mkuu tushalizungumzia sana humu jukwaani, megapixel si quality ya camera ni ukubwa wa picha, jinsi megapixel zinavyokuwa nyingi ndio jinsi picha zinavyokuwa kubwa. mfano unahitaji kupigwa picha uekwe kwenye bango la barabarani ndio utahitaji megapixel nyingi ila matumizi ya kawaida hata megapixel 2 zinatosha. kitu muhimu kwenye camera ni aina na ukubwa wa sensor ya camera. unapokuwa na sensor kali na kubwa basi mwanga utaingia mwingi na hata picha zitakuwa angavu. kuna mtu amepost sensor yake yaani sony imx 230 kama ni kweli si sensor mbaya ni ya mwaka 2014 kama unataka kuona quality yake lenovo vibe x3 wametumia sensor hii hii
kuhusu hio soc yaani mediatek helio x20 ina mambo haya mtu anasakiwa ayajue
inatumia ddr3 badala ya ddr4
wakati hadi fLagship za mwaka jana na juzi kama vile galaxy s6 zinatumia ram za lpddr4 tayari hii soc ya helio x20 inatumia lpddr3 ambazo ni ram za kizamani nsa zinatumika kwenye simu za bei rahisi. ukiwa na ram ya ddr3 inakula zaidi umeme na pia haipitishi bandwidth nyingi kama ddr4 hebu angalia hii graph
hapo unaona lpddr3 inakula umeme mwingi na ipo slow compare na lpddr4
single chanell badala ya dual chanell ram
simu za kisasa na flagship soc (processor) zake zinakuwa na dual chanell hivyo kupitisha data mara nyingi zaidi ya single chanell
mfano angalia hii test ya single na dual chanell
sasa imagine simu ina single chanell lpddr3 na nyengine ni dual chanell lpddr4 tofauti ya perfomance ipoje?
haikai na chaji kama wanavyosema
simunyingi ambazo zinatumia helio x20 hazikai na chaji, moja kati ya makampuni yaliyoitumia ni meizu, meizu pro 5 ilitumia exynos 7470 wakati pro 6 ilitumia helio x20 pro 6 ilikuwa na battery ndogo kwa mah 500 lakini ilipitwa karibia nusu nzima
manufacturing process
yenyewe inatumia 20nm wakati flagship za kisasa ni 14nm ambazo zina perfomance zaidi na pia hazili sana umeme
bei
simu za helio x20 zinapatikana kwa bei rahisi sana
, mfano le eco le 2 ipo kenya around 17,000 hadi 18,000 hivi, kwa hela za kibongo bongo ni kama shilingi laki 4 au chini ya hapo. nasubiria bei ya Tecno watakayotoa na wale wanaowatetea kuwa ni wakombozi wa maskini