barafuyamoto
JF-Expert Member
- Jul 26, 2014
- 32,405
- 29,811
Habari wanabodi,
TCRA imesikia vilio vya wadau wa simu za mkononi,taarifa za ndani zinasema kwamba kuanzia May 2015 simu yako ikiibiwa piga simu haraka sana huduma kwa wateja TCRA kuelezea upotevu wa simu yako,jambo la msingi ni kukumbuka IMEI/ESN ya hiyo simu TCRA kwa kushilikiana na mitandao ya simu wameanzisha CEIR (Bonyeza hapa Kujua maana) ambayo itakayoanza kufanya kazi May 2015.
Sasa mwizi akiiba simu yako haitofanya kazi tena chini tanzania hata wakii-flush kwa matapeli wa k/koo.Safi Sana TCRA
CEIR ni nini? Ni mtambo ambao utakuwa unafanya kazi ya kuzuia simu zilizolipotiwa kama za wizi zisiweze kukamata mtandao wowote nchini tanzania.Hii ina maanisha ukishareport upotevu wa simu na ikishakuwa blocked that means hiyo simu inakuwa Toy la kuchezea watoto.
Kwa upande mwingine inaweza kuwa pigo kwa wafanyabiashara wanaoleta simu zilizoibiwa nje ya tanzania kuja kuuza huku nchini kwetu kama TCRA wakiunganisha na CEIR za nchi nyingine maana hazitofanya kazi pia nchini.
Kumbaffu zao, tunataka watatue matatizo ya mitandao kutu-over charge, ili la wezi tunaliweza, tukikamata tunapiga kibiriti.