Tendwa kumchukulia hatua Mtikila | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tendwa kumchukulia hatua Mtikila

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ochu, Sep 17, 2008.

 1. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #1
  Sep 17, 2008
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  na Edward Kinabo

  MSAJILI wa vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, anakusudia kukichukulia hatua Chama cha DP, iwapo itabainika madai aliyotoa Mwenyekiti wa chama hicho, Mchungaji Christopher Mtikila, kuhusu kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe, yalilenga kukichafua Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

  Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu kutoka mjini Dodoma, Tendwa alisema kama msajili na mlezi wa vyama vya siasa nchini, ana jukumu la kulinda kanuni za maadili ya vyama vya siasa ambazo haziruhusu siasa za kuchafuana baina ya vyama na vyama.

  Alisema, ofisi yake itapitia madai ya Mtikila na iwapo itabainika kuwa yalipata baraka za DP na yalikuwa na lengo la kuichafua au kuiathiri CHADEMA kisiasa, hatasita kuchukulia hatua zinazostahili.

  “Nimesoma kwenye vyombo vya habari kwamba Mtikila amewatuhumu Mbowe na Mengi kuwa walifadhili mpango wa mauaji ya Wangwe. Sasa Mengi ni mtu tu si chama cha siasa na Mbowe naye ni mtu, si chama cha siasa.

  “Sasa kama alituhumu watu, basi ni jukumu la watu hao wanaodai kukashifiwa kwenda kumshitaki maana ni hivi karibuni Mtikila huyu huyu alifutiwa kesi ya kumkashifu rais aliyepita, Mkapa. Kwa hiyo kama wamekashifiwa nao wanaweza kwenda kumshitaki.

  “Lakini kama shutuma za Mtikila ziliigusa CHADEMA kama chama, hapo ofisi yangu itachukua hatua zinazostahili dhidi ya DP. Tutalitazama suala hili na kuchukua hatua,” alisema.

  Wiki iliyopita, Mchungaji Mtikila, alielezea kile alichokiita mpango kamili wa kumuua Wangwe, akidai kuwa aliuawa na watu kutoka Kenya ambao walikodiwa kwa kazi hiyo.

  Katika madai yake hayo, alimtaja Mbowe kuwa mmoja wa watu waliofadhili mpango huo na mfanyabiashara, Reginald Mengi, ambaye hata hivyo hajazungumzia lolote kuhusu madai hayo.

  Juzi akihutubia mkutano kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Mbugani jijini Mwanza, katika maadhimisho ya mwaka mmoja tangu CHADEMA itangaze orodha ya mafisadi 11, Mbowe alisema CCM inatumia wapinzani kutoka vyama visivyo makini, ili kukitumia kifo cha Wangwe kuendesha propaganda za kukidhohofisha chama chake.


  Source: Tanzania Daima
   
 2. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Sipati picha, kwani kuna uhusiano gani kati ya Mengi, Chadema, Wangwe na Mbowe?

  Nijuavyo mimi hata humu Jf huwa tukiita IPP green sasa hapa mbona sipati uhusiano? nisaidieni jama wenye kujua walau 'a little connections'.
   
 3. Lasthope

  Lasthope Senior Member

  #3
  Sep 17, 2008
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 149
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  siasa za bongo, yani zinachoosha mi nafikiri hakuna hata haja ya kupanga msitari mrefu siku nzima eti napiga kura ili kuwasaidia wezi wakaibe, ni mtazamo tu, hii bongo ustaarabu bado sana.
   
 4. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #4
  Sep 17, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  mimi nadhani mtikila ametumiwa na akina manji, rostam azizi, shubash patel. ukiangalia mtikila alivyosuka hili dili lake dhidi ya chadema lina harufu ya wahindi, ni hawa tu wanafikiri watanzania ni mabwege. mnakumbuka kuwa hata swala la gari ya wangwe kufungwa jiwe kwenye accelerator na ajali hiyo inavyoweza kutungwa iliwahi kuandikwa na gazeti la rostam azizi la mtanzania.

  mtikila yupo na hawa wahindi 100%

  ujumbe wangu kwa wenzetu wa jamii ya kiasia, wasitulazimishe kuanzisha vikundi vya kigaidi shidi yao, wawe makini hatutaweza daima kuvumilia uchochezi wao dhidi ya kaka zetu na dada zetu wauaane halafu wao wakimbilie kanada, tutawahi kabla hawajafanyikiwa
   
 5. deny_all

  deny_all JF-Expert Member

  #5
  Sep 17, 2008
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 428
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Inawezekana hapo ni ukabila unataka kutumika kuwa wachaga lao moja.
   
