Tecno watoa simu ya camera ya mbele yenye mp 21

Tecno watoa simu ya camera ya mbele yenye mp 21

mkuu tushalizungumzia sana humu jukwaani, megapixel si quality ya camera ni ukubwa wa picha, jinsi megapixel zinavyokuwa nyingi ndio jinsi picha zinavyokuwa kubwa. mfano unahitaji kupigwa picha uekwe kwenye bango la barabarani ndio utahitaji megapixel nyingi ila matumizi ya kawaida hata megapixel 2 zinatosha. kitu muhimu kwenye camera ni aina na ukubwa wa sensor ya camera. unapokuwa na sensor kali na kubwa basi mwanga utaingia mwingi na hata picha zitakuwa angavu. kuna mtu amepost sensor yake yaani sony imx 230 kama ni kweli si sensor mbaya ni ya mwaka 2014 kama unataka kuona quality yake lenovo vibe x3 wametumia sensor hii hii


kuhusu hio soc yaani mediatek helio x20 ina mambo haya mtu anasakiwa ayajue

inatumia ddr3 badala ya ddr4
wakati hadi fLagship za mwaka jana na juzi kama vile galaxy s6 zinatumia ram za lpddr4 tayari hii soc ya helio x20 inatumia lpddr3 ambazo ni ram za kizamani nsa zinatumika kwenye simu za bei rahisi. ukiwa na ram ya ddr3 inakula zaidi umeme na pia haipitishi bandwidth nyingi kama ddr4 hebu angalia hii graph
RAMPerf.jpg

hapo unaona lpddr3 inakula umeme mwingi na ipo slow compare na lpddr4

single chanell badala ya dual chanell ram
simu za kisasa na flagship soc (processor) zake zinakuwa na dual chanell hivyo kupitisha data mara nyingi zaidi ya single chanell
mfano angalia hii test ya single na dual chanell
YE49CDJ.png


sasa imagine simu ina single chanell lpddr3 na nyengine ni dual chanell lpddr4 tofauti ya perfomance ipoje?

haikai na chaji kama wanavyosema
simunyingi ambazo zinatumia helio x20 hazikai na chaji, moja kati ya makampuni yaliyoitumia ni meizu, meizu pro 5 ilitumia exynos 7470 wakati pro 6 ilitumia helio x20 pro 6 ilikuwa na battery ndogo kwa mah 500 lakini ilipitwa karibia nusu nzima
gsmarena_001.jpg

gsmarena_001.jpg


manufacturing process
yenyewe inatumia 20nm wakati flagship za kisasa ni 14nm ambazo zina perfomance zaidi na pia hazili sana umeme

bei
simu za helio x20 zinapatikana kwa bei rahisi sana
, mfano le eco le 2 ipo kenya around 17,000 hadi 18,000 hivi, kwa hela za kibongo bongo ni kama shilingi laki 4 au chini ya hapo. nasubiria bei ya Tecno watakayotoa na wale wanaowatetea kuwa ni wakombozi wa maskini


Asante mkuu
 
simu gani ata house gerl akikusanya mishahara ya miezi 3.ananunua simu aidumu ata miezi sita.walitoa h6 c8.ziko wapi kwishinei
 
simu gani ata house gerl akikusanya mishahara ya miezi 3.ananunua simu aidumu ata miezi sita.walitoa h6 c8.ziko wapi kwishin
 
Aise nina L8plus kwa charge sidhani kama inamshindani mpaka 120hrs ndio unatafuta charger ilipo, sihitaji kusikia hivyo vimeo vingine.
Kweli natumia hiyo mashine ni hatari sijaijutia tecno, nilikuwa na s5, battery ilinisumbua sana
 
Watu wengine wanapenda sifa za kijinga kama mwenzio anatumia tecno na inakizi mahitaji yake anamzarau ya nn, nilikuwa natumia Samsung Galaxy 5, battery ikanizingua sana nikaona nijaribu tecno l8 plus, iko vizuri sana, inakadhi mahitaji yetu, na nasikia inakimbiza soko la Afrika sasa hivi wameanza kuingia mid east na South America
 
