Hotuba ya JK ndio ile hotuba ya muhongo aliyoitoa pale mjengoni,
Ndio tatizo la kua kiongozi mbumbumbu. Alafu baada ya kumaliza kuongea utumbo wake anaisifu PAC pamoja na Bunge, hii ni dharau kubwa
Kikwete alikuwa anawapa darsa.
Na darsa limewaingia, hamna hoja mmebaki kubwabwaja na kuhororoja, mambo ya msingi mnayaacha.
Ngoja niwape darsa la Kikwete kwa lugha mnayoielewa.
Pesa zilizokuwa escrow account: si za Umma za PAP.
Kutaifisha mitambo: Sahauni hilo hizi si enzi za Nyerere.
Bodi ya TANESCO: Hata kuliongelea na kulipendekeza ni ujinga kwani muda wake umekwisha. Tumeshachaguwa Mwenyekiti mpya.
Mikataba ya umeme: Kuiptia tu, tutaipitia hakuna shaka, iko minne tu. PAP, Symbion, Aggreko na Songas.
Tume ya majaji - Hilo si langu tunawaachia wenyewe mahakama waamuwe.
AG: Hana makosa kaondoka kiume, hatuna haja ya kumjadili zaidi.
Tibaijuka - hakufata maadili, tumem fire.
Mhongo - Uchunguzi unaendelea, hatuhukumu bila kuwa na ushahidi kamili.
Maswi - Watajuwa kamati sijui tume ya maadili, sisi hatumfukuzi kazi.
Wenyeviti wa kamati za bunge - Hilo watajuwa wenyewe bungeni huko, si letu.
Stanbic: Uchunuzi utafanyika kubaini kama kweli wanasafisha fedha chafu, hatuwezi kuhukumu tu, kuna wenye kazi zao.
Rushwa: Tutaiongezea nguvu TAKUKURU, vipi mna zaidi?
Kodi: Aaaah toka lini mnunuaji akalipa Capital gains tax? haimuhusu Habinder hiyo kabisa. Ruge kalipwa na yeye kalipa kodi, mnataka nini zaidi?
Hongereni sana PAC kwa kazi ya kijinga na maazimio yenu yote yalipigwa chini na mlishindwa kuyatetea maazimio yenu mpaka bunge likaunda kamati nyingine ya dharura, hongera sana kamati mpya ya mama Malecela kwa kuwa save akina Zitto.
Kuna lingine zaidi?