 6. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #6
  Sep 17, 2008
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,145
  Likes Received: 1,236
  Trophy Points: 280
  Huyu Rostam huyu we acha, anafikiri hatujui kuwa yeye ndiye kinara katika mauaji ya Wangwe ili kufifisha nguvu ya Chadema iliyoibuka ghafla. F..........k
   
 7. Kamende

  Kamende JF-Expert Member

  #7
  Sep 17, 2008
  Joined: Mar 1, 2008
  Messages: 415
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Na bill sema!!!!!!
  Seemaaaa Usiogope sema!!!
  Na bill semaaa
  Seemaaa Usiogope sema!!!!

  Sisi............. hatuogopi ................ sema!!!!!!!!!!!!
   
 8. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #8
  Sep 17, 2008
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Ni kwa nini msimshauri aje kututembelea hapa nyumban Tarime?
   
 9. Mzee wa Gumzo

  Mzee wa Gumzo Senior Member

  #9
  Sep 17, 2008
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 197
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hatua ya msajili kuingilia kati ni ya kuungwa mkono.
  Jana niliandika kuwa siasa za DP kwa muda mrefu zimekuwa za gizani.Hata tuhuma zake zinaleta ukakasi na ipo haja kwa msajili kuiangalia DP.Kuna uwezekano kimesajiliwa kama chama cha siasa lakini kinatumiwa na watu wenye vijisenti vyao
   
 10. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #10
  Sep 18, 2008
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  CCM yashindwa kufungua kampeni zake Tarime


  WAKATI baadhi ya vyama vya upinzani vikiwa vimeshaanza kampeni za kuwania kiti cha ubunge cha jimbo la Tarime, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeshindwa kuzindua kampeni zake kwenye Kata ya Tarime Mjini kutokana na kifo cha kada wake, Gidioni Nyamhanga.

  Ingawa CCM ilishindwa kuzindua kampeni zake jana, mgogoro na tuhuma nzito wanazotupiana viongozi wa kambi ya upinzani, hasa kitendo cha Mchungaji Christopher Mtikila, kumshambulia mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na vigogo wengine, zinaonekana kukifagilia njia chama hicho tawala kuweza kutwaa jimbo hilo.

  CCM ambayo jana ilipanga kuzindua kampeni kwenye Kata ya Tarime Mjini, ilishindwa kutokana na kuungana na maelfu ya wakazi wa eneo hilo kushiriki mazishi ya kada huyo ambaye pia aliwahi kuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha.

  Nyamhanga, ambaye ni kada mwandamizi wa CCM, alifariki jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kutokana na ugonjwa wa saratani ya damu. Miongoni mwa waliojitokeza ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira.

  Kampeni za CCM kata ya Tarime mjini na ubunge zitaendelea hapo kesho, katika kata ya Pemba katika vijiji vya Nyabisaga, Pemba na Nyabitocho huku uzinduzi wa viongozi wa kitaifa ukitarajiwa kufanyika Septemba 21, ambao utafanywa na Makamu Mwenyekiti Pius Msekwa.

  Wakati kampeni hizo zikiendelea, tuhuma miongoni mwa viongozi wa upinzani na uamuzi wa kila chama kutaka kusimamisha mgombea, zinaonekana kuisafisha njia ya kutwaa kiti hicho ambacho kilishikiliwa Chadema, kabla ya kifo cha Marehemu Chacha Wangwe.

  Wakati Mbowe akiwa Mwanza juzi, pasipo kumtaja Mtikila, alishutumu baadhi ya vyama visivyo makini kutumiwa na CCM, Mtikila amejibu mapigo akisema kuwa kama Mbowe na wenzake wamekashifiwa wakaenda mahakamani.

  Kwa msisitizo, Mtikila jana alipoulizwa kwamba anatumiwa na CCM kuvuruga upinzani, alisema hiyo si hoja bali hoja ya msingi katika taarifa yake ya mwishoni mwa wiki ni kifo cha Wangwe, ambacho vigogo wa Chadema wakiongozwa na Mbowe wanahusika.

  Hata hivyo, Chadema imekwisha zitolea ufafanuzi tuhuma hizo kikisema kwamba hakuna kiongozi wake aliyehusika na kifo hicho, huku Katibu Mkuu Dk Wilbrod Slaa, akitaka iundwe tume ya uchunguzi.

