Hussein Massanza
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 1,016
- 2,195
Straika wa Ghana, Asamoah Gyan, alifanya kazi kubwa sana iliyosaidia kuifikisha timu yake ya taifa, Black Stars, robo fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2010, Afrika Kusini.
Robo fainali, Ghana ilikutana na Uruguay, ikiwa ndiyo timu pekee ya Afrika iliyokuwa imebaki kwenye mashindano, ilicheza vizuri sana. Gyan alikuwa nyota wa mchezo kwa ‘amsha-amsha' zake za mashambulizi.
Dakika 90 ziliisha kwa sare ya 1-1, zikaogezwa dakika 30 za nyongeza. Mechi hiyo ilikuwa muhimu sana kwa Ghana lakini zaidi kwa Afrika. Sababu ni kwamba kama Ghana ingeshinda mchezo huo, ingeweka rekodi ya kuwa ya kwanza kutoka Afrika kufika nusu fainali, Kombe la Dunia.
Ushindi huo wa Ghana ulikuwa turufu muhimu kwa Afrika kuomba kuongezewa timu katika mashindano ya Kombe la Dunia, kutoka idadi ya sasa ambayo ni mataifa matano tu.
Dakika ya 30, yaani dakika ya mwisho kabisa ya muda wa nyongeza, Ghana ilipata penalti baada ya mtukutu Luis Suarez kuokoa goli mara mbili kwa mkono. Mara ya kwanza alipangua ‘shuti' la Appiah kisha akapangua tena mpira wa kichwa uliopigwa na Adiyiah. Mipira yote ilikuwa inakwenda wavuni.
Shujaa alipoonekana; Suarez alipewa kadi nyekundu na akawa anatoka nje kwa masikitiko, akiwa anatazama chini kwa aibu. Tena inaonekana alikuwa anasali Ghana ikose penalti. Kwa muda ule, endapo Ghana ingefunga, na mpira ungeishia hapo kisha kuivusha Afrika kwa mara ya kwanza nusu fainali ya Kombe la Dunia.
Appiah alisogea kupiga penalti ile, Gyan akawahi mpira kwenda kuutenga. Gyan alipiga shuti (penalti) likagonga mwamba lakini kwa sababu alikosa, inahesabika kama fyongo katika muda wa dhahabu. Suarez alipogeuka na kuona Gyan amekosa penalti, alikimbia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo akishangilia.
Alipokosa tu penalti na mpira ukaisha, yakawekwa matuta. Ghana ikapoteza kwa Uruguay mikwaju 4-2. Wanasema mwisho ndiyo hutoa tafsiri halisi (The end justifies the means), kwa hiyo Suarez akawa shujaa wa Uruguay kwa uokoaji wake wa mkono, maana timu yake ingefungwa muda ule, ndiyo ilikuwa nitolee.
Gyan akageuka mchezaji fyongo kabisa kwa sababu alipiga penalti fyongo. Mchango wake wote ulisahaulika na akageuka adui wa Ghana, adui wa Afrika. Alishambuliwa kila kona ya nchi yake na pande zote za Afrika. Akaporomoka kutoka shujaa wa Ghana mpaka kuitwa msaliti wa Ghana.
Makosa na nyakati! Muda ambao Gyan alikosa penalti ni mbaya sana. Mguu wake ndiyo ulikuwa mwamuzi wa kwenda mbele au kungojea matuta. Fyongo lake likasababisha matuta na Ghana ilifungwa.
Ndiyo maana ilikuwepo ile sheria iliyofutwa ya goli la dhahabu, kwamba ukifungwa ndani ya dakika 30 za nyongeza na mpira unaishi hapo, maana hilo ni goli la dhahabu. Pamoja na kwamba sheria hiyo haikuwa hai mwaka 2010 Kombe la Dunia, lakini kukosa penalti dakika ya 30 ya nyongeza ni fyongo la hali ya juu.
************************

Rais Jakaya Kikwete, alikuwa na nafasi nzuri ya kuupa utukufu uongozi wake wake katika muda wa dhahabu. Maana yupo kwenye kipindi cha lala salama. Amebakiza miezi aiache Ikulu ya Magogoni na kwenda kuishi kijijini kwake, Msoga, Bagamoyo.
Badala ya kutumia vizuri pasi aliyopewa na bunge katika yale mapendekezo nane ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lililokaa kwa maridhiano ya kambi zote bungeni, CCM, Upinzani, Serikali na PAC (Kamati ya Hesabu za Serikali, iliyochambua na kutafsiri ripoti ya CAG kisha kutoa mapendekezo), JK amepiga fyongo.
