kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,317
- 12,617
Vyombo vya habari redio na tv havipaswi kuwa na ratiba za vipindi vyao zinazoonyesha muda na siku? Kama zipo ratiba ni nani anapaswa kuhakikisha kuwa ratiba hizi zinafuatwa na vyombo vya habari ili kuwalinda wasikilizaji na watazamaji wa vipindi vyao?
Mfano, Redio inasema watakuwa na taarifa ya habari saa 1 asubuhi au michezo saa 2 usiku au magazeti saa 3 asubuhi, mlaji anasubiri taarifa ya habari isomwe saa 1 asubuhi lakini redio au tv inasoma taarifa hiyo nusu saa baada ya muda wa kipindi kupita, hii inaleta usumbufu mkubwa kwa wasikilizaji na watazamaji ambao wanataka kusikiliza kipindi husika ambacho kimecheleweshwa kuanza bila taarifa kwa walaji kuwa kipindi kitachelewa kutokana na sababu fulani.
Na mara nyingi kipindi kinachelewa kwa mambo ya kipuuzi kabisa. Nchi inaonekana kuwa haijali muda wa wananchi unaopotezwa na vyombo hivi vya habari.
Je, TCRA hamlioni hili hili? Je, kila chombo cha habari kinajiamulia tu ratiba yake? Je, mnasema nini kuhusu usumbufu huu kwa wananchi?