SHIEKA
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 8,240
- 4,270
Hujambo afrodenz? Najisikia raha kukuona maana ulipotea kwa muda. The Finest hajambo?We unafanyaga na nguo ?
Last edited by a moderator:
Hujambo afrodenz? Najisikia raha kukuona maana ulipotea kwa muda. The Finest hajambo?We unafanyaga na nguo ?
1. Ndo mnavua nguo
2. Ndo mana mnazima taa
3. Ndo mana hamsimulii watu jinsi mnavyolifanya
nawakilisha
Umetisha kiongozi.....moja wakiitwa majina ya heshima mrs, wife, mke au mama fulan[/B]i!.
Yote kwa yote, ni tendo hilo hilo!.
Pasco
1. Ndo mnavua nguo
2. Ndo mana mnazima taa
3. Ndo mana hamsimulii watu jinsi mnavyolifanya
nawakilisha
Hoja zako are NOT ENOUGH..!!1. Ndo mnavua nguo
2. Ndo mana mnazima taa
3. Ndo mana hamsimulii watu jinsi mnavyolifanya
nawakilisha
Kweli mkuu, sijui hawaogopi kumeza na miba..!! Raha ya chakula ule unakiona bwana..Loh unakosa mengi unazima taa?
te he he he! kwi kwi kwi! badili forum peleka kwenye vichekesho!1. Ndo mnavua nguo
2. Ndo mana mnazima taa
3. Ndo mana hamsimulii watu jinsi mnavyolifanya
nawakilisha
Wenzio tunaenjoy wewe unalalamika...
Kwani namba 2 ni lazima kufanya usiku? Mchana unazima nini?
Mkuu Mazindu Msambule,Mkuu, Pasco, umepotea sana kule kwenye jukwa la pasua kichwa, i mean jukwa la siasa, kumbe bado upo? Anyway, michango yako hiyo uliotoa ya kwenye Biblia napingana na wewe kabisa, si kweli kwamba Shetani ndiye mbunifu wa tendo la ndoa, shetani amelifanya lifanyike nje ya ndoa na hiyo ndio dhambi! Hiyo dhambi ya asili unayoisema nayo, mh, namashaka makubwa sana na ukweli wa hilo, Bikira Mariamu? Hivi unadhani yule mama alifariki akiwa bado bikira? Kwa taarifa yako, Yusufu alikua aki enjoy naye kama kawaida na hata alizaa watoto wengine wa kiume na wa kike! Hebu soma hapa Mathayo 1:21-25, inasema hivi, "....Naye Yusufu alipoamka katika usingizi, alifanya kama malaika wa Bwana alivyomwagiza; akamchukua mkewe;asimjue kamwe hata alipomzaa mwanawe; akamwita jina lake Yesu". Hapo nilipo Bold, hilo neno maanake, baada ya kumzaa Yesu Yusufu aliendelea kumjua mkewe kama wana ndoa wengine tu. Funguka kaka, usikariri.
Dini nyingi zina limit thinking ya waumini wake, sisi Wakristu limit yetu ya thinking ni uwepo wa Mungu, haturusiwi to think beyond, huyu Mungu, alitoka wapi, alianzaje na source yake ni nini, tunafundishwa tuu kuwa yeye ndiye mwanzo na mwisho, Alfa na Omega!.
Pia tunatajiwa uwepo wa shetani, hatuambiwi huyu shetani alianzaje na kama ni muharibifu hivi, kwa nini Mungu hamuangamizi, dunia ikapata amani!.
Sipendi kuwatisha wale ambao limit ya thinking yao end with God, ila naomba niwajulishe kuwa mwanzo wa Mungu, pia ndio mwanzo wa satan, na Lucifer, sio tuu ndiye alikuwa 2nd in comand baada ya God the father, he is still is!. Lucifer alipoasi, Mungu alimfukuza ila hana uwezo wa kumuangamiza!. Mungu Baba anauwezo mkubwa kuliko shetani, ila shetani nae anaowezo wa pili chini ya Mungu. Uwezo pekee wa Mungu ambao shetani hana ni Kuumba, na kutoa uhai!. Mengine yote ambayo Mungu anayaweza na shetani pia anayaweza. Hivyo kuna hawa wahubiri kibao wanafanya miujiza kwa jina la Mungu, lakini aliyewapa uwezo huo wa kufanya miujiza hiyo sio Mungu ni shetani!.
Kabla Mungu hajamuumba Adam, baada ya uasi wa shetani, Mungu akashauriana na NENO, malaika mkuu Mikaeli, na Gabrieli, tuumbe kiumbe kitakacho tutii, ndipo akamuumba Adam!. Mara baada ya Mungu kumumba Adam, kweli Adam alikuwa mtii, shetani akamdhihaki Mungu, kuwa ataupimaje utii wa Adam kama hana temptations, akamsisitiza ili kuupima utii wa kweli, Mungu amruhusu shetani amtempt huyo Adam, akivishinda vishawishi ndipo Mungu atathibitisha kweli yeye Mungu ndiye zaidi!. Shetani akasuggest the type ya temptation!.
