Tecno User Vs Samsung and iphone user

Tecno User Vs Samsung and iphone user

Umezungumza mambo mengi lakini nasikitika kukwambia kwamba kiufundi/kiteknilojia hayana mantiki,simu karibu zote zinatumia hardware zinazo fanana kuanzia processor na chipsets mpaka Operating Systems save Iphone na Black Berry ambazo OS zake ni tofauti lakini hardware ni zile zile.

Naona maoni yako yamekaa kaa kishabeki zaidi kuliko kiuhalisia,lengo lako ni kutaka kuonyesha kwamba Watanzania wanao tumia simu za TECHNO ni washamba au masikini vile wakati wewe katika maoni yako unaonekana wazi wazi uelewi vizuri jinsi mobile phones zinavyo undwa/ fanya kazi,kuanzia: hardware,firmware,software:OS na apps zake, ndio maana unatujia na madai eti TECHNO inasumbua kwenye google!! nani kakwambia kwamba kampuni ya TECHNO inahusika katika masuala ya ku-code search engines za mitandaoni??? Mara eti speaker za Techno zinakorofisha baada ya mwaka mmoja kupita, nani kakwambia kampuni ya Techno inaweka timer ya ku-degrade quality za speaker baada ya mwaka mmoja kupita? mara, sijui IPhone haiwezi kuwa hacked kuna ukweli gani katika madai yako. Bottom line is: msitake kukatisha tamaa Watanzania wenzenu, wana akili timamu za kuchagua wanacho kipenda kutegemea na mifuko/mahitaji yao.
Hawawezi kukuelewa mkuu ata ukiwaambia hivyo wacha wapigwe cha juu.
 
Watumiaji wa tekno wabishi sana .....bhc mkuu tekno n sawa na iphone....umeshinda au sio....ila ukweli utabaki palepale tekno n simu za nchi maskini sana.....sina muda wa kukufanya uamin kuwa ubora wa tekno uko chini kulko iphone,kama kwako iphone n sawa na tekno poa tu hyo n kimpango wako wew,hata tandale n sawa na masaki mwingne anaamin hvo ila kusema iphone n sawa na tekno in quality juu n upumbavu na sio ujinga maana umevuka mipaka ....ushabiki wa kipuuz usio na fact kama huu nishaachana nao...mm natumia tekno ila najua iphone au Samsung sio sawa na haya makopo ya mchina...amini ujuavyo wew ..kimpango wako
Ukweli umekwishauzungumza kaka, katika maisha yangu, nimewahi tumia smart phone ya tecno L6 (kati ya mwaka 2014), ilikuwa ni moja ya simu nzuri tu za tecno ilhali siwezi kusema kwamba ni bora zaidi ya simu nyingine hususan kwa upande wa i phone na samsung na kamwe siwezi. Wengi wanahusisha ukweli ama "fact" na ubaguzi kitu ambacho si kweli, ukweli utabaki kuwa ukweli, hiwezekani hata siku 1 vitu viwili kuwa sawa, kuna kilicho juu ya chenzie ama kilichochini.
 
Transsion Holdings is a Chinese manufacturer of smartphones.
It is the largest smartphone company by sales in Africa, and also sells smartphones in India, Pakistan and South East Asian countries. Its brands include Tecno, itel, Infinix, Spice and oraimo.
Kumbe ni ndugu zetu mkuu na hao wa infinix wanaojiona wako juu kumbe ni ni ndugu zetu pia
 
Kumbe ni ndugu zetu mkuu na hao wa infinix wanaojiona wako juu kumbe ni ni ndugu zetu pia
Kimsingi itel ndio kaka kama sikosei.
Tecno ni ubunifu wa Mnigeria akishirikiana na Mchina walekutana huko Lagos na kuingia mkataba na hawa Transsion Holdings(pengine tuiite Itel) ili wawatengenezee simu kwa jina(brand) ya Tecno ili wakafanye biznee.
 
Mi ni tecno user na siyo kwamba sijawahi kumiliki samsung hapana ila ilinichosha kutokana na kutaka kunigeuza kuwa teja wa kwenye soketi ya umeme.

Toka nimeanza kutumia tecno hizo changamoto kwangu ni no japo hazidumu sana sometime na mapicha picha yake lakini Tecno is the best kwangu.

---inakaa na chaji 24+ hours kama sina mambo ya kufanya online.

__Camera yake iko vizuri .

__Kioo kikubwa

__Rahisi kuitumia haina mambo mengi.

__Space ya kutosha tu 16GB siyo haba kwa matumizi yangu binafsi.

__bei yake ni kawaida tu kwa mimi mjasiriamali au ata mkulima kuweza kuimudu.

__Upande wa data ni 4G+ na hazina ugumu kwenye upande wa Network setting.


Mnaotuponda watumia Tecno mkuje hapa mtupe Utofauti wa simu zenu.


Mi niko hapa natumiaTecno na hii post mnayoina nimeandika kwa kutumia tecno bila shaka mmeiona haina tofauti na atakaekuja kuandika kwa kutumia Samsung au I phone.
Kwan wewe uli tumia samsung gan? Maana samsung yangu inakaa na chaj
 
Ngoja waje mpambane ila kiukweli Tecno niliwahi tumia na ikanizingua upande wa Network yaani ukiwa mjini ndio unapatikana nikirudi home ni kama nina kopo tu.

Toka hapo sijawahi tumia tena Tecno aiseee na sitatumia tena. Ilikuwa Tecno C9 hiyo.
C9 ina mtandao mbovu
 
Ngoja waje mpambane ila kiukweli Tecno niliwahi tumia na ikanizingua upande wa Network yaani ukiwa mjini ndio unapatikana nikirudi home ni kama nina kopo tu.

Toka hapo sijawahi tumia tena Tecno aiseee na sitatumia tena. Ilikuwa Tecno C9 hiyo.
Mkuu Hajra now unatumia ipi🙂🙂🙂
 
Haijalishi una simu ya aina gani maadamu tu ni made in China sisi sote ni ndugu
 
Nilikuwa napenda sana lg na nimetumia sana kuanzia lg v10,lg g3,samsung s5,4 na 3 ila tatizo ni moja hazikai na chaji tena bora Samsung kuliko lg zinapata moto kama zimetoka jikoni.ila saizi nimeamia kwenye iphone chaji saa 24 halafu data zipo on pia haipati moto gb zakutosha 128 .
Samsung at least uchukue s6 edge kwenda juu za chini izo amna kitu
 
Haijalishi unatumia simu ya aina gani kama wewe simu yako ni made in China sisi sote ni ndugu. Aliyetengeneza yakwako ndiyo katengeneza ya kwangu,unapiga kelele wakati wewe mchina na mimi mchina pumbaaaaaaaaavu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom