Tendwa, Mkuchika watofautiana kuhusu waliotimuliwa udiwani AR

Hakuna haja ya kutukanana, matusi hayo kila mmoja anayafahamu na ana uwezo wa kutukana. Mkuchika hajatengua maamuzi ya CDM bali ameweka "pending" kutambua maamuzi hayo ili kupisha maamuzi "Mama" ya mahakama. yeye "mkuchika" ndio kiongozi mkuu katika Tamisemi, mwenye dhamana ktk wizara hiyo.ndio maana walimpelekea maamuzi ili ayatambue.sasa kama kuna "hitilafu" hapo unategemea atafanya nini kama sio kusubiri ili hitilafu hiyo iondolewe? Hatutajenga kwa kutukanana japo unaona kuwa tu mbalimbali na hatuwezi kuonana, ila si desturi nzuri.



Zia upo wrong, mkuchika alipata nakala ya kuenguliwa madiwani, na chama ndio mdhamini hivyo at present sio wanachama wa chadema na hivyo basi sio madiwani, je wasingeenda mahakamani? kakurupuka asubiri mahakama iamue jamani mbona tunaupeo mdogo wa kufikiri? ndio maana tunaingia kwenye mikataba mibovu shauri ya kutothink!
 
Kutofautiana katika misimamo ni jambo la kawaida tu hasa unapoendesha au unapowajibika kwa maamuzi makubwa.
kwahiyo hakuna tena kufuata katiba ya nchi wala misingi iliyowekwa na serikali. Tunafuata misimamo binafsi. haya! Endeleeni bana!
 
Tendwa, Mkuchika awajatofautiana kuhusu swala zima la madiwani wa Arusha. Bali Mkuchika ametumia madaraka yake vibaya kwa kukiuka
sheria, kuingilia na kuvunja katiba ya Tanzania. Tosha hapo kwa waziri mwenye dhamana muhusika ameshafanya kosa kubwa na stahiki yake
ni kujiuzulu wadhifa wake mara moja na kupisha mtu mwenye upeo zaidi aongoze, inaonyesha wazi kabisa kama huyo si mtendaji kazi bali ni
mchapa usingizi ofisini aelewi kama yupo pale kwa kuwaongoza wananchi na sio kuwakandamiza wananchi. Katiba ya Nchi,sheria ya uchaguzi
pamoja na vipengele vyote hivyo vipo katika vitabu kimaandishi kabla ya maamuzi inahitajika usome na uelewe, na kila kitu kiko wazi kama
chama kikishamvua uanachama mbunge au diwani ni kikomo cha Uongozi. Alichokifanya Mkuchika ni Abuse of competence.
kwa kukiuka katiba ya Tanzania. Na ndio maana Tendwa anamshangaa. Na hao madiwani wa Arusha ni walafi wa mali za wananchi, ina maana wapo
usingizini awaelewi kama kuendelea kuchukuwa posho ni kosa la jinai, hao hawafai kurudishiwa uanachama waelekee huko kwenye chama cha
magamba, majungu na ufisadi.
 
<br />
<br />
Sidhani kama kuna tatizo kwasababu wawili hao hawawajibiki kwa boss mmoja.

kweli? si TENDWA anateuliwa na raisi na waziri si anateuliwa na rais? wote wanawajibika kwa rais, na wanatumwa na rais sema tu kuna mmoja leo kaamua kusimamia ukweli
 
Viongozi wa hii nchi kama wamepotezwa mwelekeo vile! Jamani, hakuna semina elekezi ili hawa jamaa wafundwe kusimamia misingi ya katiba kwa maslahi ya nchi!
 
Mkuchika hajui alitendalo , na hii inaonyesha jinsi ambavyo serikali hii imechanganyikiwa kiasi kikubwa sana .

Sijui kama alipata ushauri wa mwanasheria mkuu wa serikali wakati anafanya uamuzi huo kwani angeweza kushauriwa vinginevyo , na kwa taarifa yenu ni kuwa hakuna kesi ambayo imefunguliwa kwa ajili ya watu kuomba kurejeshewa uanachama wao huko Arusha bali ni kesi ya kutaka kuzuia mikutano ya hadhara ya CDM sasa Mkuchika sijui katoa wapi anachokisema leo.
 
maamuzi ya bwana mkuchika nadhani (mtizamo wangu) yamekaa kimaslahi ya chama zaidi....
 
Msajili wa vyama vya siasa ndiye mwenye mamlaka ya kutambua au kutotambua wabunge na Madiwani, sio kazi ya Mkuchika. Na huu ni uvunjaji mkubwa wa sheria na demokrasia kwa Mkuchika ambaye ni kutochaka chama tawala kusimama na kuzungumza kwa niaba ya chama chake kutambua madiwani wasiokuwa na chama. Na hakuna mahakama duniani inayoweza kuwalazimisha Chadema kuwarudisha uanachama madiwani hao - Hakuna.

Na ndio maana siku zote tumesema chombo hiki cha msajili wa vyama vya siasa kinatakiwa kuwa huru na ajabu inashangaza sana kuona hadi leo hii hakijafanya utaratibu wa uchaguzi ktk majimbo husika ila wepesi kurudia uchaguzi wa Igunga baada ya Rostam kujiuzulu. Mbona huko hatusikii mahakama ikitoa hukumu yake kutengua kujiuzulu kwa Rostam, na Je, Chadema, CUF na TLP wakisema hawatambui kujiuzulu kwa Rostam kwa sababu alichaguliwa na wananchi, chama hakina mamlaka ya kumlazimisha kujiuzulu - tutafika kweli?
 
<br />
<br />
Sidhani kama kuna tatizo kwasababu wawili hao hawawajibiki kwa boss mmoja.

Kumbe hata hujui nini kinaendelea ktk nchi yako na unajitia eti wewe ndio mtetezi wa CCM ? Mkuchika anafanya kazi chini ya ofisi ya waziri mkuu na Tendwa ni kuwa yuko huko huko chini ya waziri Mkuu kwani ofisi yake ipo chini ya PM.

Sasa ukajifunze kwanza kabla ya kuja humu na kusema na pia kumbuka Tendwa ni msajili wa vyama na kwa mujibu wa sheria ni lazima awe na sifa ya kuwa Jaji sasa Mkuchika sijui hata alisomea kitu gani , na huyu msajili ndio huwa anasimamia sheria za vyama vya siasa kila siku ndio wajibu wake .

Barua ya Mkuchika inachekesha sana anasema eti kama kuna kesi mahakamani basi lazima kesi hiyo inahusiana na kurejeshewa uanachama kitu ambacho hakipo na hakuna kesi kama hiyo./
 
Kwa wale wanaokumbuka juu ya kesi ya Erasto Tumbo na John Cheyo ambapo Cheyo alimfukuza uanachama kwenye ITV na hivyo kupoteza ubunge wake na mpaka leo kuna kesi mahakama kuu ya Tumbo dhidi ya Cheyo kuwa alifukuzwa bila utaratibu lakini kesi inaendelea na Tumbo hajawahi kulipwa mafao yake ya Ubunge kutokana na hoja kuwa alifukuzwa uanachama sasa Mkuchika sijui anaishi wapi ama haya yote hayajui?
 
Inasikitisha kusikia kuwa Meya anasema yeye anafuata magizo ya juu yake ina maana atendi kwa kufuata sheria ila anafuata chama chake kina sema nini tu basi. nashindwa kumuelewa na nitashindwa kumuelewa daima meya huyu wa arusha
 
Suala hili lina utata, lipo mahakamani. Mkuchika yupo sahihi, hawezi kutambua kuvuliwa kwao wakati suala lipo katika vyombo vya sheria. hata kwa mfano suala la kujivua kwa Rostam kama lingekuwepo mahakamani.bunge lisingeweza kutambua kutokuwepo kwa mbunge katika jimbo la igunga. hivyo kauli ya mkuchika ipo sahihi hadi pale mahakama itakopotoa maamuzi yake. &quot;Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni&quot; wale bado ni madiwani kama sheria inavyomtambua &quot;mhalifu&quot; kuwa hana
 
Baada ya upuuzi huu wa Mkuchika je ni hatua zipi za kinidhamu na kisheria anaweza na/au anapaswa kuchukuliwa huyu jamaa???
 
