mkadiriajimajenzi
JF-Expert Member
- Dec 31, 2015
- 549
- 608
Katika hali isiyo ya kawaida, majira haya ya saa tatu na nusu usiku huu kivuko cha magari na abiria cha MV Magogoni kimeshindwa kuanza safari kutoka upande wa Magogoni kwenda Kigamboni na kusababisha taharuki kubwa kwa abiria waliokua tayari wameshaingia kwa ajili ya kuanza safari.
Ikumbukwe kwamba vivuko hivi vibovu vya TEMESA vimekua vikilalalamikiwa sana na wasafiri kwa miaka mingi sasa bila mafanikio yoyote.
Nachukua fursa hii kuiomba Serikali itazame upya suala la uendeshaji wa vivuko hivi kwa maana TEMESA maji yameshawafika shingoni.