Tendwa, Mkuchika watofautiana kuhusu waliotimuliwa udiwani AR

Mnasahau tu. Kuna Mbunge/Wabunge wa CUF aliwahi/waliwahi kutimuliwa ndani ya chama chao lakini Spika wa wakati huo akaendelea kuwatambua kama Wabunge hadi walipomaliza kipindi chao.
 
hawa jamaa na chama chao hawawezi kukaa wakelewana tena maana ufalme walioamua kuujenga hauna nia njema na haushabiiani na viapo walivyokula, tutaona zaidi ya hapa! Hii inatokea katika kipindi kisichozidi wiki woja ambapo nafasi ya juu kabisa ...rais na katibu wake kutoa maamuzi yanayopingana!
 
Viongozi wa Tanzania bwana!!. Kila mmoja anaamua alitakalo. Tutafika kwel!
 
Kutofautiana katika misimamo ni jambo la kawaida tu hasa unapoendesha au unapowajibika kwa maamuzi makubwa.

Kama kawaida yako mawazo mgando, pumba kabisa. Hapa sio shauri la kutofautiana kimawazo bali ni suala la sheria inasemaje????
 
Kutofautiana katika misimamo ni jambo la kawaida tu hasa unapoendesha au unapowajibika kwa maamuzi makubwa.
Inapokuwa misimamo isiyohusu kanuni za kisheria, hapo sawa. Lakini katika hili, kinachoangalia ni sheria inasemaje. Sheria inasema mtu akifukuzwa uanachama na chama chake, hawezi kuendelea na wadhifa wake ambao alichaguliwa kwa kofia ya chama, hata awe rais. Alichokifanya Mkuchika ni kutofautiana na sheria hii
 
Suala hili lina utata, lipo mahakamani. Mkuchika yupo sahihi, hawezi kutambua kuvuliwa kwao wakati suala lipo katika vyombo vya sheria. hata kwa mfano suala la kujivua kwa Rostam kama lingekuwepo mahakamani.bunge lisingeweza kutambua kutokuwepo kwa mbunge katika jimbo la igunga. hivyo kauli ya mkuchika ipo sahihi hadi pale mahakama itakopotoa maamuzi yake. "Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni" wale bado ni madiwani kama sheria inavyomtambua "mhalifu" kuwa hana hatia hadi pale sheria itakapomtia hatiani. Tenda ndiye aliyekurupuka.

Kwa hiyo tunakubaliana kwamba kati ya wawili hao kuna mtu alikurupuka!! Duh mbona mikurupuko inazidi kulikoniiiiii?
 
Kutofautiana katika misimamo ni jambo la kawaida tu hasa unapoendesha au unapowajibika kwa maamuzi makubwa.

Mwita nenda kisheria zaidi usiende kiubishi ubishi maana hapo kinachogomba ni sheria
Na waziri unasimamia sheria unapotoa maamuzi yako
Inakuwaje mtu ambaye anapaswa aijue sheria na then anatoa maamuzi ya kiajabu kupingana na sheria na Katiba inavyosema
 
hahaaaa, another proof there is no government....and that law is for kapukuz and not wakubwa!
 
Kutofautiana katika misimamo ni jambo la kawaida tu hasa unapoendesha au unapowajibika kwa maamuzi makubwa.
haya ni maamzi makwa kwa nani kwa CCM, Serikali, Mahakama, CHADEMA au madiwani walio temwa....
 
Inapokuwa misimamo isiyohusu kanuni za kisheria, hapo sawa. Lakini katika hili, kinachoangalia ni sheria inasemaje. Sheria inasema mtu akifukuzwa uanachama na chama chake, hawezi kuendelea na wadhifa wake ambao alichaguliwa kwa kofia ya chama, hata awe rais. Alichokifanya Mkuchika ni kutofautiana na sheria hii
MN,
KATIBA ya JMT inamtambua Rais wa Zanzibar na Waziri Kiongozi wake hadi leo! Lakini Maalim Seif ana mabenzi meusi matatu na ulinzi.
 
Suala hili lina utata, lipo mahakamani. Mkuchika yupo sahihi, hawezi kutambua kuvuliwa kwao wakati suala lipo katika vyombo vya sheria. hata kwa mfano suala la kujivua kwa Rostam kama lingekuwepo mahakamani.bunge lisingeweza kutambua kutokuwepo kwa mbunge katika jimbo la igunga. hivyo kauli ya mkuchika ipo sahihi hadi pale mahakama itakopotoa maamuzi yake. "Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni" wale bado ni madiwani kama sheria inavyomtambua "mhalifu" kuwa hana hatia hadi pale sheria itakapomtia hatiani. Tenda ndiye aliyekurupuka.
yaani kama mahakama ingetoa tamko alilolitoa Mkuchika sijui kama kungekuwa na mabishano haya yote..tatizo kwanini mkuchika yeye atoe tamko hilo badala ya mahakama ni kwa masilahi ya nani huoni kafanya kazi ya mahakama...
 
ushawahi kuingia kwenye nyumba ambayo baba hajulikani, mama hajulikani na watoto vivyo ivyo? mashemeji, mawifi, mashangazi kila mtu ana sauti kwene nyumba hio hio moja?? sasa ndio bongo hii
 
Kutofautiana katika misimamo ni jambo la kawaida tu hasa unapoendesha au unapowajibika kwa maamuzi makubwa.

Kama ni kutofautiana kwa mitizamo binafsi nakubaliana na wewe 100%. Lakini linapokuja suala la maamuzi ya kisheria inashangaza watendaji kutofautiana kiasi hicho wakati wanaongozwa (au wanapaswa waongozwe) na sheria zilezile (ile ile).

Tatizo la watendaji wetu wanaweka sheria pembeni na kuingiza ushabiki wa kisiasa na hivyo kuwa na matokeo/maamuzi tofauti mahali pasipostahili. Laiti wote wangesimamia na kuongozwa kikamilifu na sheria madudu yanayoonekana serikalini na kwenye taasisi zake yasingekuwepo.
 
MN,
KATIBA ya JMT inamtambua Rais wa Zanzibar na Waziri Kiongozi wake hadi leo! Lakini Maalim Seif ana mabenzi meusi matatu na ulinzi.

Mbona wengi tu wanalindwa mkuu. Hata Mrema aliwahi kupewa benzi na ulinzi akiwa Naibu Waziri Mkuu cheo ambacho hakipo. Zanzibar wana nchi yao tuwaache wafanye yao.
 
Tendwa,Mkuchika nao watofautiana vikali

Nakala ya barua hiyo ambayo ilibeba kichwa cha habari kisemacho: "Kuvuliwa uanachama hivyo kukosa sifa ya kuwa diwani huku mwisho wa barua hiyo ikisema kuwa 'kutokana na na madiwani hao watano kufungua kesi na
kuiomba mahakama kuwarejesha uanachama wataendelea kuhudhuria vikao vyote vya baraza na kulipwa stahili yote hadi mahakama itakapotoa uamuzi'.

Hapo kwenye Red.
Naona huyu Mkuchika ameamua kuzipumzisha akili zake za kichwani na kuanza kutumia Masaburi. Kwa akili hata ya Chekechea, Mtu anayeomba kurudishiwa Uanachama maana yake ni moja tu kwamba kwa wakati huo hana huo uanachama, wangekuwa bado wanachama sasa wanachoiomba Mahakama iwarejeshee kitu gani! Na kama hawana Uanachama wa Chama chochote cha Siasa, wakati Udiwani ni kazi ya siasa, sasa anataka wawe madiwani kwa tiketi ya chama gani au wakiwa wanachama wa chama gani!

Hii ndio aina ya Viongozi tulionao.
 
Kutofautiana katika misimamo ni jambo la kawaida tu hasa unapoendesha au unapowajibika kwa maamuzi makubwa.

Hii inatokea kwa viongozi mambumbu wasiojua katiba na sheria, walioweka maslahi yao binafsi mbele, na watu vibaraka, wenye njaa na makuwadi kama ww.
 
hizi ndio dalili nzuri za ccm kufa kifo cha aibu...wanachofanya sasa hivi ni kupinga kila kitu cha chadema..sisi yetu macho ila katiba ya nchi isivunjwe...
 
Back
Top Bottom