Habari wana JF,
TCU juzi wametangaza mfumo mpya kwa wanaotaka kuomba nafasi za chuo mwaka huu, ambapo kwa mfumo uliotangazwa, unamtaka mwanafunzi kwenda moja kwa moja chuoni kufanya application.
Sijajua hasa sabab za kubadilisha mfumo, ambapo zaman application zote zilikuwa zinafanyika kwa kutumia mfumo wao wa tehama.
Mfumo wa zamani ulikuwa unaweza kuapply chuo zaidi ya kimoja, tena vilivyopo mikoa tofauti tofauti kwa siku moja na kwa gharama isiyozidi 50,000/=
Sasa kwa mfumo huu mpya walioutambulisha, inamaanisha mwanafunzi kama anahitaji ku apply vyuo vitatu, inambidi afunge safari kutoka huko aliko na kuanza kutembelea chuo kimoja baada ya kingine, kwa haraka haraka tu hapa utaona gharama zinaongezeka mara dufu ya hiyo 50,000/= ya mara ya kwanza.
Zipo kasoro nyingi kuhusu mfumo mpya
Pro Ndalichako tunaomba uliangalie na utasaidie kwa hili tafadhali.
Tangazo lenyewe hilo hapa chini.

- Gharama zake zitakuwa kubwa sana
- Kwa tarehe mlizoweka, kuna baadhi ya wanafunzi watakuwa kwenye kambi za jeshi, kwa hiyo watakosa nafasi ya ku apply.
- Kuna uwezekano pia baadae wanafunzi wanafunzi kuja kufukuzwa vyuoni sabab ya details zao kutotambulia wizaran, kama lililotaka kutokea miezi michache iliyopita
- Na nyingine nying unazoweza kuzifikiria ..