Tech & Gadgets: Jukwaa linavyozidi kupoteza Threads zenye mvuto na old members 2015

Tech & Gadgets: Jukwaa linavyozidi kupoteza Threads zenye mvuto na old members 2015

Hili jukwaa la "Tech,gadgets and science forum" lilitakiwa kuwa na sub-forums ndani yake.

Inaweza kuwa idea nzuri lakini mbona zamani haikuwa hivi ?
au moderation za siku hizi na kipindi kile ni tofauti ?
 
Hili jukwaa la "Tech,gadgets and science forum" lilitakiwa kuwa na sub-forums ndani yake.

Hahahahaha halafu we bwana leo ulitaka kunipandisha pressure yani hiyo animated pic yako sikuiona vizuri nikadhani mdudu kaingia ndani ya simu yangu kumbe picha wacha nipaniki
 
Nadhani uwepo wa Whattsap umeifanya jamiiforums kupoteza mvuto kama miaka iliyopita.

Sio hili jukwaa tu, ni majukwaa yote yapo hivi.
 
I miss old days za hili jukwaa ,, hili jukwaa lilikiwa kina hadhi yake ya kipekee na kiubunifu, kulikuwa na e2themiza mzee wa internet tricks, chief mkwawa yupo kitambo mtaalam wa simu mpaka sasa, good guy, njunwa, mwl rct hata muanzisha thread,,, I really miss those days jukwaa katika ubora wake

Njunwa mavoko alitusaidia sana kwenye Internet kipindi kile bado mabasi yetu hayajapata pancha though na yy customer care yake haikua poa kihiivo
 
Umewataja woote lakini hujamtendea haki Chief Mkwawa huyu jamaa japokuwa na changamoto zote hizo bado yupo na amebaki na ataaendelea kuwa msaada mkubwa WA jukwaa Hili.
 
Umewataja woote lakini hujamtendea haki Chief Mkwawa huyu jamaa japokuwa na changamoto zote hizo bado yupo na amebaki na ataaendelea kuwa msaada mkubwa WA jukwaa Hili.

Mkuu angalia thread title, nimesema JF inavyopoteza old members, Chief-Mkwawa yupo humu 24/7, au unamaanisha nae apotee ?
 
Last edited by a moderator:
snipa your post is on point, couldn't agree more. Mi nimepotea because of what you said na pia kubanwa na issue kibao, mambo yakitulia tu I'll be back as usual.
 
Last edited by a moderator:
I spend most of my time on Quora na stackoverflow, ila mostly on Quora, its more social na i get to learn a lot from there japo wabongo nshawahi kukutana na mmoja tu kule.
nipo huko pia but all i do there ni kuangalia comparisons ya best tech thingys,best tech stuffs reviews in general,tech solutions etc etc.I feel very lost kule,sehemu kama hizi za nyumba zakujidai ndo upuuzi mtu!
 
Hili suala ni sahihi kabisa mkuu na tena limeniface sana binafsi, sio siri sometimes yataka moyo sana, i've been mistreated alot tena mtu from nowhere anakuletea mambo ambayo yako wazi kabisa kuwa ni chuki zisizo na msingi wowote, just because they sometimes don know a thing alike you.
Tatizo kila mtu sahivi akishajua kuroot simu then he thinks yeye ndo one Techie guy anayejua kila kitu!,na badala ya kuchangia mada kwa ujuzi,wengi wanachangia mada kwa "Majibu ya Google" bila hata kujua nini anapost!kwa style hii,ni vigumu sana Logic people kuendelea kuexit Kwenye hii Forum!
 
Kichwa e2themiza kasepa kimoja, munjy1 pia kasepa, Paje anachabo mara moja moja ila hachangii siku hizi.

sitamsahau Paje maishani hasa kwenye net ya 0/= bila kusahau uchakachuaji Wa software kama IDM nk.
Hizi kero za vifurushi vinavyobadiriswha bila taarifa tusingekuwa tunapata shida sana.
 
Last edited by a moderator:
Walichofaa kufanya hawa JF ni kuigawa hii section ya techie iwe na categories kadhaa, kama walivyofanya NairaLand. Kuwe na sehemu ya programmers na nyingine hivyo hivyo ya vitengo vingine. Binafsi huwa nakuja huku kutafuta issues za programming ili namimi nijitose humo kwenye mijadala, lakini wapi, nakutana na mada za wanaJF wanao omba jinsi ya ku-unlock simu n.k.
 
I sure miss the old Tech group indeed!! Alot of challenges zilikuwepo indeed!! But its not all gone, kuna msimu wa hawa watu na naamini utapita! This place will rise from the ashes !! :ranger:
 
Mambo mengi niliyajua huku.hasa simu, mambi ya os za simu nilikuwa mweupe, mambo mengi saaana kina Transistor na mambo ya electronics. Those day ,mambo ya ku unlock modems,ku root simu, aaaaaah! Hata internet za kuchakachua za basi jekundu tulizipata huku. Ma vpn, proxy daaaaaaaa! Raha sana net ya unlimited kwa buku 6 kwa mwezii! Daaah wapuuzi na washenzi wachache wameharibu jukwaa wanataka kulifanya kama mmu na chitchat. Pumbavu xenu nyooooote mlioharibu jukwaa. Wakongwe mrudi sasa.jamii ya hapa itakuwa imejitambua
 
Last edited by a moderator:
sitamsahau Paje maishani hasa kwenye net ya 0/= bila kusahau uchakachuaji Wa software kama IDM nk.
Hizi kero za vifurushi vinavyobadiriswha bila taarifa tusingekuwa tunapata shida sana.
Kabisa mkuu, kuna watu wakaanza kuwekea wenzao vinyongo na vivu huku, watu kama Njunwamavoko, MLMRct wakaanza kususa., dstv ya bure nk.
 
Last edited by a moderator:
Mtu alikuwa anaweza kuingia chimbo anarudi na maujanja ya free inernet anazitupia pm kwa wadau na anaonya zisiwekwe hadharani kwani watakuWa wanaharibu wenyewe wakipita hapa, lakini bado mijamaa unakuta imezimwaga peupe jukwaaani. Ni ujinga tu
Cc mzee wa nokia na symbian os CHIEF MKWAWA, Paje
 
Last edited by a moderator:
I sure miss the old Tech group indeed!! Alot of challenges zilikuwepo indeed!! But its not all gone, kuna msimu wa hawa watu na naamini utapita! This place will rise from the ashes !! :ranger:

Lets hope things will change bro, though it's not soon at al.
 
ni kweli aisee nikikumbuka hata mm kabla sijajiunga rasmi jf nishakuwa naperuzi huku zaidi ya 3yrs ndio baadae nikaamua kujiunga na jukwaa ambalo nilikuwa naperuzi ni hili.
aisee kweli Paje kapotea mazima namkumbuka.sana kipindi cha internet ya guru.

tatizo letu humu wengi hatujui kitu lakini wataalamu wanapojitolea kuweka mambo kuna wengi wanatokea na kuanza kupinga tena kwa kashfa na matuzi na zarau kubwa wakati watu wanakesha na kuumiza kichwa ni vipi wanaokoa jahazi la wana jf wengi wataalam wakakata tamaa mkuu kama @munjy 1 sasa hivi baada ya kutusiwa sana na kutukanwa juu ya vile visumbusi kaamua kuliendeleza upande mwingine kimya kimya.

tatizo wengi kujua kwingi mwisho wa siku wenye uelewa wametuacha wakiwa
Hata mimi nimepotea kitambo sana na huwa napitia kwa mwezi mara 1 au 2 katika Jukwaa ila naona maada zote hazina mvuto hata kukupa hamu ya kuchangia au kusaida na yote ni kohofia kutusiwa maana ilifikia hawa new commers kututusi hadi niliomba uwongozi wa JF wafute thread zangu zote na comments zangu zote za thread za watu wengine, unajuwa wengi hawaelewi reputation za watu sasa unapoanza kumwagia matusi mtu katika mitandao unaharibu reputation zao, na wengine wanashindwa kutambua kuwa wengi huwa tunatumia majina yetu ya ukweli na unapoanza kututusi mitandao inasomwa na wengi, wiki 1 iliyopita nilibahatika kwa mara ya kwanza maishani kuonana na Mshumaa Morogoro (huyu jamaa ni legend humu ndani kwa thread zake za misaada na kufundisha watu hadi kufunga satelite dish kama mtamkumbuka alikuwa na thread ambayo ilikuwa inaongoza kwa viewers na wachangiaji) tulipiga story zaidi ya masaa mawili na tulijadiliana sana kuhusu kurudi kuchangia JF jukwaa letu hili ila mambo mengi yanaturudisha nyuma hadi kukosa imani. Ila bado tupo na tutaendelea kuwepo ila wengi tumekuwa tukitoa misaada kwa njia nyengine, mimi natoa kwa njia ya sms, simu, mtandao wa fb na web Munjy1.com Bingwa wa Ving'amuzi but niko limited sana sababu ya muda na majukumu mengi niliyonayo.
Nafarijika sana kuona watu bado mnatukumbuka na mnatutaja tena kwa vizuri in a positive view. Tupo pamoja
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom