Sacsosanct
Member
- Sep 2, 2014
- 70
- 100
Wanafunzi wengi wa diploma wamekosa nafasi za vyuo vikuu mwaka huu kwasababu ya kuchelewa kupata AVN namba kutoka NACTE. Kosa sio Lao. Dirisha la tatu limefungwa ndo AVN namba zinatoka. TCU inagoma kuwasaidia. Kwanini wasisaidiwe vijana hawa? Kama vyuo vipo tayari kuwapokea, kwanini TCU inakataa kufungua dirisha? Je, wapoteze mwaka mzima mtaani? TCU inafanya kazi nzuri, Ila kwa hili inapaswa kutafakari hatma za vijana wa kitanzania.