Mungu alipomuumba Eva, pia akaviweka vile viungo vya temptation kama shetani alivyoshauri ni Mungu akawapa maonyo Adam na Eva kuhusu matumizi ya viungo hivyo ambavyo kwenye Biblia vimeitwa "tunda" na tendo limeitwa "mti wa mema na mabaya"!. Mema ni uzima, mabaya ni kifo!. Mungu akawaambia wakila tunda ya mti huo ni hakika watakufa!.
Ili kumlinda Adam na Eva na ushiwishi wa shetani, Mungu akaweka malaika wawili wenye upanga wa moto pale getini la bustanini, kumzuia shetani asipite. Shetani akajigeuza nyoka akapenya getini na kuingia bustanini!. Alipofika ndani, akajigeuza a very handsome man na kumfanyia timing Adam akamangemange mbali kidogo!.
Eva akashtuka kuona kuna kuna binadamu mwingine zaidi ya Adam!. Ndipo shetani akamuuliza Eva, hicho kiungo "tunda" ni cha nini?, Eva akamjibu, ni cha mema na mabaya Mungu katukataza tusivitumie!. Shetani akamwambia Eva, Mungu amewadanganya, hilo tunda la mti wa katikati, ndilo tunda tamu kuliko matunda yote (kweli au sii kweli?), na ukilila tunda hili, utapata raha kubwa kuliko raha zote duniani (kweli au sii kweli?) lakini zaidi ya yote hayo, shetani akamuhakikishia Eva, kuwa wakila tunda hilo, sio tuu watapata raha kubwa kuliko zote, bali pia watakuwa na uwezo wa Kimungu, wa kujiumbia viumbe wengine wengine wadogo! (procreation)!.
Kwa vile hayo mambo Eva hayajui, shetani akamuonjesha namna ya kumega tunda! kwa kumshughulikia na kweli, Eva alifurahi, alienjoy na kukiri hakuwahi kula tunda tamu kama lile!, na siku hiyo Eva ali mconceive Cain!. Baada ya Eva kuonjeshwa dose ya shetani, Adamu aliporudi, Eva akalazimisha anataka, japo Adamu alisita sana, Eva alimfanyia manjonjo kama alivyoelekezwa na shetani na kumuelekeza Adam jinsi ya kula "tunda", Adam akaingia line, tunda likamegwa, na baada ya kula wakaishia usingizini!.
Yote hayo yakifanyika Mungu anaona na hakuwa na uwezo wa kumzuia kwa sababu ita was a bet!. Ndipo Mungu akamuita Adam, na for the first time wakajistukia viongo hivyo ni vya nini, wakajiona uchi na kuanza kujificha!. Shetani alishinda, binadamu alimuasi Mungu and HE had no way out, bali kuwafukuza toka ndani bustani na kumpa Adam adhabu ya kula kwa jasho lake baada ya kukubali kudanganywa na mwanamke!, na Eva akapewa adhabu ya kubeba mimba miezi 9 na kuzaa kwa uchungu kufidia utamu wa starehe ya shetani!.
Tangu hapo ni kweli binadamu wakapata uwezo wa Kimungu kuzaa watoto, Mungu alikuwa na uwezo wa kuumba maumbile ya procreation kuwa kama "handshake" au hata "polination", vile viungo ni mpango wa shetani, na lile tendo ni la kishetani!.
Mtoto wa kwanza wa Eva , yule Cain ni product ya shetani ndio maana akazaliwa na tabia za baba yake, na mtoto wa Adam ni Abel. Na ndio maana sisi Wakatoliki tunaamini lile tendo la kumtengeneza mtoto ni dhambi as a result, mtoto ni product ya dhambi hivyo kuzaliwa na ndhambi ya asili (original sin) ya Adamu na Eva na ili kuiondoa kila mtoto hutakiwa kubatizwa ASAP akishazaliwa!. Watoto wate duniani, wanazaliwa na dhambi ya asili, isipokuwa Mtoto Yesu ambaye alizaliwa na Bikira Maria aliyekingiwa dhambi ya asili, hivyo Yesu sio product ya dhambi!.
Ndio maana makasisi wetu Katoliki hawaruhusiwi kuoa ili wasilifanye hilo tena, lakini kabla hawajapewa daraja ya ukasisi, kwanza ni lazima wafanyiwe vipimo kuwadhibitisha ni rijali hivyo kule kuvumilia tamaa za kimwili, ndio sadaka ya kweli ya upadirisho, na ni kiukweli kabisa mapadri wa Katoliki ni wasafi kabisa kama watakatifu na tendo hilo ambalo ni dhambi huwa hawalifanyi kabisa!. (tafadhalini sana kuhusu hili, nawaombeni msiwasingizie mapadiri wetu lolote)!.
Vivyo hivyo wale masista wa Katoliki nao wote ni kama B. Maria, sadaka yao ni kujizua kutofanya kosa kama la Eva, nao hufanyiwa vipimo kuwathibitisha wanatamani kufanya alichokifanya Eva ila wanajizuia!. Masista wetu wote ni wasafi kama malaika na hata mavazi yao huwa meupe kama theluji kuthibisha usafi wa mwili, moyo na roho!.
Pasco.
nawakilisha