ushahd
Senior Member
- Jul 30, 2019
- 180
- 101
Habari za jion wadau samahn mm nimeomba chuo round ya kwanza mpaka ya tatu sijapata chuo nimesoma Cbg na ufaulu wangu two ya 12 je nauliza kuna uwezekano wa kufungua dirisha kwa awamu ya nne kwa mwaka huu mwenye uzoefu tafadhali
=====================================
Tume ya vyuo Vikuu Tanzania(TCU), imefungua dirisha la udahili kwa awamu ya nne utakaoanza Oktoba mosi hadi 4, mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Septemba 25, Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Charles Kihampa amesema lengo ni kutoa fursa kwa wananchi ambao hawakuweza kuahiliwa katika awamu tatu kupata nafasi hiyo.
Amesema tume imepokea maombi pia kutoka kwa vyuo ambavyo bado vina nafasi kuhitaji kuongezwa muda wa udahili.
“Tume imeongeza muda wa udahili kwa kufungua dirisha la udahili kwa awamu ya nne utakaoanza Oktoba mosi hadi 4,mwaka huu,” amesema profesa Kihampa.
Amevitaka vyuo vyote vya elimu ya juu kubainisha proramu zenye nafasi ili kuwawezesha waombaji kufanya maamuzi sahihi wakati wa kutuma maombi ya udahili.
Amewakumbusha waombaji wote kuwa masuala ya yanayohusiana na udahiliama kuthibitisha yawasilishwe moja kwa moja katika vyuo husika na si TCU.