Teh teh!nabii huyu kiboko

babukijana

JF-Expert Member
Jul 21, 2009
13,071
15,928

Bw.Tito Onesmo Machibya, mkazi wa Arusha maeneo ya Sombe, ametinga jijini Dar es Salaam na kujitangazia kuwa nabii aliyetumwa na mungu kuukomboa ulimwengu.

Machibya alinaswa na kamera yetu maeneo ya Posta Mpya jijini Dar es Salaam akijitangazia unabii wake ambapo mada yake kuu anasistiza kuwa; kunywa pombe si dhambi na kila mwanaume anatakiwa kuoa wanawake kuanzia saba.

Nabii huyo amekumbwa na upinzani mkali kutoka kwa baadhi ya wakazi wa jiji wanaomshutumu kuwa anafanya kufuru na kuupotosha ulimwengu.
Licha ya kupata upinzani mkali kutoka kwa wakazi wa jiji, Nabii huyo amewaambia wakazi hao kuwa bia ya Serengeti ndio kiburudisho muruuuwa… kinachompendeza Mungu na ni kinga ya mwili.

source:global publishers
 

Attachments

  • NABII.jpg
    NABII.jpg
    24.9 KB · Views: 82
Nilimwona Arusha akiwa na mada hiyohiyo. Ningemshauri aache kupitapita mitaani na kispika chake hicho. Aweke matangazo ya mkutano au semina na awaalike watumishi wa mungu ili awze kufikisha na kutetea mada yake.
 
Halafu kaweka msalaba mkubwa...shingoni kazi kweli kweli.
aliponiacha hoi eti serengeti kinywaji muruwa na kinaondoa maradhi,nadhani kina masanilo na fidel wakimwona lazima wataamua kuwa waumini wake
 
Bongo kweli tambarale alafu maisha ni magumu sana..Naona huyo anatafuta advantage ya kupata hela tu sio vingine!
 
siku za mwishoo kutakuwepo na manabii wengi wa uongo na injili itaubiliwa bila kukoma
 
haya kazi kwenu Walokole akina Maxshimba,Buchanan, SCHMIDT,na wenzake Manabii wa uomngo wanaibuka kila pembe wakizungumzia biblia yenu iliyokuwa na upungufu haya kazi kwenu jamani
 
Oh my Jesus, forgive us our sins, save us from the fires of hell, lead all souls to Heaven especially those who are most need of thy mercy.
 
siku za mwishoo kutakuwepo na manabii wengi wa uongo na injili itaubiliwa bila kukoma

I short naweza nikasema huyu mtu Ni muhuni wa kutupwa!
Hajui asemalo, na anajua atawapata walevi wamsaidie kwa sadaka zao na aweze kuishi hapa mjini!...shame on him!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom