Tecno Camon 18 kuja na Gimbal Kamera

TECNO Tanzania

Senior Member
Jul 6, 2016
192
216
Kuelekea mwisho wa mwaka 2021 kampuni ya simu za mkononi TECNO yenye mashabiki wengi hasa upande wa simu janja inatarajiwa kuzindua toleo jipya la mfululizo wa simu zake aina ya TECNO Camon 18 yenye ubora ulioboreshwa hasa upande wa picha na video.

Series ya CAMON imekuwa ikiaminika kuwa na simu zenye kamera kali kutoka kwenye kampuni hiyo, japo simu hiyo haijatambulishwa rasmi lakini tayari kuna tetesi huenda simu hiyo ni TECNO Camon 18.

TECNO Camon 18 inasemekana kuja kuwa suluhisho kwa wenye uhitaji mkubwa wa kamera katika kazi za kila siku hata kwa waandishi wa habari itawasaidia katika kuchukua matukio kadha wa kadha ambapo ina Mega Pixel 64.

Picture 1.jpg

Picha:muonekano wa CAMON 18



Simu hii inayosemekana kuwa camon 18 ndiyo simu ya kwanza TECNO kuwa na GIMBAL CAMERA hii ni kamera ya hali ya juu sana katika mfumo mzima wa uchukuaji video kuwahi kutokea TECNO ambapo inaweza kurekodi video HD katika mazingira yoyote yale hata kama mchukuaji video anakimbia au kutembea lakini video haitotingishika, na uwezo mkubwa wa ku-zoom mara 60X zaidi.

Picture 3.png

Mfumo wa ufanyaji kazi wa Gimbal camera


Pia wameboresha uwezo wa kuhifadhia kumbukumbu ni mkubwa zaidi ambapo itakuwa na 256GB ROM kwa 8GB RAM hivyo kuzidi kumvutia mteja kumiliki simu hii yenye uwezo mkubwa zaidi.
Kufahamu Zaidi kuhusiana na CAMON 18 tembelea: shorturl.at/isvzM
 
Mkuu tetesi za Bei ya hiyo simu zikoje? Nimevutika Sana,maana kazi zangu Mimi zihusu picha muda mwingi!!!
 
Nyie vipi ? Sasa Tetesi zinatolewa na akaunti rasmi ? Tetesi zinatakiwa zitoke uchochoroni huko.
Mimi nina Tecno ipo android 6.0 ni lini nitapata android 12 au ndio basi tena ?🐒
Tulie tu ndugu yangu
 
Mkuu tetesi za Bei ya hiyo simu zikoje? Nimevutika Sana,maana kazi zangu Mimi zihusu picha muda mwingi!!!
Shida siyo hizo MP shida ni kama kamera itachukua picha kwa pixel ngapi? Na kama kioo cha simu kitasupport details kuonekana vyema.

Waweza ona picha kwenye simu inaonekana nzuri ila ukiiweka kwenye computer unaona haina ubora kama uliouona kwenye simu.
 
Shida siyo hizo MP shida ni kama kamera itachukua picha kwa pixel ngapi? Na kama kioo cha simu kitasupport details kuonekana vyema.

Waweza ona picha kwenye simu inaonekana nzuri ila ukiiweka kwenye computer unaona haina ubora kama uliouona kwenye simu.
So kipi ni kipi mkuu?
 
Eti " japo simu hiyo haijatambulishwa rasmi lakini tayari kuna tetesi huenda simu hiyo ni TECNO Camon 18. "😄😄
Hawa watu ni wajinga asee, simu inatangazwa hadi kwenye vituo vya tv afu wao wanasema eti ni tetesi haijatambulishwa bado
 
Ukiitumia baada ya Mwezi mmoja inaanza ku stack stack, kuchemka chemka hovyo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom