TCRA: Tazameni radio Kwizera - Ngara

TCRA: Tazameni radio Kwizera - Ngara

Kayoka

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2011
Posts
2,406
Reaction score
2,248
Salaam Wakuu,

Sisi wakazi wa huku kanda ya Magharibi na kanda ya Ziwa tunaomba mtufikishie ujumbe MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA kuhusu namna ambavyo Radio tajwa hapo juu kuhusu mambo kadhaa; mfano-

1. Mara kwa mara huwa wanatoa matangazo ya michezo ya kubahatisha/betting (mfano alhamisi hii saa 3:05 jioni walitoa tangazo la Chezo na Ushinde na Biko licha ya kukatazwa na Mh. Rais kufanya hivyo)

2. Wamekuwa wakirusha hewani matangazo kuhusu pombe na vileo vingine ( mfano mara kwa mara wanatangaza kuhusu bia/kilevi cha Plisner King kwa uwazi uwazi)

3. Weledi na Maadili ya baadhi Watangazaji wao sio ya kuridhisha ni wa ho.vy.o kidogo kwani mara kadhaa wamekuwa wakitangaza au kusoma vitu visivyoeleweka (mfano: kushindwa kabisa kutaja kwa ufasaha majina ya miji, vitu, watu na viongozi mbalimbali).


Tafadhali TCRA chukueni hatua na simamieni maadili na maudhui ya Vyombo vya habari kama hivi.
 
Nadhani haya matangazo ya kamari yameruhusiwa au wamelegeza masharti maana hata hapa Dsm nayasikia ya Biko via EFM hasa vipindi vya michezo
 
Hizi redio za mikoani huwa zina vituko sana, hasa kwenye utangazaji na uhabarishaji wa taarifa za uhakika.
 
Radio Kwizera
Ni Ya Kanisa Catholic Ilikuwa Inawapasha Habari Wakimbizi
Hasa Warundi, Wacongo, Ndyamkama, Hata Emmanuel Buhohela Alikuwa Anatangaza Huko,
 
Bila hayo matangazo mishahara ya wafanyakazi wa hiyo radio yatatoka wapi? Naona mkuu una nongwa na Bia na kamali.....HAMIA huko Jamhuri ya Watu wa ZAnzibar maana nasikia hakuna hayo mambo!
 
Nadhani matangazo ya makampuni ya kubashiri yatakua yamerejeshwa maana nayaskia sana kwenye ivi vituo sio redio tu ata television
 
Bila hayo matangazo mishahara ya wafanyakazi wa hiyo radio yatatoka wapi? Naona mkuu una nongwa na Bia na kamali.....HAMIA huko Jamhuri ya Watu wa ZAnzibar maana nasikia hakuna hayo mambo!

Watoe matangazo yenye kuzingatia maadili sio ya Pombe na Kamali.
 
Nadhani matangazo ya makampuni ya kubashiri yatakua yamerejeshwa maana nayaskia sana kwenye ivi vituo sio redio tu ata television

Ina maana yamerejeshwa kimya kimya?

Nakumbuka hata Mh. Rais aliingilia kati kukemea haya natangazo ya Kamali, sasa kwa nini wameyarudisha tena?
 
Bia kutangazwa redioni unaona ajabu??..

Matangazo ya kamari ni kama yamerudi rasmi..

Redio za mikoani zinachukua cheap cheap labour ndo maana hawajui lolote
 
Mikoa Ya Kagera, Kigoma
Ndiyo Radio Yao Hiyo
Kutoka Ngara Kagera Tanzania
Tatizo Watangazaji Wote Ni Wa Huko Huko
 
Hivi kumbe matangazo ya pombe hayaruhusiwi nchi hii?
 
Tuko bize na clouds fm...e fm ...radio one...radio free na east africa radio maana ndo zina wasikilizaji wengi
 
Na wewe pia unatakiwa kuwekwa ndani kwa lile kosa la kuibia watu michango ya harusi!
 
Watoe matangazo yenye kuzingatia maadili sio ya Pombe na Kamali.
Pombe na kamali ndio walipaji wakubwa wa kodi wa Tanzania....tunataka kodi kwa ajili ya kujenga reli mpya ya kisasa na mradi wa umeme wa Rufiji...
 
Back
Top Bottom