TCU mnaturudisha nyuma. Kwa mfumo wenu mpya wa udahili vyuoni, mnatuonea wananchi

huwa nashangaa sana hizi taasisi zinazojiita HURU
hiv rais anaposema fanyeni jambo flani...na niny kwa taaluma yenu mlikuwa mmejiwekea mkakati mlioona unafaa zaidi, kwanini msikatae au msimshauri akubaliane na mkakati wenu!!!???

kwa mfano mfumo wa udahili wa TCU..ulibadilishwa miaka flani ya katikati kutoka ule wa mwanafunzi kuomba moja kwa moja chuoni na kuanza kusimamiwa na TCU
na kwa maelezo yaloshiba, ulionekana ndio mfumo unaofaa kabisa
sasa inakuaje wakubali kurudi kule walikotoka tena bila ya sababu za msingi???
huo uhuru upo wapi
 
Kama mwanafunzi anataka kusomea sheria katika chuo cha UDSM, mwache aingie kwenye ushindani huo, akipata alhamdulillah, akikosa ajipime mwenyewe kama ni kujaribu kozi nyingine au chuo kingine, na hiyo pia ni fursa kwa career advisers kusaidia watoto wetu.
Nimeshuhudia vituko vingi na CAS ya TCU. Mtoto amefaulu form six masomo ya sanaa division one point 6, anaomba kusoma sheria UDSM lakini TCU wanampangia aende Ruaha kusoma ualimu! Wakati huo huo kuna wenzake wenye ufaulu wa chini zaidi kwa masomo hayohayo na wamepangiwa kusoma sheria ileile aliyonyimwa huyu aliyekuwa anaitaka! Nimeona binti alipata division one ya PCB, ya pointi nane, akaomba kusoma Medicine, akapangiwa kusoma Environmental Health, wakati wenzake wenye ufaulu mdogo zaidi wamepangiwa na hiyohiyo TCU kusoma Medicine. Upuuzi kabisa huu. Hii ni ya kuvunjilia mbali tusuke upya.
 
Habari wana JF,

TCU juzi wametangaza mfumo mpya kwa wanaotaka kuomba nafasi za chuo mwaka huu, ambapo kwa mfumo uliotangazwa, unamtaka mwanafunzi kwenda moja kwa moja chuoni kufanya application.

Sijajua hasa sabab za kubadilisha mfumo, ambapo zaman application zote zilikuwa zinafanyika kwa kutumia mfumo wao wa tehama.

Mfumo wa zamani ulikuwa unaweza kuapply chuo zaidi ya kimoja, tena vilivyopo mikoa tofauti tofauti kwa siku moja na kwa gharama isiyozidi 50,000/=

Sasa kwa mfumo huu mpya walioutambulisha, inamaanisha mwanafunzi kama anahitaji ku apply vyuo vitatu, inambidi afunge safari kutoka huko aliko na kuanza kutembelea chuo kimoja baada ya kingine, kwa haraka haraka tu hapa utaona gharama zinaongezeka mara dufu ya hiyo 50,000/= ya mara ya kwanza.

Zipo kasoro nyingi kuhusu mfumo mpya
  1. Gharama zake zitakuwa kubwa sana
  2. Kwa tarehe mlizoweka, kuna baadhi ya wanafunzi watakuwa kwenye kambi za jeshi, kwa hiyo watakosa nafasi ya ku apply.
  3. Kuna uwezekano pia baadae wanafunzi wanafunzi kuja kufukuzwa vyuoni sabab ya details zao kutotambulia wizaran, kama lililotaka kutokea miezi michache iliyopita
  4. Na nyingine nying unazoweza kuzifikiria ..

Pro Ndalichako tunaomba uliangalie na utasaidie kwa hili tafadhali.

Tangazo lenyewe hilo hapa chini.

Sio kweli , kwani watu si wanachukua fomu online na kuaplly huko huko online ?
 
HUEL

KAMA HUELEWI ULIZA USAIDIWE SIYO KUKIMBILIA KULAUMU.
 
sasa mbona mlikuwa mnapigia kelele kile chuo cha waislam Mum kwa kuwa na mfumo kama huo? hongeren sana mum kwa kuona mbali
 
Rais |Magufuli alisema vyuo vidahili vyenywe! Ndalichako badala ya kumueleza madhara ya kubadilisha mfumo, anamuogopa! Ndalichako,Ndalichako, Ndalichako, MUNGU ANAKUONA, UNATETEA TUMBO LAKO, NALO LITAOZA KAMA YA KWETU YATAKAVYOOZA

Magufuli alikuwa sahihi kutoa uamuzi huo kwani kwa mda mrefu TCU imekuwa ikilalamikiwa kwa kuwapangia wanafunzi kozi na vyuo ambavyo hawajaviomba. Sema hapa tatizo ni hiyo gharama ya kutuma apply, nadhani kuna haja ya kuitizima upya hiyo gharama.
 
Ee bwana eee Pombe kamwambukiza Ndalichako Ubashite.Tatizo haka kanchi ketu rahisi akijamba inakuwa branda ya perfume.Tatizo sio mfumo wa TCU tatizo ni chuki tu za Mkuu na uelewa mdogo.Yeye angesema tu kuwa Mtu akitaka kuomba directly chuoni its okay na akiomba via TCU its okay ila kama chuo hakina watu wa kutosha basi TCU inajazia.Shida hii nchi kuanzi mkuu wao mpaka Mama Ndalichako wote Mabashite.Kwa hiyo tutapiga rivasi mpaka tukabwe na mate yetu wenyewe.Ila mimi nafikiri niongee na TCU waniuzie ule mfumo wao ili niuendeshe privately.Ni fursa ya kibiashara hii....
 
Huu mfumo mpya ni mzuri sana kwanza umakupa uhakika wa kuchaguliwa chuo ulichoomba tofaut na CAS ambayo inaweza kukutema na kukwambia uchague tena na utaktana na vyuo uchwara vizuri vilishajaa, mfumo huu mpya ni mzuri sana kwani ndo unaotumika katika vyuo vikuu vikubwa duniani. Kwaio msilalamike tatizo wabongo mmezoea ktafuniwa
Wewe hujawahi tumia huo mfumo pale unachagua vyuo 3 nahisi kama hukufaulu vizuri ndo unatupwa vyuo vibovu hata ingekuwa unaomba direct chuo kama ukifeli chuo hakikuchagui
 
Mfumo wa CAS ni bora kuliko. TCU walitakiwa kuboresha baadhi ya mapungufu kuliko kuufuta. Hii ilikuwa ina amanisha at any time Wanavyuo data zao zipo TCU.
Huu mfuko wa kila mtu kufanya maombi kwenye chuo uwezekano wa mtu kupata vyuo viwili au vitatu na mwingine kukosa ni mkubwa sana. CAS ilikuwa inafanya sloting ya majina. Jina lako likishadondoka haliwezi kuonekana tena kwenye majina ya wanaofanya maombi.
Prof Ndalichako, inakuwaje utake kurudi ambapo ndipo uthibiti wa ubora wa vyuo na degree zake ulitiliwa mashaka. Inajulikana kuwa kuna baadhi za vyuo vilisajiliwa TCU bila kukidhi vigezo lakini hilo lingeweza kutatuliwa kwa kukagua raslimali watu na miundo mbinu ili wahitimu wa vyuo vikuu wafanane kwenye viwango vya taaluma zao.
Hakika mwaka huu kutakuwa na mkangajiko mkubwa kuliko. Watoto wa wakulima watahangaika sana.
mkuu mbona mile chuo cha morogoro wanadahili bila kupitia CAS?
 
Kumbuka kuwa kila chuo kina ukomo wa idadi ya wanafunzi inayoweza kudahili, sasa itakuaje mfano mtu kachagua vyuo vinne halafu kwa bahati mbaya akakosa vyote, inamaana ataanza tena kuomba vyuo vingine ambavyo hakuvipenda. Suala la kuchaguliwa na chuo au kupangiwa na tcu linaangalia sifa ya mwanafunzi mwenyewe na vigezo vya chuo..kwa hyo kwa kauli yako unakosea sana
Huu mfumo mpya ni mzuri sana kwanza umakupa uhakika wa kuchaguliwa chuo ulichoomba tofaut na CAS ambayo inaweza kukutema na kukwambia uchague tena na utaktana na vyuo uchwara vizuri vilishajaa, mfumo huu mpya ni mzuri sana kwani ndo unaotumika katika vyuo vikuu vikubwa duniani. Kwaio msilalamike tatizo wabongo mmezoea ktafuniwa
 
Watu wanamatatizo. Kwanini upangiwe chuo kikuu cha kusoma? Chagua chuo bora cha kusoma mwenyewe. Gharama kitu gani mbele ya elimu!
 
acha wabadili huo mfumo maana usajili vyuoni ulikuwa unasumbua sana wengine wamekuja sajiliwa semester ya pili mfumo ulikuwa jipu huo
 
Mnaosema wanatekeza maagizo ya Magufuli mnatumia kichwa kufikiri? Hoja ya msingi ni maamuzi sahihi au si sahihi? Naona wafia vyama wameshaleta siasa zao za chuki huku .....
Mkuu kwa hili hakuna swali. Raisi alitoa maelekezo na wote NACTE na TCU wametekeleza. Kama ni sahihi au vipi ndo hayo tunayozungumzia kwenye nyuzi hizi hapa na nyingi zaidi jukwaa la elimu. Na hili sidhani kama lina uchama ingawa wengine hupenda kugeuza kila kitu kiitikadi.
 
Binadamu sisi, mungu mwenyewe ndo anajua. Rais wako alikuwa haipendi CAS , TCU wameivunja, what if CAS inakuchagua ktk chuo usichokipenda?

Binadamu hawana shukrani mkuu wangu. CAS ilikuwa inafanya vitu vya ajabu sana. Kuna ndugu yangu aliomba masomo ya udaktari akaenda kupangiwa kozi za utalii na wakati hata hiyo kozi hakuiomba. Leo Rais ameliona hilo tatizo na amelipatia ufumbuzi lakini bado tunalalamika.
 
usipende kulalamikia jambo ambalo hujalielewa uliza hata kwa mzazi/mlezt wako!
Kwa mfumo huu mpya (?) ni rahisi kuapply hata vyuo vitatu kwa robo saa....kila chuo kina website yake na application forms zipo na applicant anakuwa na uhakika wa kufikia ndoto zake kwa kuchagua chuo akipendacho!!
Bila kubebwa na hiyo TCU wengi mtaishia mitaani dalili zipo wazi
 
Back
Top Bottom