Tendwa sasa atishia kukifuta CHADEMA

Vipo vyama mbadala kibao ,nia na madhumuni ni kiondoa CCM na uhuni wake madarakani ,baadae tukimaliza kuiondoa tutagawana mbao na kuweka misingi mizuri tu ya kuendesha siasa zetu. Na vyama vilivyofutwa vitaruhusiwa kurudi ,Tendwa tutamfilisi kila kitu hata kama ana miliki baiskeli au paka.Kushinda azimio la Arusha.

hivi systems za JF zinaruhusu members tofauti tofauti kutumia ID moja?
 
Nchi hii ya ajabu.

CHADEMA wameanzisha vigilantes purpotedly kulinda usalama -Red Brigade- police wamevipiga marufuku kwa sababu haviko kisheria.

Wengine tukafikiri Polisi ndio watakaochukua jukumu la kulinda raia katika mikutano.

Kumbe Polisi ndio wanakuwa wauaji.

Halafu polisi wakiua raia, CHADEMA inalaumiwa tena?

Something is not adding up here!
 
Mkuu Molemo vipi wale wachili wa Arumeru bado hawajamuua Lema kama walivyomuahidi huyu anayejiita Mlezi wa Vyama( Tendwa)

Tangu CDM ishinde Arumeru alifunga domo lake kabisa.Nasikia alikimbia Arumeru siku ile ya uchaguzi alipopata fununu tu CDM wameshinda.Inasemekana alipanda kwenye gari la kiongozi mmoja wa kampeni wa CCM na kukimbilia Dar usiku.
 
We Tendwa jaribu uone kama nchi itakalika badala ya kulaani policcm we unaimaind cdm au ndio umetumwa kama wenzio policcm

Mkuu tatizo nchi ina viongozi vilaza wa kuambiwa kila siku hapo kasha danganywa tayari na yeye kaenda kwenye tv kuropoka bila kujua nini kinaendelea....

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Msajili wa vyama vya siasa nchini John Tendwa amesema sasa amechoka kusikia mauaji kwenye mikutano ya kisiasa ya CDM na atatumia rungu lake kufutia usajili chama chochote kitakachoshindwa kutunza amani ya nchi.Tendwa amewaambia waandishi wa habari hatishiki na chama chochote kuwa na wabunge kwani sheria inamruhusu kufuta chama hata kama kina wabunge 100.

Katika hali ya kushangaza Tendwa ameshauri vyama visubiri nyajati za uchaguzi ndipo vifanye mikutano ya kisiasa.Hata hivyo amekiri sheria inaruhusu vyama kufanya mikutano na maandamano wakati wowote.

Source:Habari Radio Tumaini.

Tendwa hafurukuti mbele ya mkewe na anatawaliwa nyumbani kwa hiyo hawezi kuwa na akili zilizonyoka awapo ofisini.
 
Kama wamefikia kutumia mbinu hii ili kuuwa upinzani kipindi hiki, basi wamechelewa mno. Haiingii akilini mtu kama Tendwa kutoa sababu ya kukifuta chama wakati waliotenda uovu huo wazi ni Polisi. Je anayo majibu ya TUME ya Iringa tayari. Tulimsikia na wazee wake wa Kishili kule Arusha, watu wakamuonya hakusikia. Sasa ndiyo wanataka kuanzisha vuguvugu kubwa zaidi lisiloweza kuzuilika na linaloweza kuleta positive effect kabla ya 2015.
 
Tendwa anataka kutufanya sisi watoto.Mfumo wa vyama vingi si uamuzi wetu
bali ni shinikizo toka mataifa ya ulaya.Ndio maana kila uchaguzi mkuu wanatuma
waangalizi toka huko kwao.Hivi kama kufuta chama ni rahisi hivyo ni kwanini
Museveni asifute chama kinachoongozwa na Dr. Besyige?
 
Mungu amewaumbua.Kilichoikoa CDM ni zile picha zilizopigwa na waandishi kuonyesha yule polisi katili alivyofumua utumbo wa mwandishi yule masikini.Kwani siku ile tayari Chagonja alishasema CDM ndiyo walirusha kitu kizito kumuua yule mwandishi,kumbe walishajipanga kupiga propaganda na tayari Tendwa alishaandaliwa kuongea ujinga kama wa leo ili kuhalalisha kufuta CDM.Mungu ni mwema waandishi wamemuumbua Tendwa na wenzie.
Ndugu yangu Mungu siku zote yuko upande wa haki ndiyo maana aliweka duniani vitu mbalimbali na kuwapa wanadamu maarifa ya kutengeneza vifaa vya kiteknolojia kama vile kamera ili ukweli ulivyodhihiri katika mauaji ya makusudi kabisa ya ndugu yetu Mwangosi. Na kama polisi hasa IGP angekuwa na akili nzuri kuanzia sasa angeamua kuendeshwa na sheria, tena yeye ni mwanasheria kitaaluma. Vinginevyo kama wanasiasa wataendelea kumwingilia awakatalie na kuanza kuzungumza na vyombo vya habari kuhusu kukataa kuingiliwa na wanasiasa, wakiendelea atishie kujiuzulu ili kulinda heshima yake kama msomi. Ona bwana mdogo Nchimbi alivyomwaibisha leo kwa kujifanya anamfundisha kazi. Kama anaweza naye amjibu kupitia vyombo vya habari.
 
Ndo wameua ili wafanye maamuzi haya??
Tendwa usitufanye watoto wadogo.
Hii sio taznania ya mwaka 47.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Kwani chadema ni nini!? Jina, bendera, ofisi au ni watu!? Anataka "kufuta" watu!? Au anataka kufuta yaliyo mioyoni mwa watu!? Au mimi ndio sijaelewa!?
Huyu jamaa anakurupuka kama Mlevi wa wanzuki Mkuu hukumbuki ile single aliyokuja nayo Arumeru kuhusu Lema?
 
Mimi nilijua anatishia kulifuta jeshi la polisi maana ndio linaloua.!!
 
kiranja tengwa mbona mambo YAKOWAZI kama unaweza kufuta anza kuwafuta POLISI au huwezi basi kaa kimya wakufuta tutafuta wenyewe
 
Ndio tatizo mtu ukielimika alafu ukawa KUWADI wa mafisadi,elimu yako yote inapotea,unakua unatoa kauli za u.p.u.u.z.i mtupu,huyo Tenwa anayajua madhara ya kuifuta C.d.m?nadhani anaropoka kuwafuraisha anaowakudia!ajaribu aone kama hatofutika yeye kabisa,na hao anaowakuwadia watayapata majibu si kwa Watanzania tu bali hata kwa mataifa makubwa yanayopenda demokrasia!Tndwa awe anafikiria kwanza kabla ya kuropoka,mara washihiri mara vile,zee zima halioni hata aibu na haligundui kua linaaibisha mpaka mkewe na watoto
 
Msajili wa vyama vya siasa nchini John Tendwa amesema sasa amechoka kusikia mauaji kwenye mikutano ya kisiasa ya CDM na atatumia rungu lake kufutia usajili chama chochote kitakachoshindwa kutunza amani ya nchi.Tendwa amewaambia waandishi wa habari hatishiki na chama chochote kuwa na wabunge kwani sheria inamruhusu kufuta chama hata kama kina wabunge 100.

Katika hali ya kushangaza Tendwa ameshauri vyama visubiri nyajati za uchaguzi ndipo vifanye mikutano ya kisiasa.Hata hivyo amekiri sheria inaruhusu vyama kufanya mikutano na maandamano wakati wowote.

Source:Habari Radio Tumaini.


ANAWEZA KUFUTA CCM SASA KUTOKANA NA MATUMIZI MABAYA YA NGUVU ZA DOLA TULIYOWAKABIDHI?
 
Kufuta chadema ni vugumu kama kusema uingereza siyo nchi au kusema osama yuko hai hajafa
 
Kwani chadema ni nini!? Jina, bendera, ofisi au ni watu!? Anataka "kufuta" watu!? Au anataka kufuta yaliyo mioyoni mwa watu!? Au mimi ndio sijaelewa!?

Mkuu Filipe, huyu mzee wa kiswahili cha kiinglish anachoweza kufuta ni jina la chadema kwenye kitabu chake. Mimi nadhani kama anataka kujifurahisha ajaribu kufuta hilo jina kama atakuwa ameifuta nguvu ya umma!

Mimi nadhani wakifuta CHADEMA tutasajiri rasimi M4C kuwa ndo chadema mpya jina ambalo linawanyima usingizi mafisadi na wabunge wa magamba. Watakoma maana ndo limekaa poa!
 
Back
Top Bottom