Temesa yakanusha kuhusu magugumaji kuzuia vivuko kufanya kazi Mwanza

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
TEMESA inapenda kukanusha uvumi unaoenea mitandaoni kupitia video pamoja na picha zikielezea kusimama kwa huduma za vivuko katika kivuko cha Kigongo Busisi mkoani Mwanza kutokana na kuwepo kwa magugu maji.

Tukio la magugu maji lilitokea siku ya tarehe 24 Desemba 2019 na magugu maji hayo yaliondolewa.

Shughuli za uvushaji abiria zinaendelea kama kawaida katika kivuko cha Kigongo Busisi. TEMESA inapenda kuwataarifu abiria wote waendelee kutumia huduma za kivuko hicho kwakua kipo salama.

Aidha TEMESA inawakumbusha abiria wote kuzingatia matangazo ya usalama yanayotolewa na mabaharia watumiapo vivuko.

Imetolewa na Kitengo cha Masoko Habari na Uhusiano kwa Umma
TEMESA
28/12/2019
 
Akili za kushikiwa, kama yalikuwepo siku tajwa, uvumi ni upi sasa..na hizi video clips ni za ziwa tanganyika au? Hizi medula za miaka hii.... issue ingekua hali ilitokea na kutatuliwa sio kuita uvumi
 
Mbona hatari, n
Ushindwe mwenyewe
Mbona hatari, inamaana hayo magugu maji yamekuwa msitu hivyo ndani ya siku moja? walikuwa hawayaoni? Maana nashangaa meli zote zimesimama na kila mtu anashangaa kana kwamba ni kitu kipya kwao.
 
1577615184300.png
 
Back
Top Bottom