tetemeka, kuangalia nje hamna lari wakitu kikubwa kilichoanguka. Nilipowauliza wenzangu wengi wakasema wamesikia pia. Sasa je wataalamu wa hali ya hewa na matetemeko, kuna kitu kama hicho kimetokea leo?
 
kwel ila tuliombee lisifike kaliakoo mana yale magorofa yataondoka yote chini mana mh! Kaz kwel kwel
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom