TCU: Maombi ya kusoma "Degree" vyuo kikuu kufanyika Direct katika Vyuo husika

Kilichofanyika sasa ni kuweka entry requirements zinazofanana kwa vyuo vyote. So kama haujafikisha entry requiremens, sidhani kama kuna haja ya kuomba vyuo vingi. Na kama uko kwenye cut off point ya entry requirement, no bora kuomba vyuo visivyo na ushindani mkubwa.
Entry requirement ni kwa total lakini kumbuka katika kila kozi kuna minimum cut points zake
Wanafunzi wengi watakosa vyuo hilo lipo wazi
 
Ni kweli ndugu. Maana kama huna vigezo, kwa nini uombe? Ile system ya mwanzo ilikua na faida zake, ila imesababisha matatizo mengi kwenye mfumo wa elimu ya juu.
System ya mwanzo ilikuwa na matatizo, huoni ni bora kuboresha kuliko kurudi kwenye mfumo wa zamani ambao ulitushinda??
 
Kulikuwa na option kwa wale wanaotaka mkopo mkuu, kama hutaki mkopo unanyoosha moja kwa moja mkuu.
Utake mkopo usitake mkopo ulikua unapitia CAS ukiacha Muslim University of Morogoro ambao mtu anaomba moja kwa moja, wakisha chagua hupeleka TCU kwa uhakiki.
 
Utake mkopo usitake mkopo ulikua unapitia CAS ukiacha Muslim University of Morogoro ambao mtu anaomba moja kwa moja, wakisha chagua hupeleka TCU kwa uhakiki.
Vyuo vyenyewe vilikuwa vinapeleka mkuu, mimi nili-apply Makumira 2012-13 direct na nikachaguliwa mkuu.
 
Kama hujui Tcu ndo walikuwa wanalimit idadi ya wanafunzi wanaochaguliwa chuo husika,so hata kama chuo kilikuwa na uwezo wa kuchukua wanafunz wengi lakin bado wasingeweza ili kuruhusu vyuo vingine vipate wanafunzi,wew unafikir ni kwanin rais amelikata hilo?
Iyo SUA unayoisema wengine ndo tupo uko, na mwaka jana kuna course zimechukua watu kuliko uwezo halisi wa chuo, mpaka waalimu wanalalamika. Sasa sijui ili unalizungumzia vipi
 
His mijitu mingine ya wapi? Mimi kama nataka kusoma mzumbe kwanini unipeleke Muccobs?
TCU ilikua haipangi mtu chuo ambacho hakuchagua, unapewa option 5, ukikosa zote unaambiwa urudie tena labda kama haukuwahi kupitia uo mfumo
 
Umeomba Mzumbe lakini ufaulu wako sio mkubwa kuliko wenzako kwa hiyo tutawachagua wenzio na wewe tutakupa room ya kuchagua vyuo vingine kulingana na ufaulu wako

Hapa ndio wabongo tunapoichukia TCU,
 
Vyuo vingi vinachukua wanafunzi wengi kuliko uwezo wake .Tunapozungumzia idadi ya wanafunzi tuzingatie miundombinu wezeshi ya usomaji

Vyuo vyetu vingi vilijengwa zamani na vilikua na uwezo wa kuaccomodate wanafunzi wachache,sasa wanafunzi wameongezeka ila miundombinu iko vile vile

Kauli kwamba vyuo vinachukua wanafunzi wachache kuliko uwezo wake si ya kweli
Unajua idadi halisi ya chuo cha udom?fuatilia
 
System ya mwanzo ilikuwa na matatizo, huoni ni bora kuboresha kuliko kurudi kwenye mfumo wa zamani ambao ulitushinda??
Yes, ilifaa kuboresha ile system ya mwanzo. Hii ya CAS imekua na challenges nyingi saana kushinda ile ya mwanzo. Mpaka umeona wameamua kubadilisha usifikiri ni uamuzi wa siku moja. Imelalamikiwa saana. Wamejaribu kuiboresha kila kukicha wanaintroduce some new options, lakini bado inasumbua. Ndio maana wameiacha na kurudia ya mwanzo.
 
Iyo SUA unayoisema wengine ndo tupo uko, na mwaka jana kuna course zimechukua watu kuliko uwezo halisi wa chuo, mpaka waalimu wanalalamika. Sasa sijui ili unalizungumzia vipi
Na hilo ndio tatizo la CAS, maana hao walikua allocated hapo na TCU. Ila ingekua wanawadahili wenyewe, ingefika kipindi wasitishe udahili kwenye hiyo course, na wanafunzi wapewe choices ya pili na ya tatu
 
hii ni njaa kwa vyuo vya private
Vyuo private vimekua vingi saana sababu ya weaknesses za hiyo system. Kama vingeachwa kwenye ushindani, wala visingekua vingi hivyo. As wanafunzi wangechagua kwenda kwenye chuo wanachoona kinafaa. Kama chuo hakijiwezi, lazima kingetoka sokoni.
 
Entry requirement ni kwa total lakini kumbuka katika kila kozi kuna minimum cut points zake
Wanafunzi wengi watakosa vyuo hilo lipo wazi
Ni kweli. Ndio kinachohitajika. Hakuna maana ya kulazimisha watu kwenda chuo wakati hawajatimu vigezo, halafu kesho kutwa tunakwenda kuwanyanyapaa huko vyuoni na makazini kwamba ni vilaza. Ni bora mtu aambiwe hana vigezo mapema ili atafute option B.
 
So hiyo system itakuaje unaenda mgu kwa mgu hadi chuon kuomba au au kutakuwa na system yao kuomba online,na je mtu atakaenda moja kwa moja chuon atatofautiana vipi na atakaeomba online?
Vyuo vingi vinaanza kuweka system ya online. Ila najua njia kubwa itakayotumika ni kudownload application form online, then unaipeleka physically au unaituma kwa sanduku la barua.
 
Serikali ya CCM imekuwa ikichezea elimu yetu miaka nenda miaka rudi huku watoto wa walalahoi wakitaabika. Shame upon crooked CCM trrany!
 
Back
Top Bottom