Duh Tecno ya million 1.. Yenye camera sensor sawa na iliyopo kwenye Xiaomi mi4c kwa Ile ndogo na ile kubwa ina sensor sawa na ya xperia z3+ *kwa mujibu wa sources nilizopitia *(kwa kifupi haiwezi shindana na camera yoyote kwenye simu high end ya mwaka huu au hata mwaka Jana) na processor yenye core 10 zisizo na faida .. Tecno punguzeni bangi kama mtu una akili timamu bora ukanunue One plus 3 au ZTE axon 7.

Au kama unapenda simu zenye ui za kichina, na ma core mengi , pamoja na dual camera chukua hata Huawei honor 8 kwa bei rahisi zaidi.
Ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha, mkuu acha hasira, ila kiukweli fans wa tecno huwa wanakera, mi simu ya tecno hata ukinipa leo kesho utakuta nimeiuza au nimeigawa
 
Serious!?
yes mkuu iphone ilinizingua network nilihangaika mpaka mafundi wakawa rafiki zangu kariakoo nikaja galaxy note one hiyo betri
ilinikimbiza haimalizi siku ishaisha chaji


simu za android ni techhno tu naikubali
 
Watu wengine wanapenda sifa za kijinga kama mwenzio anatumia tecno na inakizi mahitaji yake anamzarau ya nn, nilikuwa natumia Samsung Galaxy 5, battery ikanizingua sana nikaona nijaribu tecno l8 plus, iko vizuri sana, inakadhi mahitaji yetu, na nasikia inakimbiza soko la Afrika sasa hivi wameanza kuingia mid east na South America
Tatizo mnaleta dharau kwa kufananisha na simu ambazo sio kiwango cha tecno, unawezaje kuifananisha tecno na iPhone au Samsung!? Tecno ana watu wake wa kufananishwa, kumbuka ukianza dharau lazima na wewe udharauliwe
 
21Mp Ya camera ya simu ya Techno ni Sawasawa na 3Mp ya kwenye simu za Nokia
 
yes mkuu iphone ilinizingua network nilihangaika mpaka mafundi wakawa rafiki zangu kariakoo nikaja galaxy note one hiyo betri
ilinikimbiza haimalizi siku ishaisha chaji


simu za android ni techhno tu naikubali
Tatizo lako ulinunua second hand hizo devices na tayari waliokuuzia walishaona hayo matatizo ndo wakakutupia zigo, ukitaka kuona raha ya hivyo vitu chukua new brand ila kama huna uwezo utaishia kwenye hizo tecno na utaona zipo bora zaidi
 
Dah hata utani haufananii....

Kwamba Iphone, hTC na Samsung zinazidiwa na tecno!

hayo ni maoni yangu baada ya kutumia zote hizo mpaka nikaichagua techno

kwanza interms of charge hakuna simu inayomgusa techno ndio maana techno huna haja kutembea na power bank
na hicho ndicho kitu cha msingi katika simu
camera wapo vizuri
storage the same
speed wapo vizuri
kipi cha zaidi

labda cha kuniudhi katika mfumo wao tu android maana after a while kuzingua kwingi tofauti na window phone au ios
 
Tatizo lako ulinunua second hand hizo devices na tayari waliokuuzia walishaona hayo matatizo ndo wakakutupia zigo, ukitaka kuona raha ya hivyo vitu chukua new brand ila kama huna uwezo utaishia kwenye hizo tecno na utaona zipo bora zaidi
yeah iphone nilichukua second hand lakini htc na sumsung ni new lakini matatizo ni yale yale miezi sita ilikuwa mingi kuijutia pesa yangu

pili kununua kwa mtu haiwezi justfy ubora wa kitu mkuu
 
Back
Top Bottom