poppah
JF-Expert Member
- Dec 19, 2014
- 630
- 548
Nakumbuka nilipokuwa mtoto watu wazima wakiniuliza,"ukiwa mkubwa unataka kuwa nani?" niliwajibu "nataka kuwa daktari kwani napenda nije kuwasaidia wagonjwa"
Wazazi wangu ni maskini lakini hawakutilia shaka na uamuzi wangu.Walijitahidi kwa hali na mali ili nifikie ndoto yangu.Walilipa karo zangu za shule na hata pesa kwa ajili ya tuition.
Nilipofika A level nilijitahidi sana kwenye masomo yangu ya mchepuo wa PCB.Wazazi wangu hawakuwa nyuma kunipa msaada wa kimawazo na pesa pale ilipohitajika kunilipia tuition na kununua mavitabu makubwa kama BS,Chand,Nelkon na mavitabu mengineyo ingawa hali yao kiuchumi haikuwa nzuri.
Picha lilianza pale NECTA walipobadilisha gia kwa kupandisha grades tukiwa kwenye hatua za mwisho za kumaliza kidato cha sita.Lakini hilo halikunishtua sana nilijitahidi sana bila kukata tamaa ingawa sikusoma shule bora sana.
Matokeo yalipotoka sio haba nilipata Div 2.11 yaani DDC, nikajipa moyo kwamba nitachaguliwa medical school.Part two ya picha ilikuja pale TCU ilipovifungia baadhi ya vyuo ambavyo vinatoa course za afya na kupunguza admission capacity kwenye vyuo vilivyobaki.
Nimepigwa danadana katika selections kutoka 1st round hadi 3rd round.Roho imeniuma pale nilipoona hata hii 3rd round haina vyuo za afya.
Nimebaki kushika tama, medical school ni jambo la kusikika tu kwangu.
Ndoto yangu tayari imeyeyuka.