snipa
JF-Expert Member
- Dec 10, 2013
- 4,523
- 2,164
"Tech & Gadgets" linavyopoteza Thread zenye Mvuto na Kuwa jukwaa la Misaada 2015
N:B Ain't joined here long ago, but atleast i know then and now.
Siku zinavyozidi songa mbele jukwaa letu pendwa linazidi poteza sifa stahiki, zamani nilizoea kuskia tu jukwaa bora(ustaarabu na hekima) ni jukwaa la TECH, lakini siku zinavyozidi songa mambo nayo yanazidi kubadilika.
Old members waliokuwa na Reputation(non-dashboard) kubwa wamezidi kutoweka, sio kwamba hawatembelei kabisa JF "No" lakini mtu anapita tu maana kaona thread za ovyo kwenye jukwaa letu hili la Tech and Gadgets.
Kuna members walionipokea enzi najoin JF mara baada yakuwa interested na mada zinakuwa discussed kwenye jukwaa hili, Thread ambazo ukiona title tu unapata hata hamasa kubwa tu yakuifungua, na ukifungua hizo thread unakuta point za maana tu.
- Kulikuwa na best Threads of the Year lakini siku hizi hata hizo best thread kuzipata tu ni issue kubwa sana, maana zimejaa Thread za matatizo/misaada, sio tatizo jukwaa kujaa sana mthread za misaada, lakini hizo thread ukisoma tu title hazina challenge yeyote. Mtu thread title kaandika "Iphone 6" mwingine kaandika "Facebook inagoma" yaani hata kufungua tu hizo thread unaona bora utake a rest with babydrama aside.
- Mbaya zaidi Thread za maana siku hizi zina replies 2/1/0,
- Threads za Shigongo zimejaa siku hizi, yaani mtu anakuandikia title ili uelewe ni mpaka uifungue ndani bila hivyo ni impossible, yaani ukisoma tena unapoteza tu uelewa ulio nao (unaloose badala yakugain)
- SEXTING threads nazo kibao, yaani mtu anakuandikia maneno kama anayoandikiana na mpenziwe kwenye messaging wall (si/c,the/ze,to/2,for/4)
For sure sielewi baada ya miaka 5 mbeleni itakuwaje, HQ members wengi ni nadra siku hizi kwenye kila category,
GRAPHICS DESIGNING & ANIMATING 2D/3D
- - Good Guy
- magembe jr malima
- wickerman
- kadoda11
- Joe Nyandigira
N.K
PROGRAMMING
- - Stefano Mtangoo
- zech
- Nyasiro
- NingaR
- NullPointer
- ub16
- ymollel
N.K
COMPUTING-incl "MOBILE ERAND & PC TRICKS"
- - Paje
- Njunwa Wamavoko
- Mwl.RCT
- @e2themiz
-N.K
snipa 2015