TCRA: Vocha za kukwangua mwisho Januari 2027

TCRA: Vocha za kukwangua mwisho Januari 2027

Atukuzwaye

Member
Joined
Oct 5, 2026
Posts
35
Reaction score
33
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetangaza mpango wa kuondoa matumizi ya kadi za kukwangua za muda wa maongezi ya simu na kuhamia katika mfumo wa kidijitali wa kuongeza salio, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuhamasisha uchumi usiotumia fedha taslimu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TCRA, zoezi la majaribio la kusitisha matumizi ya kadi hizo litaanza Januari 1, 2027, huku shughuli za uhamasishaji kwa umma zikiwa zimeanza Oktoba 1, 2026.

Zoezi hilo litafanyika katika mikoa mitano, ambapo Dar es salaam litahusisha Wilaya zote, Dodoma litahusisha Jiji la Dodoma, Chamwino, Kondoa Mjini na Kongwa, huku Arusha likihusisha Jiji la Arusha, Wilaya ya Arusha, Meru na Karatu.

Kwa upande wa Mwanza, zoezi litahusisha Nyamagana, Ilemela na Misungwi, wakati Mkoa wa Mbeya litafanyika katika Jiji la Mbeya, Wilaya ya Mbeya na Mbarali.

TCRA imesema mpango huo unalenga kuongeza matumizi ya huduma za kifedha za kidijitali, kurahisisha ununuzi wa muda wa maongezi pamoja na kupunguza uzalishaji, usambazaji na utupaji wa kadi za kukwangua ambazo zina athari kwa mazingira
TCRA 1.jpg
TCRA 2.jpg
 
Back
Top Bottom