Salaam Wakuu,
Sisi wakazi wa huku kanda ya Magharibi na kanda ya Ziwa tunaomba mtufikishie ujumbe MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA kuhusu namna ambavyo Radio tajwa hapo juu kuhusu mambo kadhaa; mfano-
1. Mara kwa mara huwa wanatoa matangazo ya michezo ya kubahatisha/betting (mfano alhamisi hii saa 3:05 jioni walitoa tangazo la Chezo na Ushinde na Biko licha ya kukatazwa na Mh. Rais kufanya hivyo)
2. Wamekuwa wakirusha hewani matangazo kuhusu pombe na vileo vingine ( mfano mara kwa mara wanatangaza kuhusu bia/kilevi cha Plisner King kwa uwazi uwazi)
3. Weledi na Maadili ya baadhi Watangazaji wao sio ya kuridhisha ni wa ho.vy.o kidogo kwani mara kadhaa wamekuwa wakitangaza au kusoma vitu visivyoeleweka (mfano: kushindwa kabisa kutaja kwa ufasaha majina ya miji, vitu, watu na viongozi mbalimbali).
Tafadhali TCRA chukueni hatua na simamieni maadili na maudhui ya Vyombo vya habari kama hivi.