TCU: Maombi ya kusoma "Degree" vyuo kikuu kufanyika Direct katika Vyuo husika


Tume ya vyuo vikuu nchini TCU imetangaza mfumo mpya utakaotumika kudahili wanafunzi wanaotarajia kujiunga na Vyuo Vikuu nchini kwa mwaka wa masomo 2017/2018, TCU watatumia mfumo mpya wa udahili tofauti na ule uliozoeleka wa kuchaguliwa na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU).

Haya yamebainishwa katika taarifa ya TCU iliyotolewa juzi ambapo imesema kuwa wanafunzi wote wanaotaka kujiunga na vyuo vikuu kwa mwaka wa masomo 2017/2018 watatumia mfumo mpya ambao unawataka kwenda vyuoni moja kwa moja kuomba nafasi.

Hivyo,taarifa hiyo imewataka wanafunzi waliomaliza kidato cha sita kwa mwaka wa masomo 2017/2018 kuomba nafasi ya kujiunga na vyuo vikuu moja kwa moja vyuoni kuanzia tarahe 22 Julai 2017 hadi 13 Agosti 2017.

Sifa za kujiunga kwa wanafunzi wote ni kama ifuatavyo…


 
mwaka wangu 2007 nilichaguliwa mzumbe na udsm... nikachoose mzumbe kiurahis tu..

tcu wamekuja kupiga hela tu
Fikiria tena wakati hamna CAS tulikuwa tunalipia kila app form unayochukua kwa chuo husika baada ya TCU kuja na CAS now its simple na imempunguzia sana mwanafunzi gharama..... Lakini tunawarudisha wanafunzi kwenye gharama zaidi kama zamani
 
  • Afadhali tumerudi ule mfumo wa mwanzo, kulikuwa na ukiritimba kuchagulia wanafunzi vyuo vya kujiunga.
 
Na hilo ndio tatizo la CAS, maana hao walikua allocated hapo na TCU. Ila ingekua wanawadahili wenyewe, ingefika kipindi wasitishe udahili kwenye hiyo course, na wanafunzi wapewe choices ya pili na ya tatu
Afu bado kuna mtu anasema kuwa TCU inapeleka wanafunzi kidogi kwenye vyuo baadhi( vya umma), ili vyuo vingne vipate watu (hasa private) ,

Mfumo huu wa mwaka huu utazalisha matatizo kuliko ata hayo ya CAS, tusubiri mwezi wa 11 sio mbali, tutarudi hapa kulijadili hili
 
Yes, ilifaa kuboresha ile system ya mwanzo. Hii ya CAS imekua na challenges nyingi saana kushinda ile ya mwanzo. Mpaka umeona wameamua kubadilisha usifikiri ni uamuzi wa siku moja. Imelalamikiwa saana. Wamejaribu kuiboresha kila kukicha wanaintroduce some new options, lakini bado inasumbua. Ndio maana wameiacha na kurudia ya mwanzo.
Hebu nipe baadhi ya matatizo ya CAS?
 
Fikiria tena wakati hamna CAS tulikuwa tunalipia kila app form unayochukua kwa chuo husika baada ya TCU kuja na CAS now its simple na imempunguzia sana mwanafunzi gharama..... Lakini tunawarudisha wanafunzi kwenye gharama zaidi kama zamani
Kwa hali ya maisha ya leo ambayo shule za awali tunalipa mamilioni, sidhani kama hizo application costs ni big deal kwa mtu ambaye yuko determined kupata elimu ya juu. By the way, kama unashindwa kulipia hiyo, utaweza kulipa ada? Kumbuka idadi ya wanaopata mikopo ya elimu ya juu inashuka kila kukicha.
 
Hebu nipe baadhi ya matatizo ya CAS?
Daa! Yaani zipo nyingi saana. Ya kwanza ni kuharibu notion ya the university education system. It is the kind of education system that needs only monitoring, na sio control. Ile system ilikua ina exert more of control than monitoring.
 
Na hapo naona D ni 35-39 kuanzia mwaka 2016 na kuendelea but mwaka jana nackia walisahsha 50-59 ndo D yan nchanganykiwa vbya mnooo
 
Ni utaratibu mzuri sana kwa wale wanaopangiwa vyuo wasivyovitaka.,, Na thatha ivi thjui watamlaumu nani...!! Huu ni mtego tu purposely kuua vyuo visivyo na sifa TZ...!! Ukiomba kwa hiary yako hakuna wa kukukataza

Ila wanafunzi wa Tz walivyo wa kuunga unga na ufaulu wao wakikataliwa vyuo bora ndo wengi sasa wanajazana kwenye vyuo vya uchochoroni.,, Vikipondwa wanang'aka..
 
Tanzania Commission for Universities (TCU) imetangaza rasmi kuwa wanafunzi wanaotaka kuomba chuo kwa ajili ya shahada (DEGREE STUDIES) kuanzia mwaka wa masomo huu 2017/2018 wanafunzi wawe wanaomba mmoja kwa mmoja vyuoni. Hili swala halipo sawa au huo uamuzi haupo sawa, huu uamuzi utachangia ukuaji wa rushwa katika taasisi hizi (vyuo) na kwa manaake wanafunzi wa familia za chini watakosa kwenda vyuo wavipendao kwa kukosa pesa.

Kwa nini isiwe kama NACTE? Au kwa nini TCU isiwe kama mfumo wa mwanzo?
Kauli ya Mheshimiwa Raisi wakati wa uzinduzi wa hostel za CHUO CHA MLIMANI /University of Dar es Salaam (UDSM) alisema “…TCU wawapangie wanafunzi vyuo walivyovichagua na vitavyokosa wanafunzi vitafungwa...”

Haikuwa kauli iliyolenga TCU wabadilishe Admission Procedures. Tunaomba watoe sababu kwa nini wameamua kufanya hivi na watahakikisha vyuoni hawatopokea wanafunzi wasio na vigezo.
http://tcu.go.tz/images/documents/Change_of_Admission.pdf
 

Attachments

  • Change_of_Admission_2.pdf
    86.2 KB · Views: 72
Mmhh kwa style hii...watoto wa ma prof na viongoz watajazana vyuo fulani km zamani...warudishe system ya zamani...
 
Back
Top Bottom