Ndugu wapenda technologia….
Hii yote inahusu simu yangu ya iphone
Leo nimepata pigo kubwa la security Bleach KWA KUKUSUDIA NA PASIPO KUKUSUDIA
Hivi juzi kati nimenunua simu nyingine Iphone 11 kutoka ka mtu naefahamiana nae na mm nililua natumia iphone X max
Sasa changamoto ikawa kwene kuhamisha vitu ! Sikua nauwezo wa kuhamisha vitu kutoka iphone x had 11 kwa PAAP…
Najua technologia hiyo ipo lakin ilinibid niende kwene maduka ya iphone ambapo najua wangenichaji pesa kadhaa.
kwakua sikua na haraka Nikaona niwe nahamisha vitu taaratibu kwa kutumia Airdrop lakini kuna vingine vili kua sychronized kwene icloud vilihama tu automatic had kwene iphone mpya baada ya kusign email
“MNISAMEHE MATECHNOLOGIST KWA KUA NYUMA KITECHNOLOGIA”
Nimehamisha pcha,video na doument zote zikabaki baadhi tu kama picha 100 na zingine kwene Vault.. wataalamu mtakua mnajua vizuri kua huku ndiko zambi zote zipo😀😀😀 na privacy kubwa nk
Wakati vitu baadhi nikiwa na vimalizia nikaendelea kutumia simu zote mbili huku mpya nikiwa naendelea kudownload na kuijaza na app na vitu ambavyo nitavihigaji na ambavyo huwa natumia nikiwa na simu.
kidupi nilikua sijamaliza vitu vingi tu hasa ku unstall baadhi ya app…. Lakini nikaona niwe naendelea kutafuta wateja kwene mitandao wa simu yangu hiyo ya zamani kwan nishapata nyingine. kwaiyo nikawa naipost post kwene mitandao.
SASA LEO KATIKA HALI ISIYO YA KAWAIDA
Nikaona niende kwa uyu fundi wangu wa ambae nimezoeana nae kama mwana nikamwambia nauza simu …..
kifupi ye ni fundi simu lakini yupo na duka la simu na vifaa vya simu pia.
Nikamwonesha…akaichek akaniambia kwa bei ninayouza kuna demu alikua anataka simu kwaiyo anataka amuoneshe…..
Kwakua alikua amenihakikishia kuna mteja nikasema nihamishe zile picha mia(100) zilizobakia ingawa hazikua na kipengele lakin ziko zingine n too personal, kwa wale tuliosoma risk hii ilikua (LOW RISK)
waakat nahamisha akatokea jamaa anataka kuona simu basi kwa kua nilikua pale nikasubiri sec kumi imalize kutransfer zile picha na hapo hapo nikafuta zilizobakia na ku empty recycle bin……………..MISTAKE NO I
Jamaa akaiangalia akaridhika lakini tukashindwana kwene bei…..
Basi akairudisha wakat ana ikagua simu iliji lock ikabidi niwatajie password ili ikijilock tena afungue aendele
Hili naliita……………MISTAKE NO II
Wakat nimeshare screen password ilikua nauhakika hawa wezi kuaccess Vault wala wasap, FB, nmb app, insta nk
Kwanini kwasababu app nyingi zilikua na password tofauti…..na mm kwa kuwepo pale asingeanza kupekua vitu vingine nilikua SURE 100%
Jamaa akaikagua akakwama bei ikabid mpira urudi kwa BEKI nikautuliza.
Nikapata wazo
“VIPI HATA KWA BAHATI MBAYA AKAOTEA PASSWORD YA VAULT MAANA MARA NYINGI PASSWORD ILIKUA INAFATA PATTERN”
Nikaona nitoe picha na mavideo na madoc yote huko na kuyahamishia kwene simu kisha nikaya transfer na kudelete kote kote
“kwa sasa NILIKUA SAFE japo kwa sasa!”
Nikawa nimetulia…..
Katika kupiga piga story jamaa paap katoweka kuangalia simuoni jamaa
“Uyu fala kaenda wap na simu yangu? Anyway sikutaka kujiuliza sana nikajua kampelekea SIWEMA demu aliyesema alikua anataka simu. So nikachili nikajua muda mfupi atakua amerudi
Kweli kama dk 10 akawa amerudi akasema alienda kumchek uyo demu ila hakumkuta kwaiyo karud had baadae
Kwakua alitumia muda mfupi sikua sikua na waswasi ingawa kuna baadhi ya acc zilikua wazi sikuwaza kwa muda huo angepata muda wakuangalia mambo yangu binafsi
Kuna kazi nilikua nimeitwa naenda kuichek kwa jamaa yangu basi ilibidi nimwachie simu.
Lakini kwakua this time namuachia almost kwa masa3 basi ilibid niongeze security kwene hiyo simu.
Kwakua password alikua nimempa bas niliamua kufuta app ambazo nilikua nomelog in…
Futa FB
futa. insta
Futa jamii forum
Zingine niliziacha nikiamini hawez zifikia kulingana ma app inavofanya kazi
Nikaondoka….. baada ya saa2 hivi nilirudi kupita offisini kwake alikua amefunga.
muda ulikua saa1:30 usiku (ya kiswahili) cha ajabu nilikuta amefunga.Na si kawaida yake,,, kawaida anafunga saa 3 :30 nikajiuliza huyu leo vip na mbona amefunga hajaniambia na nilimuachia simu yangu na ina line yangu ana lengo gan….
kwa kua kulikua na kamvua kadogo dogo sikuwaza ilo nikasepa nyumbani….
Inaendelea