Tenda ya billion 100 kupungua hadi billion 10 kuna usalama kweli??

tikatika

JF-Expert Member
May 6, 2011
2,330
4,115
Leo nimebahatika kumsikiliza mtukufu wetu kwa bahat mbaya tu, nikiwa nanyoa saloon moja hivi, yalikua ni marudio ya hotuba ya chuo cha mliman kufungua hostel zinazojengwa. kuna mengi kaongea ya kujadili. Ila tujadili mawili , kama sio moja. Katka maongezi ya mtukufu katka awamu hii hamna kutangaza tenda za serikali ni mwendo wa kupiga simu TBA na ujenzi unaendelea

Nanukuu niliongea na makampuni ya nje wakaniambia b100, nikapiga cm kwa boss TBA akasema b12 nikamshusha had b10. Sahz nimewapa wajenge magomeni , dodoma nitawapa, na nimewapa na kujenga kule kagera!!
Na kipind cha likizo nitawapa majengo mengine hapa hapa mmalizie...!!
Mwisho wa kunukuu.
Yaan awam hii makampun hakuna haja ya kuomba tenda kuna mwenzenu kachukua zote bila kushindanishwa!

Hoja yangu nzito ipo hapa kutoka b100 had kupungua had kufika b10. Maana kwa swala la kutofata sheria za nchi hususan za namna ya kupata tenda kwa makampuni ya ujenz hiyo ni kawaida kwa mtukufu wetu. Swali la kitaalam, ni hili!!

Inawezekana kupunguza bei ya ujenz kwa 90% ikabakia 10%? Kuna usalama hapa?? Naona mwanya wa hatari hapa kwa sehem zote mbili. 1; kukubali kujenga kwa 10% ya bei majengo hayatakua na ubora!!
Na kama hiyo ndio bei yake ya 10% basi miradi mingine yote tunaibiwa . Tunaomba mkuu atuweke sawa!! Kuna majengo kibao yanajengwa na wachina.
Na makampuni mengine nje ya TBA ya mtukufu.

Yaan nijuavyo kila tenda ina kiwango cha juu cha mwenye project na kiwango cha chini, mjenzi haitakiwi azid hayo makadilio wala asipungue chini ya makadilio ya kiwango cha chini cha project. kauli ya mkuu kufurahia kupunguziwa toka b100 had b10 ya ujenz wa mabweni. sijaelewa kuna namna nchi hiii inavyoendeshwaaaa...............!!

Kwa wale ambao hamjasikiliza angalieni wenyewe hapa!!
 
mzee anauzi sometime daaaah,tufanyeje sasa tufanyje zaid kunyamazq kimyaaa
 
Kazi ipo lkn mhe. Anapaswa ajiridhife kwenye ubora hayo majengo kutokana na hicho kiasi cha pesa huenda ikawa ni danganya toto labda jamaa wamevuta mpunga mwing sasa Anasem hvy ili hata makampuni mengine yashushe bei yaweze kuingia kwenye ushindani na TBA..
 
Bothways,rahisi bila viwango ni hasara na hatari kwa watu na mali zao,lakini ipo rahisi kwa gharama yake lakini imezingatia viwango vya ubora vya makazi ya vyuo.
Kawaida aghali uwa ni bora,lakini Tanzania imezoeleka kulipa gharama kubwa kwa kazi mbovu.
Jambo lingine ni mfumo wa ajira za ujenzi kwa mfano China hutumia wafungwa kujenga miradi mikubwa kwa ujira mdogo,labda Raisi anataka kutumia wafungwa au JKT kutimiza malengo,ikiwa njia mmoja wapo wa kubana matumizi.
 
mkuu ungetembelea shule ya hai day iliopo wilaya ya hai ushuhusie hio ghorofa jinsi ilivyo na mipasuko kwenye ukuta jengo hata halijazinduliwa UFA na gemsum zinakaribia kuisha zikibanduka
 
Ungejua watu wanavyoiba fedha kwenye hizo tenda za kujenga majengo ya serikali ungemuunga mkono rais.
Nyumba ya mtu binafsi ambayo ingejengwa kwa milioni 60 serikalini inajengwa kwa milioni 400.
Kuna fedha nyingi pia inapotea kabla hata tenda haijatolewa mfano kuna vikao vya kamati za tenda ambazo wajumbe hulipwa.
 
Huyu ndye zake. Ndyo maana tuna barabara nyingi za lami ni chini ya kiwango.
 
Mlipiga kelele sana kipindikile mlivyogundua serikali inanunua pen za Bic na Speedo kwa sh 2,000 wakati bei ya soko ni sh 200. Leo tena mnakuja na hoja mufris kana kwamba hamna kumbukumbu! Shaaaabashh
 
Kazi ipo lkn mhe. Anapaswa ajiridhife kwenye ubora hayo majengo kutokana na hicho kiasi cha pesa huenda ikawa ni danganya toto labda jamaa wamevuta mpunga mwing sasa Anasem hvy ili hata makampuni mengine yashushe bei yaweze kuingia kwenye ushindani na TBA..
Hivi kuna mtu ana mashaka na Magufuli linapokuja swala la viwango? Mmesahau jinsi alivyokua anagoma kukabidhiwa barabara (tena za misaada( zilizo chini ya viwango).
 
Sawa lakn ujenz una kanuni zake. Sijui kama unalijua hilo. Kwa mfano barabara kiwango cha lami kila km 1 inaweza kujengwa kwa b2. Huwez ukatenda kwa million 100 ukapewa. Tutajua hujui unacho kitafuta. Lakn pia km 1 huwez kuomba tenda kwa b100. Sijui kam nimeeleweka bosss
 
Hivi kwanini mnapenda kujivika upofu? Barabara ngapi aluikataa na ni barabara ngapi zina hali mbaya licha ya kutumia pesa nyingi? Bara bara ya Dar Mwanza kuanzia Singida kuendelea unaona hali yake?

Kiwango cha kivuko kilichonunuliwa kwa pesa nyingi nacho ni umakini wa viwango?

Naunga mkono jitihada za kubana matumizi zenye tija na sio mazingaombwe ya aina hii.
 
Sawa lakn ujenz una kanuni zake. Sijui kama unalijua hilo. Kwa mfano barabara kiwango cha lami kila km 1 inaweza kujengwa kwa b2. Huwez ukatenda kwa million 100 ukapewa. Tutajua hujui unacho kitafuta. Lakn pia km 1 huwez kuomba tenda kwa b100. Sijui kam nimeeleweka bosss

Kuna Mzee mwenye General tyre pale Msasani aliwaita wahandisi wawili akawaonyesha Kazi, mmoja akaleta M40, akamwambia wewe njaa inakusumbua utaniharibia Kazi, wa pili akaleta mapendekezo ya M120 akaambiwa aanze Kazi kesho yake.
 
Leo nimebahatika kumsikiliza mtukufu wetu kwa bahat mbaya tu, nikiwa nanyoa saloon moja hivi, yalikua ni marudio ya hotuba ya chuo cha mliman kufungua hostel zinazojengwa. kuna mengi kaongea ya kujadili. Ila tujadili mawili , kama sio moja. Katka maongezi ya mtukufu katka awamu hii hamna kutangaza tenda za serikali ni mwendo wa kupiga simu TBA na ujenzi unaendelea

Nanukuu niliongea na makampuni ya nje wakaniambia b100, nikapiga cm kwa boss TBA akasema b12 nikamshusha had b10. Sahz nimewapa wajenge magomeni , dodoma nitawapa, na nimewapa na kujenga kule kagera!!
Na kipind cha likizo nitawapa majengo mengine hapa hapa mmalizie...!!
Mwisho wa kunukuu.
Yaan awam hii makampun hakuna haja ya kuomba tenda kuna mwenzenu kachukua zote bila kushindanishwa!

Hoja yangu nzito ipo hapa kutoka b100 had kupungua had kufika b10. Maana kwa swala la kutofata sheria za nchi hususan za namna ya kupata tenda kwa makampuni ya ujenz hiyo ni kawaida kwa mtukufu wetu. Swali la kitaalam, ni hili!!

Inawezekana kupunguza bei ya ujenz kwa 90% ikabakia 10%? Kuna usalama hapa?? Naona mwanya wa hatari hapa kwa sehem zote mbili. 1; kukubali kujenga kwa 10% ya bei majengo hayatakua na ubora!!
Na kama hiyo ndio bei yake ya 10% basi miradi mingine yote tunaibiwa . Tunaomba mkuu atuweke sawa!! Kuna majengo kibao yanajengwa na wachina.
Na makampuni mengine nje ya TBA ya mtukufu.

Yaan nijuavyo kila tenda ina kiwango cha juu cha mwenye project na kiwango cha chini, mjenzi haitakiwi azid hayo makadilio wala asipungue chini ya makadilio ya kiwango cha chini cha project. kauli ya mkuu kufurahia kupunguziwa toka b100 had b10 ya ujenz wa mabweni. sijaelewa kuna namna nchi hiii inavyoendeshwaaaa...............!!
Kama kiwanja kimoja kilinunuliwa na NSSF shilingi milioni 800 kwa heka, inapaswa pia tujiulize viwango/ubora wa hivi viwanja vinavyouzwa milioni 2 hadi 10 kwa heka kama vinastahili kwa ujenzi wa nyumba za kuishi binaadamu.
 
Kazi ipo lkn mhe. Anapaswa ajiridhife kwenye ubora hayo majengo kutokana na hicho kiasi cha pesa huenda ikawa ni danganya toto labda jamaa wamevuta mpunga mwing sasa Anasem hvy ili hata makampuni mengine yashushe bei yaweze kuingia kwenye ushindani na TBA..
ninachokiona hapo raisi na watu wake wanataka kupiga hela, kwa nini hataki ushindani labda angepatikana mkandarasi wa chini ya b.10 kama wangeshindanishwa, raisi atainia kwenye kashfa muda si mrefu, raisi hawezi kukiuka sheria ya manunuzi akabaki salama. kumbuka kashfa ya richmond ilibuka katika mazingira kama haya. eti raisi annawapigia simu wakandarasi kuwauliza bei utaratibu wa wapi misijawahi ona
 
Back
Top Bottom