Wana jf msidangayike na watu wanaotumia mtandao huu kutisha watanzania.
Ndani ya tanzania sheria zinafuatwa kikamilifu na tcra pamoja na mitandao yote na watoa huduma mbalimbali za "vas" wanafuata taratibu zilizowekwa na tcra kikamilifu.
Kumekuwa na ujumbe unaosambazwa unaosema:
"tuma neno hapana kwenda 15016 uone maajabu" huku wengine wakisema mitandao na ccm zinachukua fedha za wateja kwa wizi - yaani ujanja ujanja.
1. Hii namba ni ya bure hai chaji hata sent moja - jaribu ukikatwa nenda kadai utarudishiwa hela yako
2. Hii ni namba ya mawasiliano.
3. Ukituma neno ccm au chochote - utaambiwa asante kwa kujiunga.
4. Ukituma neno ndio - utaambiwa "asante kwa kujiunga na huduma hii ya changia ccm na ushinde zawadi kati ya pikipiki 64, baiskeli 200 na millioni 45 kutoka ccm. Kujitoa tuma neno hapana kwenda 15016"
5.ukituma neno hapana - utaambiwa asante kwa ujumbe wako, utaondolewa kwenye huduma hii ya changia ushinde na ccm.
Tcra na mitandao vinajua hii namba inafuata sheria zote ndio maana haitahangaika na wazushi wasio fikiria bali kuropoka ropoka tu. Hawa inabidi tcra na polisi iwashughulikie kwani ni kosa la jinai kuanzisha false panic alerts kwa jamii.
Lakini pia kumbuka kila unapotuma neno lolote kwenye namba hiyo tayari unakua kwenye database ya ccm. Wakikutumia ujumbe wowote rpomosheni au mawasiliano usije lalamika maana umeingia anga zao.
Kumbuka haya majibu yote yamewekwa kwenye computer na inakujibu kufuatana na ulicho andika.
Guys hakuna wizi hapa - acheni kudanganya watu bure.
Vinginevyo baada ya kutuma neno lolote kwenye hiyo namba, nenda tcra na majibu uliyopata ukashtaki, kama watakuuliza ulifuata nini kwenye hiyo namba na unataka wakusaidie je.