Teknolojia ya TBC hakika iko chini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Teknolojia ya TBC hakika iko chini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Stevemike, Dec 13, 2011.

 1. Stevemike

  Stevemike Senior Member

  #1
  Dec 13, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Jana nilitoa kero zangu dhidi ya TBC1 na leo wanaotazama taarifa ya habari ya saa 2.00 usiku mmejionea wenyewe. Taarifa inasomwa badala ya kuletewa picha inayohusiana na tukio, linakuja advertisement kisha wanajichanganya na kutulia kama dk 5 kabla ya kuendelea. What's the problem? Is it poor preparation or low technology?
   
 2. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #2
  Dec 13, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Chuki zako zisikufanye uache kutumia akili kufikiri. Hakuna uhusiano wa technology na hilo ulilolisema, hizo ni errors na hufanywa na stations zote hapa bongo kwa nyakati tofauti tofauti. Ndio maana tukaitwa nchi za ulimwengu wa tatu
   
 3. Tony Almeda

  Tony Almeda JF-Expert Member

  #3
  Dec 13, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Aaaaaagh! TBC wamezidi bhana! mpaka wanaboa.
   
 4. YEYE

  YEYE JF-Expert Member

  #4
  Dec 13, 2011
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 440
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Af mbaya zaidi ndo only Channel ya kibongo ambayo hk mikoani tunaipata kupitia Ma-Dish...
   
 5. libent

  libent JF-Expert Member

  #5
  Dec 13, 2011
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 385
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  kusema ukweli maana ya hiki chombo kuitwa 'shirika la utangazaji Tanzania' sielewi kwa sababu nijuavyo mimi shirika kama shirika la utangazaji linastik kwenye kutoa habari 24/7 lakini tbc taarifa ya habari inasomwa saa 7 mchana, 2 ya usiku na saa moja ya asubuhi hawaleti habari za matukio
   
 6. twatwatwa

  twatwatwa JF-Expert Member

  #6
  Dec 13, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 2,036
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Unachezea wachina wewe
   
 7. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #7
  Dec 13, 2011
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,816
  Likes Received: 1,155
  Trophy Points: 280
  duh yaani ukiangalia hiyo tv inashangaza hapo kwenye taarifa ya habari wanajichanganya sana inabidi wabadilike aisee
   
 8. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #8
  Dec 13, 2011
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Yote 9 wadau! 10 namna wanavyorudia hasa movie zao mf. Kama ile movie ya ki'bongo (sijui GALA-GALAUKA) wanairudia hadi inatia kichefuchefu! Nakwazwa na hilo kuliko la errores technology!
   
 9. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #9
  Dec 13, 2011
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Yote 9 wadau! 10 namna wanavyorudia hasa movie zao mf. Kama ile movie ya ki'bongo (sijui GALA-GALAUKA) wanairudia hadi inatia kichefuchefu! Nakwazwa na hilo kuliko la errores technology!
   
 10. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #10
  Dec 14, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Mkuu...kitu gani ambacho unaona ni chuki aisee? TBC tv ina quality mbaya sana hasa na ukizingatiwa mabilioni ya shilingi yaliowekwa pale....
   
 11. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #11
  Dec 14, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mkuu kila penye mkono wa ccm hapajakamilika hata kidogo 7bu wanaweka maslahi mbele kuliko huduma. Twamkumbuka Tido wetu aliyetolewa kwa fitina za wachache
   
 12. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #12
  Dec 14, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,531
  Trophy Points: 280
  Stevemike,
  Kwa kawaida mtu kama hujui kitu, unauliza na unapatiwa majibu na sio kutoa coinclusive statement!.

  thread yako, "Teknolojia ya TBC hakika iko chini.".
  Hii ni conclusive statement ikionyesha wewe unajua na ni hakika!. Baada ya hiyo conclusive sweeping statement yako, ndipo mbele ndani unakuja leta maswali "What's the problem? Is it poor preparation or low technology?"!.