Kikwete angeitumia vizuri pasi aliyopewa kupitia mapendekezo ya Bunge kuhusiana na skendo ya Tegeta Escrow, siyo tu kwamba angeonekana kiongozi wa mfano Tanzania, bali pia angeacha rekodi iliyotukuka. Watanzania wangemuenzi, kumpenda na kumheshimu sana.
JK hakusoma alama za nyakati. Hata kama ni kutoa nusura kwa watuhumiwa wa akaunti ya Tegeta Escrow, alipaswa kuangalia kipindi ambacho anaucheza huo mchezo wake. Kwanza ni kipindi ambacho wananchi wana hasira sana kufuatia wizi uliofanyika Tegeta Escrow, pili huu ni muda wake wa dhahabu, anapaswa kuutumia vizuri.
Ajabu ya Dk. Kikwete ni kwamba katika muda ambao anatakiwa kupalilia thamani yake kikazi (legacy), yeye ameutumia kusafisha watuhumiwa wa Tegeta Escrow na wakati huohuo anafifisha wasifu wake kazini. Rais wetu ana upendo wa mshumaa?
Kwamba yeye anaungua, halafu anahakikisha Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Eliakim Maswi wanapona. Katika nyakati hizi za kuangushiana jumba bovu, yeye ameamua achafuke, watu wake wapone.
JK anasahau kuwa nchi ilisimama na mamilioni ya Watanzania walifuatilia hatua kwa hatua mjadala wote wa Bunge kuhusiana na Tegeta Escrow. Kwa maana hiyo hawajasahau. Alichozungumza na Watanzania kupitia wazee wa Dar es Salaam, hakuna kigeni hata kimoja.
Zaidi, tumeona makosa kadhaa ya makusudi. CAG (Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali), ripoti yake huwa haipelekwi kwa mkaguliwa, bali huwasilishwa kwa msimamizi wa shughuli zote za Serikali, yaani bunge.
Kwa maana hiyo, bunge lilikuwa sahihi kwa namna zote, maana lenyewe ndilo lenye jukumu la kupokea ripoti ya CAG, kuichambua, kutafsiri na kutoa mapendekezo katika sura ambayo linaona inafaa.
JK kama mkuu wa Serikali, yeye ndiye mkaguliwa, kwa maana hiyo, haruhusiwi kwa mujibu wa taratibu kuchambua na kutafsiri ripoti ya CAG kama alivyofanya. Mimi nimekaguliwa, halafu ripoti ya ukaguzi naichambua na kuitafsiri, ni lazima tafsiri yangu itaelekea kwenye kunipa unafuu mimi. Ndivyo JK alivyofanya!
JK kama mkuu wa Serikali, shughuli zake zinasimamiwa na Bunge. Kwa mantiki hiyo, alichotakiwa kufanya ni kusoma na kutekeleza tafsiri ya Bunge. Palipo na kokoro, alipaswa kufuata taratibu zinazotakiwa kurejesha mjadala bungeni.
Kwa mantiki hiyo, bado natambua kwamba fedha zilizochotwa na PAP (na ushirika wake wote) kwenye akaunti ya Tegeta Escrow ni shilingi bilioni 306, na siyo shilingi bilioni 202 ambazo JK alizitaja kwenye kikao chake na wazee. Sababu ni kwamba JK anajaribu kupindisha tafsiri kwa sababu yeye ndiye mkaguliwa, lazima apunguze makali ya madudu katika Serikali yake.
Dhamira ya hotuba ya JK, ilikuwa ni kuwafanya Watanzania waone kwamba bunge zima lenye wabunge zaidi ya 300, wengi wao wakiwa wasomi wakubwa kabisa, madaktari, maprofesa, eti baada ya kusoma ripoti ya CAG walikosea hesabu kusema ziliibiwa bilioni 306. Akasahihisha, zilizoibiwa ni bilioni 202.
Hata kwa hoja yake hiyo, JK namna alivyokuwa anafafanua, utadhani fedha hizo shlingi bilioni 202 ni chache, kwamba wananchi wasishtuke kudhani ni nyingi, bali ni shilingi bilioni 202 tu! Tafadhali sana mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
JK akanena jambo lenye mshangao mkubwa: "Mwanasheria Mkuu alipojiuzulu, alisema wengine wote waachwe kwa sababu kama ni makosa waliyafanya kwa ushauri wake." Nilijisikia vibaya sana Mkuu wa Nchi kuzungumza hivi.
Kumbe tuna viongozi wasiotumia akili zao. Wasio na uwezo wa kuchanganua ushauri mbaya na mzuri. Yaani mtu analitia hasara taifa bado anaombewa huruma na Mkuu wa Nchi. Ni makusudi tu, kwani JK anajua kwamba kuufanyia kazi ushauri mbaya ni uzembe.
Ni makusudi tu; JK anajua kwamba watu hufanya uzembe wa makusudi. Wanatengeneza mazingira ya kupiga noti, kisha wanajikinga katika kivuli cha kutojua, kudanganywa au kushauriwa vibaya. Kufanya makosa kwa kutojua, kudanganywa au kushauriwa vibaya yote ni uzembe. Na ni uhujumu uchumi.
Mwaka 2008, Zakia Meghji aliachwa kwenye muundo wa Baraza la Mawaziri baada ya kuvunjika kufuatia aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa kujiuzulu kutokana na skendo ya Richmond. Kosa la Meghji lilikuwa kukiri kwamba aliwahi kupotosha ukweli kuhusiana na sakata la EPA kwa sababu alidanganywa na maofisa wa Benki Kuu.
Waziri mzima unadanganywa! Alishambuliwa kwelikweli kwa sababu ni uzembe wa hali ya juu. Ila hivi sasa, Muhongo na Maswi wanaombewa msahama kwa sababu walishauriwa. Hapa ndiyo inanifanya niamini kuwa Fredrick Werema alilazimishwa kujiuzulu ili awanusuru wengine. Eti walishauriwa vibaya. Waziri mzima unashauri vibaya na unatekeleza ushauri husika.
Novemba 29, mwaka huu, Werema pamoja na kukiri kuwa yeye ndiye mtoa ushauri, ila alijitetea kwa kuhoji kuwa ni kwa nini mzigo wote anaangushiwa yeye? Kama aliagiza fedha za Tegeta Escrow zitoke bila kulipiwa kodi, waziri wa fedha alikuwa wapi kuzidai?
Hapa ni wazi kwamba Werema alitaka aondoke na wenzake akiwemo waziri wa fedha. Haya maneno ya JK kwamba wengine waachwe kwa sababu yeye ndiye aliwashauri si ya kweli. Tafadhali JK, Watanzania wamekuchagua kwa imani kubwa.
Namshangaa JK; pamoja na kujaribu kutetea kwamba zile pesa za Tegeta Escrow hazikuwa za umma lakini mwishoni alikiri kuwa zilikuwepo fedha za Tanesco kwa maana ya gawio baada ya ukokotoaji wa viwango vipya vya tozo ya uwekezaji (capacity charge). Data zilimsuta.
Akakiri pia kuwa zilikuwepo fedha za umma kwa maana ya kodi. Kwa maana hiyo, pamoja na jaribio lake la kuzungukazunguka ili ije tafsiri tofauti na ile ambayo wananchi wanaijua kutokana na mijadala ya Bunge, bado alirejea ukweli uleule kwamba fedha za umma zimechotwa kwenye akaunti ya Tegeta Escrow.
Nikashangaa sinema hii; Profesa Anna Tibaijuka aligawiwa tu. Na kitendo cha kutengua uteuzi wa Tibaijuka, maana yake JK bila shaka anakubali kuwa zile fedha hazikuwa halali. Sasa inakuwaje unamfukuza kazi aliyepewa mgawo na kuwaacha walioruhusu fedha zile zitoke?
JK anamuondoa kazini Tibaijuka, wakati huohuo anampongeza Werema kwamba ni mtumishi mwadilifu na mwaminifu. Tibaijuka anaondoka kwa kupokea fedha chafu, halafu mtu ambaye ushauri wake ndiyo ulisababisha uchafu huo ukafanyika, unamwita mwadilifu na mwaminifu. Sikutarajia kama Rais wetu anaweza kututania kiasi hiki.
Hivi hatuwazi kweli kama ushauri wa Werema ulikuwa na sura ya rushwa? Hatuwazi kweli kama mgawiwa wa mbali, Profesa Tibaijuka alipewa shilingi bilioni 1.6, je waliohusika na ‘mchongo' wenyewe, kama Werema, Muhongo na Maswi, wao wamebeba ngapi? Sandarusi na lumbesa!
Katika hotuba yake, JK alikiri kuwa PAP haiaminiki na hata umiliki wake IPTL una mashaka mengi. Mtu aliyeruhusu kampuni hiyo itwae uwekezaji mkubwa nchini kwa uzembe ni Muhongo kwa sababu hakufanya uchunguzi hakiki (due diligence). Eti huyu anawekwa kiporo.
