TCRA: Wenye akaunti ‘feki’ kukiona

TCRA: Wenye akaunti ‘feki’ kukiona

Nikitaka ku deactivate account yangu ya JF nafanyeje. Maana naona msala wanukia...teh teh teh.. Maana sipati picha mtu anakutukana tusi humu kumbe ni mtu mnaheshimiana sana mtaani
 
Mabosi wa nchi yetu mi huwaga siwaelewagi kabisa alikuja yule Jamaa yetu wa NIDA anaesurubiwa sasa hivi na mpango mzuri sana wala magu asingepata shida na mambo ya feki feki alikagua vyeti kwenye mpango wa vitambulisho vya uraia aliyoyakuta ni aibu akaambiwa huo mpango aachane nao ungeleta shida kwenye nchi hasa kwa yale ma POTI pote pote kumejaa usanii cheti kimoja mijamaa mitatu ILIKUSUDI ipate jobu watuache tuendelee na feki zetu viongozi wangapi wamejitambulisha kwa majina yao humu
 
Watawakamata wanaotumia fake ID kuikosoa serikali na CCM (in fact ni kuishauri serikali kile ambacho haipendi kukisikia) ila wenye Fake ID watakaomtusi/kejeli nk Lowasa, Mbowe, Mtatiro, CHADEMA, CUF, nk hawatakamatwa. Nani mwenye akili timamu ambaye hadi sasa hajui kwamba hizi sheria za mtandao na habari ni dhidi ya upande fulani tu?
 
Kwa hiyo kuanzia leo Nyumba Kubwa ni marufuku...sasa tunafukuzana mitandaoni...
Kwani humu JF namuibia nani na ID yangu fake?

Mimi nilidhani hiyo ibaki kwenye suala la kusajiri simu ...
Lakini kwingine itakuwa ngumu...au ndio mnatutoa kwenye hizi media kiaina...
 
Kama nilivyosema,ukijiita jina hilo kwa lengo la kuaminisha watu kwamba wewe ndiye yule mcheza filamu wa kimarekani ni dhahiri unafanya kosa lakini ikiwa ni jina lako halisi bali yamefanana tu hakuna kosa
Bora nibaki na hili jina langu halisi RIDCULOUZ
 
wadeal na mitandao ya simu ambayo inazidi umiza mnyonge
 
wanaongelea account fake au username?fake ki vipi,wabainishe hapo,kama shida Ni usernames' VP twitter na Instagram?VP humu Jamii Forums?sijaelewa ufeki VP,kumbuka facebook wamefail katika Hilo hata baada ya Kuja na mkakati mpya,labda kama kutumia jina la mtu kama lako na kujinasibisha na yeye kwa shughuli na wajihi wake,na hapo Facebook ndo ujinga huo upo kwa Sana..ila kama Ni usernames' wamebugi ramani
 
MAMLAKA ya Udhibiti wa Mawasiliano hapa Nchini (TCRA) imewaonya watumiaji wa mitandao ya kijamii wanaojisajili katika mitandao hiyo kwa kutumia majina na taarifa za uongo, anaandika Charles William.

James Kilaba Kaimu Mkurugenzi wa TCRA amesema, vitendo vya watu kujisajili katika mitandao ya kijamii kwa kutumia majina na taarifa zisizo sahihi, ni kosa kisheria na kwamba wanaofanya hivyo watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Kilaba ameyasema hayo leo, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuongeza ufahamu kuhusu matumizi sahihi na salama ya mitandao ambayo inasimamiwa na Kitengo cha dharura cha kuitikia matukio ya usalama kwenye mitandao hapa nchini (TZ-CERT).

“Tumeamua kuzindua kampeni hii ili kuwasaidia wananchi kuepuka makosa ya kimtandao na kuepuka kufanyiwa utapeli au wizi mitandaoni kwa sababu matukio mengi ambayo yamekuwa yakiripotiwa au kulalamikiwa yanazuilika kwa watu kupewa elimu ya matumizi sahihi ya mitandao,” amesema Kilaba.

Kampeni hiyo ya kuongeza ufahamu kuhusu matumizi sahihi na salama ya mitandao, itafanyika kupitia matangazo ya redio, televisheni, magazeti pamoja na mitandao ya kijamii ambapo katika mitandao ya kijamii itajulikana kama, “Darasa mtandao”.

“Miongoni mwa mambo ambayo tutawafundisha wananchi ni kutoweka wazi taarifa zao binafsi zote katika mitandao, kubadili na kutunza neon la siri (password), kutojibu ujumbe unaosema umeshinda bahati nasibu na mengineyo mengi,” amesisitiza Kilaba.
mfa maji haishi kutapatapa
 
Back
Top Bottom