  Kama badala ya kuanza na "Teknolojia ya TBC hakika iko chini.", ungeanza na "Jee Teknolojia ya TBC iko chini?".
  Kwa kusaidia tuu
  1. TBC ndio kituo cha kwanza hapa nchini, kuanza na digital recording kwa kutumia digital cameras za technolojia ya DV, mwaka 2000, wakati huo ikiitwa TVT, ikafuatiwa na Star TV mwaka 2002 ndipo vituo vingine vikafuatia. Wakati huo, vituo vingine vyote bado vilikuwa kwenye VHS na Super VHS.
  2. Japo TBC ndio ilikuwa ya kwanza kwa digital production, ililazimika kurusha matangazo yake kwa analoig transmiters kwa sababu miaka hiyo ya 2000, Tanzania hatukuwa na digital receivers zaidi ya kingamuzi cha DSTV
  3. Licha ya TBC kuwa na vifaa bora kabisa tangu wakati huo, ikiwa ndio kituo pekee kilichokuwa na portable edditing suites zaidi ya 6, bado hawakuweza kuandaa vipindi bora kwa sababu "maalum".
  4. Licha ya TBC kuanza kwa kutumia vifaa bora mwaka 2000, Star TV aliyefuatia mwaka 2002, ndiye aliyenunua vifaa vyenye ubora wa hali ya juu zaidi ya TBC.
  5. TBC ndio kituo cha kwanza kutumia tekniolojia ya HDV wakati vituo vingine vyote vikitumia DV
  6. Ni Star TV tena ndio inayoongoza kwa kamera zinazotumia teknolojia ya hali ya juu kabisa mpaka sasa kwani ndio kituo pekee hapa nchini Tanzania, ambacho kinatumia kamera za HDV zinazotumia kadi za SD wakati vituo vingine vyote, bado vinatumia HDV zinazotumia kanda (DV Tapes). Pia ampuni ya matangazo ya PPR ndio kampuni pekee ya production inayotumia HDV za SD kupeleka vipindi kwenye Televisheni mbalimbali.
  7. Wakati mwisho wa kutumia matangazo ya analojia duniani ni mwaka 2014, TBC ndicho kituo pekee cha Televisheni hapa nchini ambacho kimeshahamishia matangazo yake katika mfumo wa Digital toka mwaka 2010 kupitia ubia wake na Star Media ya Wachina, hivyo TBC ndio inayoongoza kwenye technology transfer. Mpaka sasa Tanzania tunayo makampuni maane manne yenye kibali cha kusambaza matangazo ya televisheni ya digital, yanaitwa Multplex Oparators il`a ni mawili tuu ambayo yameshaanza kazi ambayo ni Star Media na Agape.
  8. Baada ya TBC kutangaza kwa digital, Channel ten nayo imehamia na Clouds pia imejiunga na kingamuzi hicho cha Star Media, vikifuatiwa na Agape Televisheni na kingamuzi chake cha Ting. ITV na Star TV bado ziko kwenye analoijia ila nazo zimeungana na kuunda kampuni yao itakayorusha matangazo yao kwa digital hivi karibuni.
  9. Hata hivyo, pamoja na vifaa vya ubora wa hali ya juu vya TBC, na biggest pool ya watangazaji mahiri wa TBC, wenye vipaji lukuki waliotapakaa Tanzania nzima, bado TBC haijaweza ku perform na kudeliver according to expectaions za Watanzania hivyo kuonekana bado ni waborongaji.
  10. Kikampuni kidogo cha matangazo kwa jina la PPR, wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru, kwa kutumia teknolojiua ya kisasa, kimeandaa vipindi maalum vya "Miaka 50 ya Uhuru na PPR", na kuandaa vipindi 50 vya televisheni vya muda wa dakika 30, na kuvirusha katika televisheni 5 tofauti kwa muda wa siku kumi mfulilizo.
   
Loading...