Hivi kuna kesi Arusha ya waliokuwa Madiwani kutaka warudishiwe Uanachama wao?
 
Wana JF,

Hivi Katiba na sheria ya Nchi inasema nini kuhusu uhalali wa Mkurugenzi wa Manispal?
Je kuwepo kwake ni kuwa juu ya Madiwani?
Mwajili wake ni Yupi Madiwani au Serikali nikiwa na maana madiwani wa Manispal hiyo husika si ndio wanayo nguvu ya kumwadabisha Mkurugeni kwani wao ndio wanmfanya mkurugenzi kuwa hapo?
Je madiwani wanayo haki kikatiba kumbinga Mkurugrnzi anae letwa na Serikali? Kwanini Mkurugenzi asiwe chaguliwe kwenye jopo fulani
 
Hivi kuna kesi Arusha ya waliokuwa Madiwani kutaka warudishiwe Uanachama wao?

Hapo hakuna kesi mkuu tokea lini mahakama ikaingilia uhuru wa Chama fulani kukiambia no huyo ni mwanachama wenu tuuuu na kuwalazimisha kuwa anahaki ya kubaki kuwa mwanachma huku chama kimeisha kutema inakuja hiyo akilini haiiniitaji mi/au wewe kuwa na LLB kulitambua hilo
 


Hapo hakuna kesi mkuu tokea lini mahakama ikaingilia uhuru wa Chama fulani kukiambia no huyo ni mwanachama wenu tuuuu na kuwalazimisha kuwa anahaki ya kubaki kuwa mwanachma huku chama kimeisha kutema inakuja hiyo akilini haiiniitaji mi/au wewe kuwa na LLB kulitambua hilo
Ofcourse mahakama inaweza kuingilia chama kinawafukuza vipi watendaji waliochaguliwa kwa dhamana ya wananchi. Chama inakuwa mpito kwa hawa wachaguliwa na chama hakiwezi kufukuza viongozi wakati wapo bado kwenye kipindi chao cha kuongoza. Chadema ingesubiri tu 2015 iwavue uongozi kwa kuto wasimisha lakini ni kuwavunjia haki watu waliowachagua as reps.

Unless wamefanya uahini wa kitaifa lakni vinginevyo ni uoneaji na ukiukwaji wa demokrasia warudi makazini tu.
 


Hapo hakuna kesi mkuu tokea lini mahakama ikaingilia uhuru wa Chama fulani kukiambia no huyo ni mwanachama wenu tuuuu na kuwalazimisha kuwa anahaki ya kubaki kuwa mwanachma huku chama kimeisha kutema inakuja hiyo akilini haiiniitaji mi/au wewe kuwa na LLB kulitambua hilo

Ndiyo maana nikauliza kuna Kesi Mahakamani ya wale waliokuwa Madiwani wa Arusha kuomba/kutaka warudishiwe uanachama? Tuanzie hapo!
 
Ofcourse mahakama inaweza kuingilia chama kinawafukuza vipi watendaji waliochaguliwa kwa dhamana ya wananchi. Chama inakuwa mpito kwa hawa wachaguliwa na chama hakiwezi kufukuza viongozi wakati wapo bado kwenye kipindi chao cha kuongoza. Chadema ingesubiri tu 2015 iwavue uongozi kwa kuto wasimisha lakini ni kuwavunjia haki watu waliowachagua as reps.

Unless wamefanya uahini wa kitaifa lakni vinginevyo ni uoneaji na ukiukwaji wa demokrasia warudi makazini tu.

Sijajua uwezo wa akili yako Mkuu eric cartman kuna wakati inatupasa kusoma tu na kubonyeza like pasi kuchangia
 
Back
Top Bottom