Katika wizara hiyohiyo ya Nishati na Madini, alikuwepo Katibu Mkuu, David Jairo. Alipokutwa na skendo ya rushwa, alisimamishwa kazi haraka sana. Safari hii kwa Maswi, JK anasema kumwadhibu mtumishi wa umma kuna taratibu zake, kwa hiyo mpaka uchunguzi kwanza ufanyike.
Kwa kifupi, JK alichofanya, alisoma ripoti ya CAG kivyake, akaitafsiri kwa namna ambavyo ilimpendeza, halafu akaanza kujibu mapendekezo ya Bunge. Hakuwa pale kutekeleza, hotuba yake ilikuwa inajibu mapigo ya Bunge.
Bunge lilishauri mikataba iwekwe wazi, JK anajibu hilo likifanyika litakimbiza wawekezaji. Swali; ni kampuni gani inayofanya kazi na serikali isiyojua kwamba serikali ipo kwa ajili ya wananchi? Kituko; mwananchi ndiye anachagua watu wa kuwapa dhamana ya serikali, halafu serikali inafanya mambo yake kwa usiri, mtoa dhamana hajui.
Na huo usiri una maana gani basi? Hapa tusiendelee kuuziana mbuzi kwenye gunia, mtu ambaye hataki kufanya kazi kwa uwazi na serikali, anataka mambo ya mafichoni, huyo atupishe. Waje wawekezaji wanaojiamini katika biashara zao, wenye kuruhusu mikataba iwe wazi, wananchi waone, wabunge waipitie na kuijadili.
Bunge limeshauri serikali iichukue mitambo ya IPTL na kuimilikisha Tanesco. JK anajibu hilo pia litakimbiza wawekezaji. PAP ni matapeli, tayari imeshaonekana hivyo, Mkuu wa Nchi anataka tuendelee kuuziwa umeme na mtu ambaye ametufanyia utapeli mkubwa. Hapa kuna namna.
JK hakujibu swali hili; IPTL ina wabia wawili. Menchmar yenye umiliki wa asilimia 70 na VIP yenye asilimia 30. Kwa mantiki hiyo, fedha zilizokuwemo kwenye akaunti ya Tegeta Escrow, katika hesabu stahili ya IPTL, VIP gawiwo lake ni asilimia 30.
Kwa mfano, kama fedha zote za Tegeta Escrow (shilingi bilioni 306), zingekuwa mali ya IPTL, maana yake VIP fedha zake ni shilingi bilioni 91.8. Na zinazobaki, ndizo zinazomilikiwa na Menchmar ambayo inatajwa kuuza hisa zake mpaka kufika kwa PAP.
Ajabu ni kwamba PAP baada ya kuchota fedha hizo (shilingi bilioni 306), ikazitumia hizohizo kununua hisa asilimia 30 za VIP kwa shilingi bilioni 104. VIP inatambua kuwa imeuza hisa zake kwa fedha ambazo na yenyewe ilikuwa inastahili.
Wewe na mwenzio mnamiliki duka, halafu mwenzio anatumia mauzo mliyopata pamoja kununua hisa zako zote ili duka libaki mikononi mwake, na wewe unakubali, wakati mlitakiwa kwanza mgawane mauzo kisha ndiyo mazungumzo ya mauziano ya hisa yafanyike.
Ukiangalia mchezo mzima ulivyokwenda, hakukuwa na bahati mbaya hapa. Kila kitu kilifanyika kwa makusudi. Hata wanaojaribu kumsafisha James Rugemalira wa VIP nao wanakosea, maana huo ulikuwa mchongo wa jumla.
Rugemalira anavyoijua fedha, asingekubali aibiwe kwa kununuliwa kwa fedha zake mwenyewe kisha akae kimya na matokeo yake aanze kugawa fedha kama mtu aliyechanganyikiwa. Kuna kitu hapa. Regemalira, Herbinder Sing Sethi wa PAP, Werema, Muhongo, Maswi, Andrew Chenge na Tibaijuka, wakibanwa sawasawa watataja tu!
Sidhani kama JK anashindwa kuwa na tafakuri hii. Ila atambue tu kwamba anapiga fyongo katika muda wake wa dhahabu. Katika muda wake huu wa lala salama, matendo na maneno yake, ndivyo vitaamua aondoke Ikulu kwa heshima kinyume chake.
By Luqman Maloto