  Akizungumzia onyo la Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, kwamba atakichukulia hatua chama hicho iwapo kilitumika kuendesha siasa za kuchafuana, Mtikila alisema msajili huyo hana uwezo huo.

  Tendwa alinukuliwa akionya kwamba, atapitia taarifa ya Mtikila kuona kama DP ilihusika kukichafua Chadema na pia akahoji kutuhumiwa watu.


  Mvutano huo umeifanya Chadema kushutumu vyama vingine kwamba, vinatumiwa na CCM kukihujumu huku vyama vingine navyo wakiwemo wanasiasa kama Mtikila, wakitoa tuhuma nzito kwa Chadema.
   
 11. r

  rpg JF-Expert Member

  #11
  Sep 18, 2008
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 3,516
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Cha msingi ni sheria kuchukua mkondo wake. Mtikira anatakiwa awasilishe ushahidi wake polisi kama DPP alivyosema ili tuweze kujua ukweli. Hofu yangu ni kama Mtikila atakuwa lake moja na CCM, na tujuacyo vyombo vya dola havina meno katika kukabiliana na wababe wa CCM, basi tusitegemee jipya. Naamini majibu ya sakata la kashfa alizotoa mtikila yatapatikana (hata kama ni ya kweli au la) baada ya uchaguzui mdogo wa Tarime. Mtikila ataendelea kuwa huru, kashfa itaachwa ikieleaelea kwa lengo la kuidhoofisha chadema katika kinyang'anyiro cha uchaguzi huo mdogo. CCM ni wataalam wa kubuy time ili either issues zao zifanikiwe ama kuzolotesha jambo fulani lililo hot katika jamii.
  Tusubirini tuyaone!
   
 12. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #12
  Dec 12, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Hivi tendwa alishamchukulia hatua huyu baba?
   
 13. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #13
  Dec 14, 2009
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  hakuna chochote....Tendwa mzee wa maneno bila vitendo
   
 14. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #14
  Dec 14, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Haya ni maandalizi ya CCM kukishughulikia chama cha CUF kwa kauli aliyotoa Lipumba kuwa "CCM chama cha wauza madawa ya kulevya".

  Sasa kwa kuwa wameguswa wameona waanzie mbali kidogo ili kupunguza malalamiko ya kuipendelea CCM. Tendwa alikuwa wapi wakati wa Uchaguzi mwaka jana?, kwa nini anasubiri kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu ambapo CCM imeanza kufunuliwa mabaya ya baadhi ya watendaji wake ndiyo aichukulie hatua DP?.

  Kwa mtu yeyote mwenye kuona mbali, atagundua kuwa Tendwa anatumiwa na kina Makamba na genge lake ili kuvihujumu vyama katika kipindi hiki. Kama CHADEMA ilichafuliwa na DP ilikuwa na haki ya kuenda mahakamani kuomba kusafishwa na si Tendwa, hayamuhusu!.
   
 15. K

  Kabonde JF-Expert Member

  #15
  Dec 14, 2009
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  MTM vipi unataka Mtikila achuliwe hatua gani kwani kakosa nini.Kusema CHADEMA walihusika na mauaji ya Chacha Wangwe ni kosa wakati inajulikana wazi viongozi wote wa juu wa NGO ohoo samahani CHADEMA walihusika moja kwa moja au indirect na kifo cha mpiganaji wetu Chacha Z wangwe.
   
 16. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #16
  Dec 14, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Watanzania tunapendwa na Mungu bado yupo nasi. Can you imagine mtu kama Mtikila na Mrema wangechukua nchi hii kama viongozi wakuu tungekuwa wapi? Mtikila ambaye miaka ya 1980 alitikisa nchi na sera zake za "saa ya ukombozi ni sasa" na kuwatisha "ma*********" ndie huyu huyu anayefanya umbea? Mtikila ambaye amefanya mengi kortini kwa kuiedesha serikali puta puta na kushinda kesi muhimu (landmark) ndie huyu alipewa na vijisenti na ku-sign IOU mbele ya Rostam? Farisayo mkubwa!
   
 17. SHUPAZA

  SHUPAZA JF-Expert Member

  #17
  Dec 14, 2009
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 548
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  sawa sawa mwikimbi hizi fitina uko sahihi bongo sanaa tu
   
Loading...